Lihakanga
JF-Expert Member
- Dec 17, 2016
- 4,829
- 6,376
Nianze kwa kuaema sipingi imani za dini za watu wala chama cha siasa. Ninaandika kile ambacho nimekiona kwenye maisha toka nikiwa mdogo.
Nikiwa mdogo, miaka ya mwisho ya 70 hadi miaka ya 80, nilizoeakuona mikusanyiko ya watu kwa kigezo cha sikukuu au sherehe fulani za kisiasa au kidini.
Kwa mfano, sikukuu za kidini kama mwaka mpya, pasaka, watakatifu wote na krismas, na zile za kisiasa kama sabasaba, Muungano, Uhuru nk zilipewa uzito na msukumo mkubwa na viongozi husika.
Sijazungumzia sikukuu za kiislamu kwa kuwa ninaona kama bado wana utamaduni wa kukusanyika kwenye matukio yao.
Lakini kadri ninavyoishi ninaona upungufu mkubwa sana wa kukusanyika kwa watu katika matukio haya.
Siku hizi hata kuja kwa kiongozi wa chama au serikali mahali fulani, viongozi wenyeji wanatumia nguvu kubwa sana kuwalazimisha watu waende kwenye tukio ikiwemo kufunga milango ya biashara na kuahirisha matukio ya kijamii ili tu watu wote waelekee kumpokea kiongozi huyo.
Kilichonifanya niandike ni hali ya leo. Niko zangu kijijini huku. Kumedorora hatari. Hakuna amsha amsha kama ni xmas. Watu wengi wako mashambani kama siku tu ya kazi ya kawaida.
Yale mambo ya kuvaa nguo mpya hayaonekana sana. Na msukumo wa kuhudhuria ibada umepungua sana nikilinganisha na zamani.
Hii ni ishara ya nini? Watu wamebadili mtazamo? Hakuna umuhimu tena wa kuheshima sikukuu hizi kama zamani? Hakuna umuhimu wa kuwapokea na kuwasililiza viongozi kama zamani?
Inakuwaje siku hizi hata Rais akienda mahali fulani, viongozi wa sehemu husika hukodi hata magari kusomba watu wakusanyike kumsikiliza Rais?
Mbunge akipanga ziara kwenye jimbo lake, anaweza akutane na wazee wachache na viongozi wa chama na serikali amabao nao huenda kwa kuhofia kumulikwa.
Je kama hali itaendelea kuwa hivi, huko tuendako nini kitatokea?
Ninawatakia Xmas njema.
Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app