Sikukuu zinapoteza thamani

Sikukuu zinapoteza thamani

Kwa hiyo miaka wengi tuliokuwa tunasherehekea tulikuwa sisi (watoto) leo ni watu wazima tuna familia zetu kule vijijini tumehama leo tupo maeneo tofauti na tuna majirani wenye tamaduni tofauti na na zetu so huwezi kutegemea kuyaona leo hayo.

Mimi kuna wakati nilienda makwetu nikashangaa hakuna watoto wenye harakati kama tulizokuwa tukizifanya zamani (japo watoto wapo na siyo wengi but wapo tofauti sana na kizazi chetu)
 
Wewe hutumii akili kufikiri

Kuna maendeleo makubwa ya teknolojia hasa simu na computer

Kila kitu utakacho unakipata online

Sasa miaka hiyo watu wangapi Tanzania walikuwa na Television au Computer

Wewe umezaliwa wakati wa ujima enzi za maisha ya giza

Unataka watu watembee tembee hovyo barabarani kisa x mass

Wewe uliishi maisha ya disko vumbi tena sio disko bali ngoma za kienyeji

Jaribu kufikiri nje ya box mkuu

Unataka turudi miaka ya 80 watu shule hawavai viatu na anayevaa watu wanamshangaa
Licha ya yote uliyosema, bado mleta uzi ana hoja sikukuu na sherehe zimekosa hamasa mfano rahisi kabisa ni pale JPM alipofuta hafla za kusheherekea uhuru na kuelekeza fedha zitumike kuleta maendeleo.

Kwa mfano huo nadhani hali ya kiuchumi inachangia sana hii hali.
 
Nianze kwa kuaema sipingi imani za dini za watu wala chama cha siasa. Ninaandika kile ambacho nimekiona kwenye maisha toka nikiwa mdogo.

Nikiwa mdogo, miaka ya mwisho ya 70 hadi miaka ya 80, nilizoeakuona mikusanyiko ya watu kwa kigezo cha sikukuu au sherehe fulani za kisiasa au kidini.

Kwa mfano, sikukuu za kidini kama mwaka mpya, pasaka, watakatifu wote na krismas, na zile za kisiasa kama sabasaba, Muungano, Uhuru nk zilipewa uzito na msukumo mkubwa na viongozi husika.

Sijazungumzia sikukuu za kiislamu kwa kuwa ninaona kama bado wana utamaduni wa kukusanyika kwenye matukio yao.

Lakini kadri ninavyoishi ninaona upungufu mkubwa sana wa kukusanyika kwa watu katika matukio haya.

Siku hizi hata kuja kwa kiongozi wa chama au serikali mahali fulani, viongozi wenyeji wanatumia nguvu kubwa sana kuwalazimisha watu waende kwenye tukio ikiwemo kufunga milango ya biashara na kuahirisha matukio ya kijamii ili tu watu wote waelekee kumpokea kiongozi huyo.

Kilichonifanya niandike ni hali ya leo. Niko zangu kijijini huku. Kumedorora hatari. Hakuna amsha amsha kama ni xmas. Watu wengi wako mashambani kama siku tu ya kazi ya kawaida.

Yale mambo ya kuvaa nguo mpya hayaonekana sana. Na msukumo wa kuhudhuria ibada umepungua sana nikilinganisha na zamani.

Hii ni ishara ya nini? Watu wamebadili mtazamo? Hakuna umuhimu tena wa kuheshima sikukuu hizi kama zamani? Hakuna umuhimu wa kuwapokea na kuwasililiza viongozi kama zamani?

Inakuwaje siku hizi hata Rais akienda mahali fulani, viongozi wa sehemu husika hukodi hata magari kusomba watu wakusanyike kumsikiliza Rais?

Mbunge akipanga ziara kwenye jimbo lake, anaweza akutane na wazee wachache na viongozi wa chama na serikali amabao nao huenda kwa kuhofia kumulikwa.

Je kama hali itaendelea kuwa hivi, huko tuendako nini kitatokea?

Ninawatakia Xmas njema.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Ukiona sikukuu imepoteza thamani jua tayari umekuwa mtu mzima.
 
Kwanza ushazeeka tulia. Pili mambo yakuvaa sijui nguo mpya kupika pilau nk ile ilikuwa kipindi nchi ni maskini.

Siku hizi kila ijumaa biriani halafu jumapili pilau pombe pia ni kila mtu anapojisikia.

Kuvaa nguo mpya sikukuu sio dili tena watu wamejaza nguo kwenye kabati kibao

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Hao mabwashee labda pale Wami River uondoe lile daraja.

Jamaa wana utamaduni wao wa kipekee sana
Moja ya 90 nilikua naona watu wanavyokuja nyumbani mamia kwa mamia , miaka ya 2000 kuja huku tulipo inapungua sana, hususani mwaka huu wa 2023 upungufu ni mkubwa na mno, wengi tupo nao hapa mjini na hata ile magari kujaa na kukosa nafasi mwaka huu hamna, sio muda kule watakata .
 
Pia ujamaa unapungua, Sikukuu za zamani zilikuwa zinaunganisha ndugu na jamaa... Lakini siku hizi watu hawaharikani kwenye sikukuu kama zamani... Hii inapelekea jamii kukosa ushirikiano na kila mtu kusherehekea kivyake, kipindi tunakua sisi sikukuu ilikuwa ni jambo la jamii, yani mkijua fulani leo yeye hana ratiba ya msosi au hayuko vizuri basi mnamuharika au kumpelekea msosi.

Hivyo hivyo kwa Dini tofauti, Muislamu alikuwa anaharikwa na mkristo kwenye Christmas na Mkristo anaharikwa na Muislamu kwenye Idd... Ndio maana jamii za zamani zilikuwa na ushirikiano sana, siku hizi kila mtu na mambo yake
 
Nianze kwa kuaema sipingi imani za dini za watu wala chama cha siasa. Ninaandika kile ambacho nimekiona kwenye maisha toka nikiwa mdogo.

Nikiwa mdogo, miaka ya mwisho ya 70 hadi miaka ya 80, nilizoeakuona mikusanyiko ya watu kwa kigezo cha sikukuu au sherehe fulani za kisiasa au kidini.

Kwa mfano, sikukuu za kidini kama mwaka mpya, pasaka, watakatifu wote na krismas, na zile za kisiasa kama sabasaba, Muungano, Uhuru nk zilipewa uzito na msukumo mkubwa na viongozi husika.

Sijazungumzia sikukuu za kiislamu kwa kuwa ninaona kama bado wana utamaduni wa kukusanyika kwenye matukio yao.

Lakini kadri ninavyoishi ninaona upungufu mkubwa sana wa kukusanyika kwa watu katika matukio haya.

Siku hizi hata kuja kwa kiongozi wa chama au serikali mahali fulani, viongozi wenyeji wanatumia nguvu kubwa sana kuwalazimisha watu waende kwenye tukio ikiwemo kufunga milango ya biashara na kuahirisha matukio ya kijamii ili tu watu wote waelekee kumpokea kiongozi huyo.

Kilichonifanya niandike ni hali ya leo. Niko zangu kijijini huku. Kumedorora hatari. Hakuna amsha amsha kama ni xmas. Watu wengi wako mashambani kama siku tu ya kazi ya kawaida.

Yale mambo ya kuvaa nguo mpya hayaonekana sana. Na msukumo wa kuhudhuria ibada umepungua sana nikilinganisha na zamani.

Hii ni ishara ya nini? Watu wamebadili mtazamo? Hakuna umuhimu tena wa kuheshima sikukuu hizi kama zamani? Hakuna umuhimu wa kuwapokea na kuwasililiza viongozi kama zamani?

Inakuwaje siku hizi hata Rais akienda mahali fulani, viongozi wa sehemu husika hukodi hata magari kusomba watu wakusanyike kumsikiliza Rais?

Mbunge akipanga ziara kwenye jimbo lake, anaweza akutane na wazee wachache na viongozi wa chama na serikali amabao nao huenda kwa kuhofia kumulikwa.

Je kama hali itaendelea kuwa hivi, huko tuendako nini kitatokea?

Ninawatakia Xmas njema.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Maarifa yameongezeka siri zinafichuka Kila siku!

Huwezi mdanganya Tena mtu mwenye akili timamu eti hii no Xmass,huu ni mwaka mpya na hiyo no pasaka akakuelewa!!

Siri zimefichuka kuwa Kuna makanisa na viongozi wake ushoga kwao no sawa Leo nani atamheshim padri,askofu kadinali na papa!!?

Makanisa kama uyoga na tote yana make money !

Nani utamdanganya eti hivi au vile!!?

Sikukuu nazikumbuja miaka ya tisini huko mitaa ya RTC Bunda enzi za power Mabula siku ya mwaka mpya Raha sana!

Sasa hivi ubwabwa na maharage mchungu Tena haunukii na kuwa mtamu kama zamani!!
 
Leo nani atamheshim padri,askofu kadinali na papa!!?
Papa noma Ila sio kosa lake amezaliwa December 17, 1936, akiangalia Argentina wanaume wanaolewa akiangalia huko kwenye wanasema wao ni nchi ya ahadi waisrael nao wanaume wanaolewa akaona ngoja atembee na huo upepo kumbe akasahau Africa alipokuja aliishia Congo DRC tu
Screenshot_20231226-155206.png
 
Ukiona sikukuu inapoteza thamani jua umeshakuwa mhenga...
 
Nimekaa nikaangalia sikukuu za siku hizi zimepungua mvuto zamani kipindi Kam hichi ilikuwa hela hela mtaani jingle bell kila nyumba au ni sehemu Mimi ninapokaa

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Kwa sababu umri wako umesogea tu. Kwa watoto wadogo sikukuu bado zipo vile vile
 
Back
Top Bottom