Sikukuu Njema Ndugu zangu wa JF

Sikukuu Njema Ndugu zangu wa JF

Dharra

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2017
Posts
1,661
Reaction score
2,975
kwenye simu nikiwa kwenye corridor za posta mpya. Mimi: Boss njaa inanisumbua naenda kula kwanza
Boss: Ukitoka kula nenda kajiandae na safari ya dodoma kesho
Mrembo kisu ile mbaya akiwa karibu yangu. Mrembo: eeeeh!!! nilivyokusikia kwenye simu si unaweza kula hata mbuzi mzima
Mimi: HAbari yako mamii ni kweli nahisi njaa sana karibu tukapate msosi.
Mrembo: Akuu naogopa
Mimi: Kama unaogopa poa mimi naenda kula mbuzi mzima
Mrembo: Unaenda Resta gani hapa
Mimi: Leo naenda pale Holiday inn
Mrembo: Poa tuunganishe
Msosi wa watu 2 pamoja na mazagazaga zikanitoka 35,000 cash haina shida
Mimi: Nampungia mkono muhudumu aje kufata hela (alishaniwekea invoice)
Muhudumu: cashier anakuita
Nimenyanyuka kwenda kwa cashier
Cashier: Mambo vipi? hujambo wewe?
Mimi: Poa vipi mrembo? za siku mbili tatu
Cashier: Poa tu za kutukimbia
Mimi: Salama tu nimefurahi kuwaona tena, nilisafiri kidogo
Cashier: Poa. Nilitaka tu kukwambi, dada uliekaa nae namfahamu ni malaya mnoo mnoo ni bora ukatafuta mwengine
Mimi: Umemfahamuje?
Cashier: Yule anaishi kawe na anauza nyago Mediterraneo. Mi naishi Kawe pia na hiko kiwanja mimi na hubby wangu ndio mapumziko yetu. Kweli yule binti ni mrembo mnooo na ndio maana wengi wananasa pale.
Mimi: Duuh!!!
Cashier: Huwa anawauzia wazungu na mapedeshee na watu wanasema keshaumia tiyari:
Mimi: Simjui ndo nimekutana nae muda huu kibahati tuu na sikuwa na nia mbaya ingawa kama mwanaume tamaa zilishaanza kunipanda, ila ahsante sana kwa kunipa tahadhari.
Mrembo: Ulikuwa unaongea nini na cashier?
Mimi: Nilikuwa namsalimia unajua mimi sometimes hapa ni kijiwe changu na hivi siku nyingi hawajaniona ndo hivyo alikuwa ananiulizia kulikoni.
Mrembo: Ohhh! poa.
Tumemaliza kula maongezi ya hapa na pale tukirudi usawa wa posta saa nane na kitu
Mrembo: Nimeshiba sasa hapa nipambane na usafiri wa Kawe
Mimi: Kwani Bajaji hapa ni bei gani
Mrembo: Hata buku 15 anakupeleka lakini mimi na prefer zaidi boda boda ndio fasta
Natoa tena mwekundu kumsaidia usafiri
Mrembo:Ahsante. Boda Bodaaaaaa
Mrembo: Kesho zamu yangu kukupa offer ya lunch ingawa sio Holiday Inn, unatumia namba gani ili nikutafute kesho?
Mimi: Ahsante lakini haitosaidia, kesho ninasafiri Dodoma na nikirudi tu nasafiri nje na tayari nina tiketi mkononi. Ahsante kwa company yako
Mrembo: Jamaniiiii wee nipe tu!!
Huku nikipambana na shetani kijasho chembamba kinanitoka kuashiria vita kali kati yangu na shetani,mimi nisimpe shetani mpe.
Mimi: NIkitembea kwa haraka kuelekea usawa wa Benjamin Mkapa tower. Bye mamii mara ingine.
Nilirudi Holiday inn. Baada ya maongezi marefu na cashier nilithibitisha maelezo yake na hivyo cashier aliniepusha na kikombe kikubwa. moral of the story club ama Bar ama cocobeach sikukuu hii kuvinjari ama siku nyengine yoyote msisahau kuwafanyia wema wahudumu kwa angalau kuwaachia senti kidogo ipo siku usioijua wanaweza kuwa msaada mkubwa kwako. Pia inajenga undugu na urafiki baina yenu. Nikutakieni Sikuuu njema na mapumziko mema ninyi na familia zenu.
 
Back
Top Bottom