SIKUJUA:sehemu ya tatu
Mwandishi:shamsi shabani
Ilipoishia.... Kabla sijamjibu ili bidi nijiulize... Sawa nitampeleka je ana nauli??? au wanafahamiana na hao madereva??? au ana ndugu huku??? lakini Kama ana ndugu huku siangenda huko na si kwangu ......
JIMWAGE NAYO SASA
****************
ilikuwa ni mida ya saa mbili nikiwa nakatiza Katiza chocho za mtaa wetu nikirudi nyumbani ama getoni kwangu
Nikitokea standi baada ya kumpeleka Yule dada nilie msaidia usiku wa Jana...... nilitimiza ombi lake lakuniomba nimpeleke standi kuu yakuelekea mkoni kwao kwakuwa nilipokuwa mimi na kwao si mbali sana ni Kama kutoka Dar es Salaam na kwenda morogoro tu
Basi nikiwa njiani naelekea pangoni kwangu nilikuwa nikifikiria nifanye nini siku ya Leo maana ni wikiendi na siku hizi mbili huwa tunapumzika kwenda kazini
Cha kwanza nilichofikiria ni kwenda kumtembelea kodraki lakini kitu ambacho kilionekana kuwa tatizo nitava nini!!!! Sio kwamba Sina nguo ila ni chafu Sana maana Sinaga muda wakufua siku za kazi....
Basi wazo lakumtembelea kodraki likawa limeyeyuka palepale wazo lililokuja kwa kasi kichwani ni kufua nakufanya usafi pale pangoni kwangu
Kutokana na mwendo lilokuwa nao na mawazo ya hapo na pale nilijikuta nampamia mama wa watu bahati mbaya na ndiye alienitoa katika fikra zangu za mipango ya Leo baada yakuongea kwa hasira.... Watu wengine bwana wanajifanya wanamawazo.. Kwahiyo tuseme hujaniona!!!!??? Sikuwa na jibu lakumjibu ila nilimuomba msamaha tu japo hakuelewa Sana ila ndio yalisha hivo.... Baada ya hapo ili nibidi nipunguze fikra zinazonifanya nijisahau Kama nipo njiani basi sikuchukua muda mrefu nikafika nyumbani kwangu japo napenda kuita pango maana haina hadhi yakuitwa nyumba......
Kwakuwa tayari nilishapanga chakufanya kilichofuata ni utekelezaji tu nilikusanya nguo zangu chafu zote nakuzitoa nje nikaziweka chini ya mti wenye kimvuli kizuri kabisa maji hayakuwa tatizo katika kijiji chetu chakuongezwa hapa ni sabuni tu
Nilienda dukani nikanunua sabuni yakutosha ata hivo nilikuwa na bahati Sana kuwa karibu na duka maana kuna watu wengine hutembea mwendo mrefu mpaka kufikia duka.....
Nilianza kufua nikijifariji kwa nyimbo maana rundo languo nilokuwa nao lilikuwa linakatisha tama na sio wingi wanguo tu pia zilikuwa ni chafu sana maana kuna zingine zilikuwa zimerudiwa kuvaliwa............
***********
Katika familia hii yakitajiri mambo yalikuwa yanazidi kuwa magumu ni sawa nakulazimisha maji yapande mlima
Mama shiny sasa alianza kupungua kidogokidogo sikwamba alikuwa ni mgonjwa ila tu ni mawazo mengi ndio yaliomfanya awe katika hali hiyo maana hakuwa na jibu sahihi kuhusu mtoto wake
hii hali imekuwa na mkanganyiko maana wakisema watangaze mtoto wao amefariki itakuja kuwaletea shida Kama siku akija kupatikana kwahiyo walibaki njia Panda nakufanya familia hii kuwa katika mzozo kila kukicha.......
Mama shiny alikuwa akimlaumu sana mumeo kwanini hampati mtoto wao utafikiri anajua alipo!!
Leo mama shiny alionekana kuwa mwenye huzuni sana kupita siku zote mpaka baba shiny alivorudi kutoka kazini alimshanga nakumliza... Mama shiny vipi unaumwa tuende hospitali!!!!?? kabla hajajibiwa baba shiny aliendelea kuongea lakini mama shiny mbona uko hivo mbona kila siku nakuambia upunguze mawazo siunaona mpaka umeugua sasa.... Baba shiny aliongea utafikiri mama shiny kishamjibu....... Mama shiny alijibu kwamba haumwi ila anamuwaza mtoto wake nakuongeza maneno makali yaliyomkera baba shiny...... Wewe siunanenepa tu huna mawazo na mtoto wako acha mimi nikonde kwa sababu ndiye nilie uona uchungu....baba shiny kwasasa hayo maneno alikuwa ameyazoea alichokifanya alinyanyuka nakuingia chumbani kwake
Lakini sasa nayeye alionekana kuanza kuingiwa na hofu zaidi maana siku zina zidi kwenda na wametumia njia zote kumtafuta mtoto wao wakipeke lakini hazija zaa maua wala matunda.....
Ooh my daughter where are you!!??? Baba shiny aliongea peke yake chumbani......
**********
Baada yakufua Sana nikajikuta nachoka ghafla nakujisemea peke angu... Kwani lazima nimalize zote!!!!
hazikuwa nguo nyingi ila nilikuwa nimechoka sana baada yakukatiza zoezi la kufua nilihamia ndani kidogo nisafishe na humo kwakuchoka kule nilijikuta nafanya Kama nimelazimishwa na kama ningekuwa nimeajiriwa basi nilikuwa sina changu
Nilimaliza kufanya usafi ilikuwa ni saa saba nilikuwa nanjaa sana kwakuwa nilikuwa nimechoka sikuweza kupika nilienda mgahawani nikala nikarudi nyumbani kupumzika kidogo...
**********
Mama,,Baba watakuwa katika hali gani wazazi wangu hawajui nilipo pia hawajui Kama nipo hai ama lah!!,,,shiny alikuwa akiwaza sana
Tayari alikuwa kwenye basi linaloekea mkoani kwao hatujui katumia mbinu gani kupanda katika basi hilo na Kama mjuayvo makondakta huwa hawamwachi mtu wanamna hii hivihivi bila yakumpa maneno machafu na kejeli na kumsukumilia mbali..........
Usikose kufuatilia simulizi hii sehemu ya nne.......