Sikujua kama ndio ulikuwa unaniaga na ulikuwa unaenda kufia mikononi mwa mama yako

Jplus Jr

Senior Member
Dec 29, 2018
124
147
Awali ya yote nianze kwa kutoa pole zangu kwetu watanzania wenzangu kwa kuondokewa na aliyekuwa Rais wetu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Joseph Magufuli. Hiyo ndiyo njia yetu kila mmoja ataipitia kwa wakati wake.

Baada ya pole hizo nije katika mada: Wiki 3 zilizopita nilikuja humu kuomba ushauri na msaada kwenu kwa magumu ninayopitia.

Kwa uchache tu kwa wale ambao hawakujua ilikuwa hivi: Mm ni kijana wa kiume wa miaka 27 nakaa mbezi Dar. Nilipanga chumba kimoja mm na mke wangu tukiwa na mtoto mchanga.

Haukuwa wakati sahihi wa kuishi na mke kwangu lakini baada ya kubeba ujauzito na mazingira aliyokuwa nayo sikutaka kumtelekeza ilinibidi niishi nae.

Awali nilikuwa nafanya kaz kwa mtu aliyekuwa katuajiri vijana 8. Baadae hali ya biashara kama mjuavyo iliyumba na kupelekea malipo kuanza kusumbua ingawa malipo pia yalikuwa kidogo sana, hali iliyopelekea boss kupunguza baadhi ya wafanyakazi.

Miongoni mwa waliopunguzwa kazi ni mm pamoja na wenzangu 3. Hapo maisha yakaanza kuwa magumu kuliko hata awali. Ilinibidi sasa niwe natoka asubuhi kwenda kutafuta vibarua huko ili jioni naporud basi niwe na chochote kwaajili ya familia.

Baadae mke wangu aliugua na ni kipindi ambacho nilikuwa nakaribia wiki kila nikitoka kwenda kutafuta kibarua chochote sipati kitu, kama tujuavyo hivi vibarua hali ya sasa kuna kupata na kukosa.

Maisha yale yalinikosesha hata pesa ya kumpeleka mke wangu kwenye matibabu, nilikuwa mtu mwenye mawazo sana, nilijaribu kuomba ushauri kwa watu wachache lkn wengi wao walikuwa wakinushauri niitelekeze familia, kitu ambacho sikuwahi kukifikiria kwani niliipenda sana familia yangu licha ya hali tuliyo nayo.

Ndiposa nikaja humu kuomba ushauri na ikiwa kuna mtu ana kibarua chakufanya huko basi mm niko tayari kufanya ilimradi tu kiwe kibarua halali, yote hayo ni ili familia yangu ipate kula na nipate pesa ya matibabu kwa mke wangu.

Namshukuru Mungu wako wachache kwa kidogo walichokuwa nacho walinisaidia na wengine walinitia moyo ingawa wapo pia walioniahidi, kuwatafuta wakanipotezea. Ila katika yote namshukuru Mungu kwa wote waliojitoa kwa namna moja ama nyingine kunisaidia na kunitia moyo, nawaombea mibaraka tele toka kwa Mungu.

Basi hatimaye nilimpeleka mke wangu hospitali akapimwa na kupewa matibabu. Na namshukuru sana Mungu aliendelea vzr.

Wiki moja baadae mama mkwe alimuita aende nyumban kupumuzika, kwao ni Igunga Tabora. Yeye na mm sote tuna mzazi mmoja tu mama baba zetu walishatangulia mbele za haki.

Kwa vile mama mkwe maisha yake nayo ni sawa tu na ya mama yangu nilimwambia mama hata nauli tu kwa sasa sina atakujeje huko? Alinijibu Atakopa hata hela aje, basi kwa vile mama mkwe aling'ang'ania nikasema sawa.

Wiki mbili baadae mke wangu aliugua tena, hela ya kumpeleka hospital kule ikawa hamna, niliendelea kutafuta vubarua ili nipate chochote nitume aende hospital, Mungu akasaidia nikapata kidogo nikawa nimetuma wakampeleka hospital.

Jana tarehe 24 nilipigiwa simu hali yake ilibadilika, nikiwa nachekecha akili namna ya kwenda, usiku wa kuamkia leo tarehe 25 nikapewa taarifa za kulala mauti kwa mke wangu. Nimeumia sana, kaniacha peke yangu na mwanetu mchanga aliyekuwa bado anahitaji kunyonya maziwa ya mama yake, huku pia nikiwa bado sijasimama kiuchumi.

Umeniachia mapambano magumu peke yangu mke wangu kipenzi, lala salama tutakutana paradiso.

Nimeona nilete mrejesho ndugu zangu maana tulilianza hili sote. Bado nipo na sijui nini chakufanya nimempoteza mke, kaniachia mtoto mchanga na bado hali yangu kiuchumi haijatengemaa, sijui nini chakufanya.

Ikiwa una ushauri wowote kwangu na kutiana moyo tuwasiliane kwa No 0742843490.
 
Doh Ina sisimua na kusikitisha .rest in peace
ikulu_mawasiliano-20210323-0001.jpg
 
daahhh pole sana mungu akupe nguvu.

ndio maana y kuzaliwa mwanaume jikaze sana.

Mimi pia nimetandikwa na misiba mingi ndani ya mwezi huu!!nimefiwa na aunt zangu wawili sijakaa sawa mama akaanza kuumwa ghafla naye akafariki!!ila sababu ni kazi ya mungu haina makosa inabidi upokee tuu
 
Awali ya yote nianze kwa kutoa pole zangu kwetu watanzania wenzangu kwa kuondokewa na aliyekuwa Rais wetu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Joseph Magufuli..
Pole sana na Mungu akupe wepesi katika kipindi hiki. Hakuna msiba mdogo kaka ila tumshukuru Mungu kwa kila jambo na Muombee sana mtoto wako kwani ndiyo faraja namba moja. Ukiwa unamshukuru Mungu waombee pia wale wazazi waliopoteza watoto wa nne kule Dar kwa mara moja.
 
Hakika unapitia mtihani mgumu sana mkuu,-usife moyo Mungu mkubwa kiongozi wangu.

Amani ya Mungu idumu kwako-idumu na kwa wengine pia....pole sana....pumzika kwa amani shemeji yetu.
 
Pole sana.

Japo maelezo hayajitoshelezi kushawishi watu kutoa chochote kitu hasa ukizingatia dunia ya sasa matapeli wana mbinu zao zenye akili sana.
Mimi sijaisoma mkuu, vipi anataka hela au 🤔
 
Unaweza wiwa kusaidia kwa chochote ulichonacho. Ila tushaumizwa sana na dunia hii kiasi kwamba jani likitikisa tu mguu tunakimbiza.

Ila pole sana mkuu kwa matatizo haya
 
Unachosema uko sahihi kabisa, licha ya kunipa hela ila ikiwa ulipo kuna kazi au kibarua chochote cha kufanya mm niko tayari ilimradi tu kiwe halali. Sibagui kazi niniyo na uwezo nayo wa kuifanya.
Pole sana.

Japo maelezo hayajitoshelezi kushawishi watu kutoa chochote kitu hasa ukizingatia dunia ya sasa matapeli wana mbinu zao zenye akili sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom