Sikudai mama

Sikudai mama

Bukya

Senior Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
196
Reaction score
121
Mtoto mmoja alimwendea mama yake akampa kipande cha karatasi ambayo alikuwa ameandika madai yake
Ulinituma kukata nyasi Sh. 2,000
Kwa kusafisha chumba changu wiki hii Sh.1,000
Kwa kwenda kununua vitu sokoni 1,000
Kwa kufagia uwanja Sh. 2,000
JUMLA NAKUDAI SHILINGII ………6,000.

Mama yake naye alitafuta karatasi na kuandika:


Kwa miezi tisa niliyokubeba tumboni . HAKUNA MALIPO.
Kwa nyakati zote za usiku nipokosa usingizi nikikuhudumia, HAKUNA MALIPO
Nilikufulia nguo zote chafu. HAKUNA MALIPO.
Nilikutoa makamasi. HAKUNA MALIPO.
Nilikupikia chakula. HAKUNA MALIPO.

Ukijumulisha hayo yote jibu lake HAKUNA MALIPO.
Kijana alichukua kalamu na kuandika. SIKUDAI MAMA

 
Back
Top Bottom