Siku ya Wajinga tuwe makini sana

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,469
3,342
Siku kama hii nakumbuka miaka 15 iliyopita kuna Dada yangu mmoja alipigiwa simu na kuambiwa aende kwenye interview ya kazi fulani hivi aliyokuwa akiifuatilia.

Siku kama hii na mwezi huu alipopigiwa simu aliondoka na kwenda Posta ya zamani wakati huo katika jiji la Mindule. Alipofika ofisini aliwakuta wanaka wengi tu nao wakiwa kwenye foleni wakidai na wao walipigiwa simu kama yeye kwenda kwenye interview.

Walikaa hapo huku wakipiga stori za hapa na pale kama tunavyofahamu kabla ya interview watu wanapokuwa nje huwa na muda wa kupeana chai kidogo huku wakishusha na wengine kupandisha kimuhemuhe au kimwemwe.

Wakati wakiwa kwenye foleni baada ya nusu saa kupita bila kuona chochote ukiendelea mmoja wao kwenye foleni alijisikia kutoka kwenye foleni na kutembeatembea kidogo akamfyata mlinzi na kumuuliza taratibu kwa upole kabisa na aliniuliza swali hili."..habari Kaka hivi leo kuna zoezi la interview hapa kweli?.

Yule mlinzi alimjibu kwa sauti ya kuning'oneza akamwambia Dada niliwaona sana tangu nafika hapa na sikutaka kuwaambia chochote ila kwa kuwa wewe umekuja ngoja nikuambie ukweli kuwa hapa hakuna taarifa hiyo na ninadhani leo ni siku ya wajinga hivyo basi nakushauri ukitaka kujiridhisha saini kwenye kitabu cha wageni nenda ofisi ya mapokezi pale watakujulisha na ukishapewa taarifa sahihi rudi nyumbani kimyakimya ukaendelee na majukumu yako, pole sana Dada yangu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom