Uchaguzi 2020 Siku ya uzinduzi wa kampeni kwa upande wa CHADEMA Dar es Salaam kutafurika umati wa watu haijawahi kushuhudiwa tangu tupate Uhuru

Wakuu kwema!

Siku ya uzinduzi wa kampeni, siku ambayo Mh. Tundu Antipas Lissu atatema madini adimu bila kumung'unya maneno.

Mimi binafsi nitahudhuria, umati utakaoshuhudiwa siku hiyo utakuwa mkubwa sana. Watumishi walioongopewa mishahara minono watatoroka kazini kwenda kupata tumaini, wafanyabiashara walioteswa na TRA watafunga biashara zao kwenda kula neno la tumaini.

Vijana waliokosa ajira ambao wengi wako hapa Dar es Salaam hawatakosa.

Itakuwa aibu kubwa kwa CCM, chama ambacho rushwa ni halali. CCM nao watawazoa wajumbe na UVCCM kwa ujira wa elfu tano ili wakasikilize mambo ya ununuzi wa Bombardier, SGR na viwanda zaidi ya elfu 8 na ajira hewa zaidi ya milioni sita.

Najua wapo watakaokuja na kauli za umati wa mikutanoni si kitu. Lakini mutambue kuwa CHADEMA haisombi watu kwa malori kisha kuwalipa sahani ya ubwabwa na sh.elfu tano, watu wataacha kazi zao willingly ili wakamsikilize watakayempigia kura mheshimiwa Lissu ambaye hatumii nguvu kujibrand.

Kama umati sio issue mbona akina johnthebaptist na wenzake wanateseka kila wanapoona Lissu analakiwa kama mfalme kila anakokwenda!
HIVI UCHAGUZI WA 2015 DSM NANI ALIPATA KURA NYINGI CCM AU CDM?
 
Watu wanaenda kwenye mikutano ya chadema kupata burudani jinsi viongozi wa chama wanavyopayuka na kufika, ukweli wataupata siku ya kupiga kura na msije singizia umeibiwa sababu kwenye kampeni watu walikuwa wanaacha kazi wanakuja kuwasikiliza.
 
Back
Top Bottom