Siku ya tatu nitavaa gunia, nitajipaka majivu na nitafunga kuiombea nchi yangu

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
SIKU YA TATU NITAVAA GUNIA,NITAJIPAKA MAJIVU,NITAFUNGA KUIOMBEA NCHI YANGU TANZANIA.

Leo 23:30pm 18/04/2020

Katika vita hakuna mtu atakae kwambia kitu cha kufanya kuokoa maisha yako,hasa kwa adui asiye onekana,

In the War,you dont argue ,nobody asks anyone to stay indoors, rather you thank God for seeing another day in the Land of the living,and you Pray to see another day,by His grace,May His Will be done.

Nimechagua kumuomba Mungu kwa kufunga,niseme tu kufunga ni kitendo kinachotoka rohoni na sio mwilini. Hivyo kwa jinsi mtu atakavyoguswa moyoni au atakapoona yeye mwenyewe umuhimu wa kufunga kwa ajili ya vita iliyo mbeleni basi na afanye hivyo,

Kufunga kunaweza kuwa kwa kuomba neema na rehema za Mungu,kuomba toba pengine kutokana na gonjwa hatari linaloshambulia nchi mfano tauni wakati wa Mfalme Daudi na corona hivi sasa,

Au ugumu wa hali fulani anayopitia katika ulimwengu ambamo kila kitu kinaanzia upande wa kiroho na Kushinda au kushindwa kunaanzia rohoni,Sasa haja yako unayotaka kupeleka kwa Mungu, ndipo unapolazimika kujichagulia mwenyewe aina ya maombi au ufungaji wako utakaoendana na haja zako.

Kulingana na vita ya corona kama adui asiyeonekana,na kwa kuona vita kubwa mbele yetu na kutaka kufahamu mambo gani yatakayokuja kutokea huko mbeleni,

Imenilazimu nifunge siku ya tatu ya kuliombea Taifa letu la Tanzania, pasipo kula chakula kitamu wala kujipaka mafuta,kadhalika na kujipaka majivu mwili mzima na kuvaa gunia kama ishara ya toba mbele za Mungu wetu ili aweze kuiponya Tanzania.

Rejea habari ya Musa, kwa kuwa alifahamu anakwenda kukutana na uso wa Mungu na kupokea amri za Mungu kule mlimani ilimlazimu afunge siku 40 usiku na mchana bila kula chochote,

Pia wakati wa Esta wayahudi walipoona wanapitia hatari ya kuuawa walifunga siku tatu usiku na mchana bila kula chochote,

Kadhalika na wengine mfano Nehemia, Daudi, Mitume Pamoja na Bwana wetu Yesh Kristo hata yeye wakati wa kwenda kujaribiwa na shetani nyikani alifunga siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa chochote,hii ni vita na adui hatumuoni, imenilazimu kutumia silaha ya kiroho ambayo haionekani,nami nitafunga kuomba toba na rehema kama Baba yangu Daudi alivyofanya.

Je nifunge vipi!?

Wapo wengine wanaweza kufunga pasipo kula chakula wala maji kwa siku kadhaa, wapo wengine wanafunga kwa kutokula chakula walichokizoea, mfano walikuwa wanakula nyama mara mbili kwa siku, wanaamua kujinyima kwa kutokula chakula kitamu kama nyama kwa muda wa labda mwezi mmoja hivi au zaidi wanakuwa wanakula tu pengine maji na mkate basi.

Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.

Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;

Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.

Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.

Hata Mungu atakapoliepusha janga la corona hata sasa akiwa tayari ameshaliepusha kiroho bado kutokea duniani ambapo tunasubiriwa sisi wanadamu kusema Amina na janga la corona litafutika juu ya nchi.

Itakuwa siku takatifu ya Bwana yenye heshima; tukiitukuza, kwa kuwa hatukuzifanya njia zetu wenyewe, wala kuyatafuta yatupendezayo, wala kusema maneno yetu wenyewe;

Ndipo itakapokuwa furaha katika Bwana; Mungu atatupandisha mahali pa nchi palipoinuka; atatupa urithi wa Abrahamu,Isaka na Yakobo baba zetu, kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo.

Niwatakie mfungo mwema tunapo malizia siku hii ya tatu ya maombi ya kitaifa ili Mwenyezi Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo atuepushe na mauti ya ugonjwa wa corona na kuenea kwake.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
 
.
Isaya 58:5-12
Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?
6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
9 Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;
10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
11 Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
12 Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Isaya 43:22-26

22Lakini hukuniita, Ee Yakobo, bali umechoka nami, Ee Israeli.
23 Hukuniletea wana-kondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani.
24 Hukuninunulia manukato kwa fedha, wala hukunishibisha kwa mafuta ya sadaka zako; bali umenitumikisha kwa dhambi zako, umenichosha kwa maovu yako.
25 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

Mungu anatupenda upeo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mathayo 6:5-14
5“Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao. 6Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango, kisha umwombe Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
7“Mnaposali, msipayuke maneno kama watu wasiomjua Mungu. Wao hudhani kwamba Mungu atawasikiliza ati kwa sababu ya maneno mengi. 8Msiwe kama wao. Baba yenu anajua mnayoyahitaji hata kabla ya kumwomba. 9Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali:
‘Baba yetu uliye mbinguni:
Jina lako litukuzwe.
10Ufalme wako ufike.
Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
11Utupe leo chakula chetu cha kila siku.
12Utusamehe makosa yetu,
kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
13Usitutie katika majaribu,
lakini utuokoe na yule Mwovu.’ [
Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
14“Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nyinyi pia. 15Lakini msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe nyinyi makosa yenu.

Kuhusu kufunga
16“Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni kweli, hao wamekwisha pata tuzo lao. 17Wewe lakini unapofunga, paka kichwa chako mafuta, nawa uso wako, 18ili mtu yeyote asijue kwamba unafunga, ila ujulikane tu kwa Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.

Aisee nakusii acha Siasa kwenye masuala ya dini
 
Huyu mzee wa Iringa alishakutangulia kimawazo
FB_IMG_15872305984921112.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIKU YA TATU NITAVAA GUNIA,NITAJIPAKA MAJIVU,NITAFUNGA KUIOMBEA NCHI YANGU TANZANIA.

Leo 23:30pm 18/04/2020

Katika vita hakuna mtu atakae kwambia kitu cha kufanya kuokoa maisha yako,hasa kwa adui asiye onekana,

In the War,you dont argue ,nobody asks anyone to stay indoors, rather you thank God for seeing another day in the Land of the living,and you Pray to see another day,by His grace,May His Will be done.

Nimechagua kumuomba Mungu kwa kufunga,niseme tu kufunga ni kitendo kinachotoka rohoni na sio mwilini. Hivyo kwa jinsi mtu atakavyoguswa moyoni au atakapoona yeye mwenyewe umuhimu wa kufunga kwa ajili ya vita iliyo mbeleni basi na afanye hivyo,

Kufunga kunaweza kuwa kwa kuomba neema na rehema za Mungu,kuomba toba pengine kutokana na gonjwa hatari linaloshambulia nchi mfano tauni wakati wa Mfalme Daudi na corona hivi sasa,

Au ugumu wa hali fulani anayopitia katika ulimwengu ambamo kila kitu kinaanzia upande wa kiroho na Kushinda au kushindwa kunaanzia rohoni,Sasa haja yako unayotaka kupeleka kwa Mungu, ndipo unapolazimika kujichagulia mwenyewe aina ya maombi au ufungaji wako utakaoendana na haja zako.

Kulingana na vita ya corona kama adui asiyeonekana,na kwa kuona vita kubwa mbele yetu na kutaka kufahamu mambo gani yatakayokuja kutokea huko mbeleni,

Imenilazimu nifunge siku ya tatu ya kuliombea Taifa letu la Tanzania, pasipo kula chakula kitamu wala kujipaka mafuta,kadhalika na kujipaka majivu mwili mzima na kuvaa gunia kama ishara ya toba mbele za Mungu wetu ili aweze kuiponya Tanzania.

Rejea habari ya Musa, kwa kuwa alifahamu anakwenda kukutana na uso wa Mungu na kupokea amri za Mungu kule mlimani ilimlazimu afunge siku 40 usiku na mchana bila kula chochote,

Pia wakati wa Esta wayahudi walipoona wanapitia hatari ya kuuawa walifunga siku tatu usiku na mchana bila kula chochote,

Kadhalika na wengine mfano Nehemia, Daudi, Mitume Pamoja na Bwana wetu Yesh Kristo hata yeye wakati wa kwenda kujaribiwa na shetani nyikani alifunga siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa chochote,hii ni vita na adui hatumuoni, imenilazimu kutumia silaha ya kiroho ambayo haionekani,nami nitafunga kuomba toba na rehema kama Baba yangu Daudi alivyofanya.

Je nifunge vipi!?

Wapo wengine wanaweza kufunga pasipo kula chakula wala maji kwa siku kadhaa, wapo wengine wanafunga kwa kutokula chakula walichokizoea, mfano walikuwa wanakula nyama mara mbili kwa siku, wanaamua kujinyima kwa kutokula chakula kitamu kama nyama kwa muda wa labda mwezi mmoja hivi au zaidi wanakuwa wanakula tu pengine maji na mkate basi.

Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.

Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;

Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.

Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.

Hata Mungu atakapoliepusha janga la corona hata sasa akiwa tayari ameshaliepusha kiroho bado kutokea duniani ambapo tunasubiriwa sisi wanadamu kusema Amina na janga la corona litafutika juu ya nchi.

Itakuwa siku takatifu ya Bwana yenye heshima; tukiitukuza, kwa kuwa hatukuzifanya njia zetu wenyewe, wala kuyatafuta yatupendezayo, wala kusema maneno yetu wenyewe;

Ndipo itakapokuwa furaha katika Bwana; Mungu atatupandisha mahali pa nchi palipoinuka; atatupa urithi wa Abrahamu,Isaka na Yakobo baba zetu, kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo.

Niwatakie mfungo mwema tunapo malizia siku hii ya tatu ya maombi ya kitaifa ili Mwenyezi Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo atuepushe na mauti ya ugonjwa wa corona na kuenea kwake.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
Wee Endelea tu na upopompo wako. Utapigwa miti na mapepo hapo ndio utajua Mungu hadhihakiwi
 
Sijawahi kusikia wala kuona mfanya toba au sala.ya dhati akijitangaza na kutangaza aina ya sala au toba anayofanya na namna anavyoifanya.

BADO HATUJAIONA HASIRA YA BWANA
 
Kama una allergy na majivu au nyuzi za gunia angalia usije ukawashwa au kuugua ngozi ukatumia pesa kutibiwa pesa ambayo ungeweza kuwapa wahitaji
 
Corona haiwezi kuondoka Kwa mikwala ya kuvaa gunia ebu acheni UJINGA na huo ni unafiki Tu wa kujifanya mnajua kuomboleza.

Kuna magonjwa kibao yanaitesa DUNIA mbona hatujawasikia mnavaa magunia??
 
Back
Top Bottom