Nilianza kusikiliza radio nikiwa na miaka 10 tu kipindi hiki ndipo nilipoanza kukariri majina ya watangazaji wa radio mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Nilipofikisha miaka 13 nilikuwa nikimwibia baba radio yake ndogo nakwenda nayo mtaani mpaka alipoamua kuniachia radio hiyo.
Radio ya kwanza kwa kununua kwa hela yangu niliinunua nikiwa na miaka 15 tu kijijini huko nililima mpunga nikapata gunia moja nilipouza nikanunua radio kimbembe ikawa kupata hela ya betri.
Nilikuwa betri zikikaribia kuisha naishiwa raha kabisa mpaka mzee akawa ananunua Catone nzima ya betri ananipa sita zangu na yeye anatunza sita.
Baadae nikahakikisha naanza kufuga kuku ili niweze kufinance radio yangu hapo nikawa nimepatia sikuteswa tena betri.
Leo ni miaka 23 sasa tangu nianze kusikiliza radio ambayo kwangu ni ngumu sana kuishi bila kusikiliza radio.
Sipendi kuangalia television ila radio ni lazima nisikilize siku asubuhi mchana na jioni.
Hapa nilipo nimetune EA radio 88.1 FM nasikilizia gnoma ya Bele 9.
Radio for life.
Sent using
Jamii Forums mobile app