Siku ya Redio Duniani: Je, ni sahihi kwa wasio na taaluma ya habari kutangaza?

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,591
20,748
Amani kwako.

Dunia inaadhimisha uwepo wa utoaji wa habari duniani kupitia redio na siku ya tarehe 13.02.2020 tunaadhimisha Siku ya Redio.

Toa maoni yako juu ya siku hii, ikiwa ni pamoja kuangazia tasnia hii ya redio inayoongozwa na waandishi wa habari:

- Kwa sasa imeingiliwa na watangazaji wengi wasio na taaluma ya uandishi wa habari.

- Serikali ya Tanzania kuwataka watangazaji wasio na elimu ya uandishi wa habari kutafuta au kuongeza elimu.
 
cloudstv_B8fmVqapltz.jpeg
 
hivi mi sijui ni lini nilisikiliza redio, yani niache kuangalia watu wakituliwa vichwa uko nisikilize #WasafiFM
 
Dah aise bora leo ni Siku ya Redio Duniani. Kuna redio ipo kwetu huku inaitwa Ice FM Makambako kuna watangazaji wanaboa kiukweli wpo wawili ni ndugu wafamilia moja taaluma ya hiyo kazi hawana walianza na uDJ waka jipenyeza mpaka kuwa watangazaji kamili yani mtu anacho elezea hakieleweki tayar kipindi kimekwisha.
 
Nilianza kusikiliza radio nikiwa na miaka 10 tu kipindi hiki ndipo nilipoanza kukariri majina ya watangazaji wa radio mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Nilipofikisha miaka 13 nilikuwa nikimwibia baba radio yake ndogo nakwenda nayo mtaani mpaka alipoamua kuniachia radio hiyo.

Radio ya kwanza kwa kununua kwa hela yangu niliinunua nikiwa na miaka 15 tu kijijini huko nililima mpunga nikapata gunia moja nilipouza nikanunua radio kimbembe ikawa kupata hela ya betri.

Nilikuwa betri zikikaribia kuisha naishiwa raha kabisa mpaka mzee akawa ananunua Catone nzima ya betri ananipa sita zangu na yeye anatunza sita.

Baadae nikahakikisha naanza kufuga kuku ili niweze kufinance radio yangu hapo nikawa nimepatia sikuteswa tena betri.

Leo ni miaka 23 sasa tangu nianze kusikiliza radio ambayo kwangu ni ngumu sana kuishi bila kusikiliza radio.

Sipendi kuangalia television ila radio ni lazima nisikilize siku asubuhi mchana na jioni.

Hapa nilipo nimetune EA radio 88.1 FM nasikilizia gnoma ya Bele 9.

Radio for life.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bonge La Experience Mkuu

Nimeacha kusikiliza radio baada ya kuwa na wimbi la watangazaji uchwara waliokosa weredi na skills za utangazaji.
Sasa mpaka "lokole" mtangazaji, seriously?? Hii tasnia imevamiwa kweli.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom