Ikiwa ni Siku ya Redio Duniani, ni Redio ipi au mtangazaji gani unamkumbuka?

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Mimi naikumbuka Channel Africa idhaa ya Kiswahili kutoka Afrika kusini miaka ya 1993 hadi 1997 hivi. Ilitisha sana hii redio. Nawakumbuka watangazaji km Jenny Zondo (Marehemu) na Mike Alelengi. Hii ndo redio pekee iliyokuwa inashika vzr bila mikwaruzo.

Zamani usikivu wa redio nyingi ulikuwa wa taabu sana. Kipindi hicho muziki wa Afrika kusini ulikuwa juu saba.Ni kupitia redio hii ndo tulikuwa tukisikiliza nyimbo za Luck Dube i.e (Remember me), Ivon Chaka chaka (Mama land), Brenda Fessie, Chicco nk. pamoja na habari mbalimbali za kimataifa. Sina hakika km bado iko hewani. Nai mic sana hasa ule mlio wa ndege kabla ya kuanza kipindi.

Daah! time really flies
 
Mimi naikumbuka Channel Africa idhaa ya Kiswahili kutoka Afrika kusini miaka ya 1993 hadi 1997 hivi. Ilitisha sana hii redio. Nawakumbuka watangazaji km Jenny Zondo (Marehemu) na Mike Alelengi...
Safi kweli!Jane Zondo na Mike Araleng walikuwa vizuri.Sikujua kama Jane Zondo amefariki.Alale mahali pema,aamin!🙏
 
Watu na kumbukizi zenu!
Hivi hiyo Radio (RSA) iliacha kusikika mwaka gani?

Maana ilipoingia teknolojia ya mitandao, radio nikazifungia masanduku, zipo zinanyewa mende tu.
 
Nakumbuka kipindi cha redio one cha nani zaidi na kipindi kile cha ladha 10 za bongo ya radio one vilisababishwa niwe nachapwa mara kwa mara nimekumbuka mbali sana
 
Julius nyaisanga mambo mseto. Jumapili saa 5-6. Radio one stereo. Mauongo yaliyofanana na ukweli yalikuwa ya kutosha aisee.
 
Back
Top Bottom