Hebu ushughulishe kidogo ubongo wako kufikiri!! Hebu tutafakari sasa>-
-Wiki mbili kabla ya kifo anapumulia mashine
-Madaktari walitambua ukimwondolea mashine, moyo unasimama na ndiyo mwisho wa uhai wake
-Familia ililidhia mashine zizimwe kwa mgonjwa wao maana hakukua na kuokoa maisha yake tena
-Kwa tamaduni zetu taarifa za msiba hazitolewi tu kiholela, mpaka uhakikishe unapozitoa kila kitu kipo kwenye order..
-Hata wewe ukifiwa na mtu wako wa karibu, watu hawawezi kukurupuka tu kukwambia, lazima wajirdhishe kama akili yako iko sawa na unaweza kuhimili taarifa hizo.
Nadhani kwa sasa si muhimu kujua Nyerere alikufa lini, labda ningekuelewa ungehoji chanzo na sababu za kifo chake ili tujue kama kweli it was a natural death!!.. So far tutumie muda huu kujitathmini kama Nyerere angekuwepo, CCM ingechakachua Katiba yetu, Mafisadi wangekiteka nyara chama chake, tembo wetu wangeuwawa hovyohovyo, vipi madini na gesi yetu ingetumikaje, Viwanda alivyoanzishwa vingekuaje?
Hayo ndo mambo ya msingi ya kuyatafakari