Siku ya kwanza

Siku ya kwanza

Bangi mbaya kuna mwehu miaka michache iliyopita alisababisha mti kukatwa baada ya kudai ameona nzi anapiga ngoma. Mzazi wake akashauriwa na mganga akate mti uliopo uwandani kuna vitu kwenye huo mti ndio vinamzingua kijana. Waliomshawishi kuvuta waliposikia hizo habari wakacheka sana. Na mwingine nae alihangaika kutundika nguo kwenye msumari kumbe ni nzi ametua ukutani sio mzumari. Mjinga mwingine alitoka na taa ya chemli usiku wa manane nje kusubiria mpita njia ili aombe kibiriti awashe sigara. Mzembe mwingine ya alitoka na tochi mchana kweupe ameiwasha akielekea msalani.
 
Hizi bange hatariiiiii.
Kuna jamaa ye siku ya kwanza mchana kweupe tena jua kaliii,alikuwa akikiogopa na kukikimbia kivuli chake.
Ganja ganja ganjaa.
 
Back
Top Bottom