Siku ya kwanza kuamkia kwenye nyumba yako, furaha yake usipime!

Miaka mi5 ulikuwa unajenga Ghorofa? Kama nyumba zetu hizi ramani kidole ni ndani ya miezi 6 tu ushamaliza!
 
Wakuu, ninakuja kwenu kijana ninayetaka kumiliki mjengo!

Nina mil 8! Kiwanja ninacho chanika! Kipo tambarare ardhi ni Mchanga.

Mchanga roli la 15m3, ni 250,000, maji yapo karibu Ni kufunga tape tu.

Nyumba ya sebule, master, jiko, store.. njoo Cha ndani Cha kawaida.

Kwa pesa hiyo naweza kujenga Boma, kuezeka, plaster, na kufunika paa pamoja na milango na madirisha ya grill?
 
Wakuu, ninakuja kwenu kijana ninayetaka kumiliki mjengo!
Nina mil 8! Kiwanja ninacho chanika! Kipo tambarare ardhi ni Mchanga...
Hapana utalipua... kama huna dharura sana jenga taratibu nyumba yako ...finishing ya nyumba ni gharama ..nenda taratibu utakapoishia pumzika, vuta pumzi then endelea utapata nyumba nzuri sana
 
Umaskini ni pale kijana anapowaza kujenga nyumba badala ya biashara
Akili zetu zina shida kubwa sio kidogo
 
Nilikuwa na akili kama zako mpaka pale nyumba niliyopanga ilipouzwa bila mimi kupewa taarifa na nikiwa bado na mkataba!! aliyenunua akaja na vyombo vyake anataka kuingia ndani .. kesi zikaanza na amani ikatoweka ..muda wa kwenda kazini we unaenda kumsubiri mwenyekiti wa serikali za mtaa kusikiliza shauri lenu.. mwenyekiti naye keshapewa cha juu anakuambia bora utafute nyumba nyingine.. ukirudi home wife anakuuliza vipi mmefikia wapi.. ukitazama dogo anacheza na wenzake nje kwa furaha hajui kama pale sio kwao tena!!.. acha kabisa!..
Dah pole sana hiyo stress yake sio ya kitoto bora ukaishi kwenye nyumba yako ambayo haija Isha kuliko fedheha kama hiyo
 
Nilikuwa na akili kama zako mpaka pale nyumba niliyopanga ilipouzwa bila mimi kupewa taarifa na nikiwa bado na mkataba!! aliyenunua akaja na vyombo vyake anataka kuingia ndani .. kesi zikaanza na amani ikatoweka ..muda wa kwenda kazini we unaenda kumsubiri mwenyekiti wa serikali za mtaa kusikiliza shauri lenu.. mwenyekiti naye keshapewa cha juu anakuambia bora utafute nyumba nyingine.. ukirudi home wife anakuuliza vipi mmefikia wapi.. ukitazama dogo anacheza na wenzake nje kwa furaha hajui kama pale sio kwao tena!!.. acha kabisa!..
Umeongea kwa hisia na nimekuelewa sana mkuu. Ukweli lazima usemwe, nyumba ya kupanga huwezi kuwa na amani, ni kheri gharama kubwa ya usafiri lkn nipo kwangu
 
Sikupingi ndg lakini tuna vitu pia sisi tunashindwa kwenda navyo tunapokuwa kwenye nyumba za watu,,watu kutaka kuishi kama waonavyo wao na si kama mwenye nyumba atakavyo au taratibu zake zilivyo,,wengi wetu tunataka tujiendeshe kama vile uko kwako! Hapana!

Wengi wetu hata vikazi vidogo tu vya nyumbani hatutaki kufanya,,na hatuwezi kuchukuliana na mazingira mapya.. Mim nililelewa na baba mdogo na mama mdogo (RIP Mama), niliwakuta wakiwa na bint wa Kazi tu na nikaendelea kuishi hapo tangu mdogo,,mama alikuwa very straight na nilijitaidi kushi vizuri.

Alikuja bro mmoja alishindwa kwa sababu ambazo mim naziona ni ujinga tu,,Kazi za walezi wetu waliokuwa wanalazimika kurudi jioni Sana,,sasa jamaa yeye hata akiwa yupo home hawezi fanya chochote jikoni anamsubiri mama maana Kuna kipindi mfanya Kazi aliondoka...hii mama mlezi hakuivumilia kbs..jamaa nae anapanda juu kwamba yeye mwanaume hawezi pika n.k mwisho aliondoka...

Majuzi Nina mdgo wangu kbs upande wa mke wangu,,Mungu wa rehema ametusaidia tuko kwetu,,sasa jamaa hataki kuchota maji na eneo niliko maji hayajafika,,yaani mtu ananuna Sana akipewa Kazi kusaidia,,

Hitimisho langu sisi tunakoaa kwa watu tujitaidi kwenda na mazingira ya nyumba husika,,wachache wenye kuonea...let's be smart.
Fact kabisa hii. Unapoishi endana na mazingira ya mahali husika. Kipimo cha utu ni kazi, ikiwa mtu hataki kazi basi huyo hana utu, hafai kuishi naye
 
Mkuu, nimekuelewa sana na umesema ukweli asilimia

Siwez kujisifia jns navoishi hapa kwa watu ila mm n mchapa kazi sana (kuna usemi unasema yatima hadeki) huo usemi kwangu ndio unaoniongoza tangu nlipoanza kuishi kwa watu ila kuna baadhi ya mambo inakubid uyafanye ht kama utanuna au hupendi n lazima ufanye tuu

Nikikuambia hapa nlipo watoto wa mwenye nyumba wanafuliwa ad chupi na wao wapo degree mwaka wa mwisho huu(mwanamke) na mwingine ndo anaanza degree mwaka huu (wakiume) utakubali.?
Hiyo ni shida! Kufuliwa chupi graduate?
 
Umaskini ni pale kijana anapowaza kujenga nyumba badala ya biashara
Akili zetu zina shida kubwa sio kidogo
Nilidumbukiza 30M kwenye biashara, biashara imekufa within 3 years, na nyumba sina. Heri hiyo pesa ningeanza kujenga nyumba sasa hivi ningekuwa na mahala pangu pa kujisitiri ndio nianze kuhangaika na biashara.
 
Umaskini ni pale kijana anapowaza kujenga nyumba badala ya biashara
Akili zetu zina shida kubwa sio kidogo

Biashara sio kwa kila mtu! Mwingine hiyo pesa ataipeperusha asubuhi kabla jogoo hajawika.
Mtu anaweza kujenga nyumba yenye thamani kubwa lakini sio kwamba alikua na hiyo pesa yote kwa mara moja.
Kwa mfano huyu jamaa kajenga kwa miaka mitano, unaweza kukuta alianza kujenga akiwa na milioni moja au mbili.
Akajichanga kidogo kidogo tena akaendeleza hadi kuja kukamilisha. Usimlaumu sana ila wewe unaweza kuweka ushuhuda wako hapa kama ambavyo yeye ametuletea wake wa maamuzi ya kujenga.

kitu nakubaliana nawewe ni kwamba wengi wetu hatuna elimu ya uwekezaji/ Biashara.
 
Back
Top Bottom