Siku wananchi wakichoka kipigo cha askari, nini kitatokea?

Siku wananchi wakichoka kipigo cha askari, nini kitatokea?

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,767
Reaction score
288,340
Mtatiro.jpg

Julius Mtatiro

Posted Jumapili,Februari1 2015


Na Julius Mtatiro


Kwa ufupi
Lengo la makala hii ni kuonyesha tatizo hili linaloendelea kukua na kushauri hatua za kuchukua. Ni kweli kabisa kuwa nchi yoyote inakuwa na vyombo vyake vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kulinda mipaka ya nchi na hata hali ya amani ndani ya nchi yenyewe. Askari hawa huwa katika makundi tofauti na kazi tofauti kila mara. Kwa mfano, askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) huwa na jukumu la kulinda mipaka ya nchi. Majeshi mengine kama vile Polisi, Magereza, JKT n.k huwa na kazi maalumu ya kulinda amani ndani ya nchi. Wanajeshi mara zote hufunzwa mafunzo muhimu na hukanywa dhidi ya matumizi ya nguvu huku wakijulishwa kuwa siri ya mafanikio ya askari ni kuwa karibu na wananchi wa kawaida.

Matukio ya vyombo vya ulinzi na usalama kunyanyasa raia yamekithiri nchini kwetu. Raia wamekuwa wakinyanyaswa, wakiteswa, wakitishwa, wakiumizwa na mara nyingine kupoteza maisha kutokana na kipigo kutoka kwa vyombo vya dola au hata kupata ulemavu wa kudumu katika miili au akili kwa sababu ya kujeruhiwa vibaya na askari wetu.

Lengo la makala hii ni kuonyesha tatizo hili linaloendelea kukua na kushauri hatua za kuchukua. Ni kweli kabisa kuwa nchi yoyote inakuwa na vyombo vyake vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kulinda mipaka ya nchi na hata hali ya amani ndani ya nchi yenyewe. Askari hawa huwa katika makundi tofauti na kazi tofauti kila mara. Kwa mfano, askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) huwa na jukumu la kulinda mipaka ya nchi. Majeshi mengine kama vile Polisi, Magereza, JKT n.k huwa na kazi maalumu ya kulinda amani ndani ya nchi. Wanajeshi mara zote hufunzwa mafunzo muhimu na hukanywa dhidi ya matumizi ya nguvu huku wakijulishwa kuwa siri ya mafanikio ya askari ni kuwa karibu na wananchi wa kawaida.

Kwa mfano, Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania yalipoingia Uganda kumfukuza Idd Amin Dada yalipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wa kawaida yalifurahiwa sana na hivyo yalipewa kila taarifa muhimu za kupambana na adui. Askari wa jeshi lolote lile wanapokuwa hawana maelewano na raia huangukia mikononi mwa maadui kirahisi. Kwa hiyo, majeshi yote duniani hivi sasa yanajenga mikakati na maboresho makubwa ya kuwa "rafiki wa raia" na yanafanya kila yawezalo ili kukubalika kwa raia kwa lengo la kurahisishiwa kazi ngumu ya kulinda na kufuatilia masuala ya usalama.

Vyombo vyetu vya dola vimekuwa mstari wa mbele kunyanyasa na kuonea raia, kuwapiga, kuwadhalilisha na kutweza utu wao, kuna matukio kadhaa yanathibitisha hali hii:

Vurugu za gesi Mtwara

Januari hadi Mei mwaka 2013 kulikuwa na hali ya kutoelewana mkoani Mtwara. Wananchi waliandamana wakitaka majibu kutoka kwa mamlaka husika juu ya masuala ya gesi inayochimbwa mkoani humo. Wananchi waliona kuwa, ahadi zote zilizotolewa na Serikali hazijatekelezwa na badala yake Serikali imeanzisha mpango wa kusafirisha gesi kupeleka Dar es Saalam bila kuwajulisha wananchi uamuzi huo na una faida na hasara gani kwao. Maandamano yale yalipoanza Serikali ilituma askari jeshi wakatulize raia bila kuwekeza nguvu kwenye majadiliano na hatua za kistaarabu. Tulichokishuhudia Mtwara baada ya hapo ni wananchi kuteswa.

Sekeseke la gesi liliisha huku kuna raia wakiwa na vilema vya kudumu, watu karibia 12 walifariki dunia na miundombinu mbalimbali kuharibiwa. Wananchi mara zote hupenda maswali yao yajibiwe kwa wakati hasa kama yanahusu jambo lenye masilahi, na Serikali kwa kawaida huwa haitaki kutoa majibu hayo kwa wakati kuogopa kujichanganya kwa sababu haifanyi kazi kama timu. Wananchi wanaponyimwa majibu huanza viashiria vya kuchukua hatua mkononi na hata Serikali za mikoa na serikali kuu zinapoona viashiria hivyo, mara zote hazichukui hatua ya kupeleka ujumbe mzito wa viongozi ili wakae na viongozi wa wananchi na hata wananchi wenyewe ilimradi jambo lifafanuliwe na makubaliano ya msingi yafanyike, la! Mara zote serikali ikiona viashiria tu vya wananchi kudai jambo lao tena kwa maandamano ya amani kinachofuatia ni kutuma askari ili wananchi wapigwe na kukamatwa, wateswe na wakomeshwe.

Njia hii ya Serikali nyingi za Kiafrika na hususan Tanzania ni "njia ya kipofu", maana haisaidii kitu, inawafanya wananchi wawe sugu, wazoee kupigwa, wajenge uadui na serikali na vyombo vyake, wasiwe wazalendo na waaminifu kwa taifa lao na inawafanya wananchi waone kama viongozi ni madikteta wasio na huruma hata kidogo. Wananchi wakijenga imani hii dhidi ya serikali na vyombo vyake na kisha ikaachwa iendelee kukomaa, tunajiandalia bomu zito siku za usoni ambalo likilipuka hakuna atakayejiokoa. Nasema hivi kwa sababu ni hatari sana kuwazoesha wananchi "usugu", kuzoea mateso na kuonewa, kuichukia serikali na vyombo vyake n.k. maana wananchi ni wengi mno kila mahali na siku wakichoka hali hii ya kuonewa na kutwezwa, sote hatutakuwa salama.

Kuuawa kwa Daudi Mwangosi - Iringa

Tabia ya vyombo vya dola kutumia nguvu bila sababu katika mambo ambayo yanahitaji busara na mazungumzo ya kawaida ilikuwa sababu kubwa ambayo baadaye ilipelekea matumizi makubwa ya nguvu na kuuawa kwa Mwangosi. Daudi Mwangosi aliuawa Septemba mwaka 2012 akiwa katika majukumu yake ya uandishi wa habari. Eneo alilouawa huko mkoani Iringa lilikuwa na shughuli za kisiasa za Chadema.

Pamoja na Mkuu wa Polisi wa Wilaya kuruhusu shughuli za Chadema ambazo zilikuwa ni pamoja na ufunguzi wa matawi, Mkuu wa Polisi wa Mkoa alizuia shughuli hizo zisiendelee (jambo ambalo ni kinyume na sheria na ni nje ya mipaka ya kazi yake.

Wakati viongozi na wanachama wa Chadema wanatembelea vijiwe na ofisi kadhaa kufungua matawi yao, Polisi kwa maagizo ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa waliamua kutumia nguvu kuwatawanya na kuwakamata wananchi waliohusika katika tukio lile. Hapa ndipo Mwangosi alipolipuliwa na bomu ambalo mpaka leo halijulikani ni la aina gani. Mwili wa mwandishi huyu kijana ulisambaratika vipandevipande, baada ya hapo Serikali ilianza kutoa taarifa za kila namna za kujitetea na kuwasukumia waandamanaji makosa. Kuna wakati Serikali ilidai haijui bomu lile lilitoka wapi, mara ikasema lilirushwa na Chadema na mwisho wa siku ikakiri kuwa lilimponyoka askari mmoja.

Tukio la Daudi Mwangosi liliacha simanzi kwa wananchi wengi. Kila mtu alijiuliza matumizi ya nguvu ya namna hii yalikuwa ya nini? Yalikuwa na faida gani? Kwa nini nguvu itumike kuwashughulikia watu ambao kwa mujibu wa sheria walilijulisha Jeshi la Polisi juu ya shughuli zao? Je, shughuli za Chadema zilizuiliwa ghafla na RPC kwa sababu gani na kwa nini OCD aliziruhusu kabla ya hapo?


Jambo la kusikitisha ni kuwa, Kamanda wa Polisi wa mkoa ambaye alichukua madaraka nje ya mamlaka yake na kuingilia mkutano wa Chadema na kusababisha mauaji hayo, hakufukuzwa kazi wala kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu hata baada ya ripoti mbalimbali kuonyesha kuwa alikuwa chanzo cha mauaji yale na hadi sasa serikali inamlinda kwa udi na uvumba. Wananchi wanayajua haya na yanawaumiza sana.

Kuuawa kwa wananchi Nyamongo –Tarime

Mgodi wa dhahabu wa Nyamongo umekuwa ni uthibitisho mwingine wa matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya raia. Tatizo la Nyamongo linajulikana tangu zamani, awali huu ulikuwa ni mgodi wa wachimbaji wadogowadogo, baadaye Serikali iliamua kuuchukua ili kuwakabidhi wachimbaji wakubwa. Uchukuaji huo ulifanyika kiholela na ni kama wananchi waliporwa mgodi wao, baadhi yao walifidiwa kidogo na wengine hawajafidiwa hadi leo na huku maeneo yao yalichukuliwa.

Baada ya utaifishaji huo, Serikali haikuweka kinga yoyote ya kiuchumi kwa wananchi. Serikali ilifikiria kuwapa wawekezaji wa kigeni maeneo yote ya mgodi bila kufikiri kuwa wachimbaji wadogo ni lazima watengewe maeneo yao ili na wao waendelee na uchimbaji. Serikali haikufanya hivyo na haitaki, mwisho wa siku wananchi wanachoshwa na wanaamua kufanya maandamano kwenda mgodini na Serikali hutafsiri kitendo hicho kama "uvamizi wa mgodi" na wananchi hao huishia kupigwa risasi na polisi na kuuawa, Serikali haioni shida jambo hili likitokea tena na tena.

Mauaji ya wananchi Nyamongo ni tatizo kubwa sana na yanaendelea kila uchwao na hakuna hatua thabiti ambazo zimechukuliwa kuzuia mauaji haya na machafuko siku za usoni. Kila mara mauaji yakitokea, utasikia Serikali inasema "wananchi walivamia mgodi na kutaka kupora dhahabu hivyo polisi wamewapiga risasi na kuwaua". Je, ni Serikali gani inayofurahia wananchi wake waendelee kuuawa kwa sababu wamevamia mgodi. Kwa nini wanavamia mgodi huo? Je, Serikali bado inashindwa kufanya uamuzi wa kuwapa maeneo maalumu waendeleze uchimbaji. Ama Serikali inataka wananchi hawa wakafanye kazi gani wakati kazi waliyoizoea tangu wamezaliwa ilikuwa ni kuchimba dhahabu. Kwa nini pia migodi hii isiwaajiri wananchi hawa wenye uzoefu ili watoe mchango wao? Tunadhani suluhisho ni kuwapiga risasi tu? Na tutawapiga risasi hadi lini ikiwa hatutaki kutatua mgogoro uliopo?

Jumapili ijayo tutaendelea na sehemu ya pili ya makala hii.

(Mwandishi ana uzoefu wa masuala ya uongozi wa kisiasa nchini. Ana shahada ya uzamili ya utawala na uongozi (M.A) na ni mwanafunzi wa fani ya sheria (LLB) – Anapatikana kupitia +255787536759, juliusmtatiro@yahoo.com).


CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, MziziMkavu, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Ablessed, Kikulacho Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, Daudi Mchambuzi, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, Kill 3, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto
 
Mkuu,inapofikia hapa huwa nakosa maneno ya kuandika

Hii inawezekana ni kwasababu ya hasira yangu kubwa kwa hawa watu

Ni aibu kubwa sana,hii amani ni ipi hiyo?

Ya wananchi kuuwawa na kuogelea kwenye dimbwi la umasikini au kitu gani?
 
Mkuu inasikitisha sana kuona mamilioni ya Watanzania wakiendelea kuishi maisha ya umaskini uliokithiri katika nchi yenye utajiri mkubwa huku wezi, wahuni na mafisadi ndani ya Serikali hii dhalimu wakiendelea kukwapua matrilioni ya shilingi kila mwaka, halafu wanachi wanapodai haki zao mbali mbali huishia kupata vipigo vya hali ya juu vinavyosababisha vilema na hata mauaji ya raia wasio na hatia yoyote ile.

Mkuu,inapofikia hapa huwa nakosa maneno ya kuandika

Hii inawezekana ni kwasababu ya hasira yangu kubwa kwa hawa watu

Ni aibu kubwa sana,hii amani ni ipi hiyo?

Ya wananchi kuuwawa na kuogelea kwenye dimbwi la umasikini au kitu gani?
 
CHa kusikitisha sana ni kwamba watanzania ni waoga na wanafiki... hiyo siku inaweza isifike, kwani pale wanaoanza kuchoka, kunatokea wachache wanakuja na masufuria ya ubwabwa na kupoza machungu

Tuna evidenc za kutosha kabis kwamba watanzania hatujamaliza ubwege, sasa basi, ni muhimu kuendelea kuelimisha wananchi wa kawaida kuhusu haki zao za msingi, wajibu wao, majukumu yao na nini jukumu la serikali na wanasiasa wao... tukiweza hilo, basi tutachoka wote and the results will speak for themselves
 
Ni udhaifu wa kiongozi katika utunzi na usimamamizi wa utelezaji wa sera, kukosa confidence na maamuzi ya kibabe bila kujali sheria za nchi na democrasia.

Mauaji yanayofanywa kwa wapinzani hayana weledi, siri wala sababu zenye mashiko. Mwangosi aliuawa kwa kisingizio kwamba CHADEMA hawakuruhusiwa kuwa pale kwa sababu intelligensia ilisema kungekuwa na fujo. Na hii kauli imekuwa ikitumika kwa hila aktika kila mikutano ya wapinzani bila kujali kwamba ni watanzania na wanaakili timamu. Zaidi ya kuua wananchi, hakuna hata siku moja tumeona kwamba leo polisi imekamata watu wanaopanga kufanya hujuma kwenye mikutano ya CHADEMA, kwamba wamekamatwa kutokana na taarifa za intellijensia.

Ninasikia hasira sipendi kuendelea kuhoji kama ilikuwa ni sahihi kuua mwandishi wa habari kwa fujo zilizoanzishwa na kuhitimishwa na polisi wenyewe.

Kwa ufupi, kinachojiri ni wananchi kuondoa imani yao kwa serikali na jeshi la polisi, kuwanyima ushirikiano na kuanza kujihami na kulilpa visasi.

Hakuna atakayepona. Ccm wanapoharibu amani , waasidhani wao watakuwa salama. Tena wana maadui wengi kuliko mtu yeyote na hao polisi ni wachache sana. Dawa yao ni kudhibitiwa kul wanakoishi ili waone radha ya mauaji ya watu wasio na hatia.
Mkuu inasikitisha sana kuona muamilioni ya Watanzania wakiendelea kuishi maisha ya umaskini uliokithiri katika nchi yenye utajiri mkubwa huku wezi, wahuni na mafisadi ndani ya Serikali hii dhalimu wakiendelea kukwapua matrilioni ya shilingi kila mwaka, halafu wanachi wanapodai haki zao mbali mbali huishia kupata vipigo vya hali ya juu vinavyosababisha vilema na hata mauaji ya raia wasio na hatia yoyote ile.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakuna marefu yasio na mwisho kwani hata Shah reza wa Irani pamoja na kuwa na support ya usa na jeshi lilosheheni zana za hali juu alitimuliwa na wananchi bila ya kuwa na silaha kama za majeshi yake.
 
Siku wananchi wakisha choka kupigwa na askari patakuwa hapatoshi kabisa. Na wala isije kutokea hivyo itakuwa Palestina ndogo Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wacha ndugu yangu hasira za Watanzania za miaka nenda miaka rudi siku hiyo hawa maharamia wanaojiita polisi watatafuta pa kutokea. Wataua wangapi!? Waache uharamia wao mara moja kunyanyasa kutia vilema na kuua ili hao Mainterahamwe waendelee kung'ang'ania madarakani.

Siku wananchi wakisha choka kupigwa na askari patakuwa hapatoshi kabisa. Na wala isije kutokea hivyo itakuwa Palestina ndogo Tanzania.
 
Mkuu inasikitisha sana kuona mamilioni ya Watanzania wakiendelea kuishi maisha ya umaskini uliokithiri katika nchi yenye utajiri mkubwa huku wezi, wahuni na mafisadi ndani ya Serikali hii dhalimu wakiendelea kukwapua matrilioni ya shilingi kila mwaka, halafu wanachi wanapodai haki zao mbali mbali huishia kupata vipigo vya hali ya juu vinavyosababisha vilema na hata mauaji ya raia wasio na hatia yoyote ile.

Wakuu, tayari wananchi wameishaanza kuchoka unyanyasaji wa poliCCM. Tazama jnsi wananchi wenye hasira walivyolipasua hili jizi, pamoja na kwamba lilikuwa limevaa ngao. Haya mapoliCCM yatapasuliwa mpka kieleweke...hakuna kurudi nyuma kwa kuwa uchokozi wameuanza wao wenyewe....
View attachment 223473
Polisi wanakodiwa na kuahidiwa kulipwa mamilioni ya pesa za mlipakodi/mwananchi/mlalahoi kwa ajili ya kuua raia wasiokuwa na hatia.
http://www.mwananchi.co.tz/hab...

Kuna mama wajawazito na watoto wadogo wanafariki hospitalini kwa kukosa huduma muhimu kwa kisingizio cha kukosa fedha lakini serikali inatumia pesa nyingi kiasi hiki kwa
ajili ya kuwaua wafuasi wa vyama vya siasa na waandishi wa habari.

Mashambulizi yapolisi dhidi ya CHADEMA na wafuasi wake ni mpango wa kishenzi unaosukwa na Chama Cha Magamba (CCM) na serikali yake ya kikauzu. Na jambo la kusikitisha ni kwamba, badala ya kutumia bajeti ya chama chao kutekeleza hii kazi ya kichama, hawa umbwa wa mafisadi wanalipwa mamilioni ya pesa za walipakodi kwa ajili ya kufanya kazi wanayotumwa na mafisadi.
http://www.mwananchi.co.tz/uch...

Watoto wa shule za kata wanaketi chini kwa kukosa madawati, hawafundishwi kwa kukosa waalimu, na hawasomi kwa kukosa vitabu (wanaingia sekondari wakiwa hawajui kusoma wala
kuandika)! Lakini bado serikali hii ya mafisadi inatumia mamilioni ya fedha za
umma kiasi hiki kwa manufaa ya kuwafurahisha mafisadi! Ni lini hasa wananchi
mtaamka na kukataa upumbavu kama huu? Nchi ina matatizo lukuki badala ya
kuyashughulikia maCCM yanahangaika na CHADEMA kana kwamba HADEMA ndilo tatizo kuu linaloisumbua nchi.

Jamani tuache uchama katika hili na tujadili bila jazba. Inakuwaje serikali inachezea pesa za
umma na kuhatarisha amani ya nchi kama hivi huku tumekaa kimya?
Haya ni mauaji ya kulipwa. Serikali inayokodi watu kwa ajili ya kuua raia wasokuwa na hatia ni serikali ya kigaidi. Na wala tutakuwa hatujajosea kuiita hii serikali kwamba ni serikali ya kigaidi. Inasikitisha kuona kwamba polisi wanakodiwa kwenda kuua badala ya kwenda kuimarisha amani!

Mikono ya serikali hii ya mafisadi imejaa damu na hiyo damu haitapotea bure. Polisi
wakiitwa kwenda kulinda mikutano ya vyama vya upinzani, wanadai hawana nafasi,
lakini wakiitwa kwenda kuua na kulipwa posho, wako tayari kufanya hivyo! Hapa
pana tofauti gani na serikali ya kikoloni iliyokuwa imejikita kwenye kuua tu?
Yaani polisi wanatumwa wakaue ili walipwe posho na wao wanashangilia kupokea
posho za damu? Huu ni ushetani wa kutisha unaofanywa na serikali dhalimu ya CCM!

Tazama jinsi poliCCM wanavyowadhalilisha wananchi bila sababu za msingi.Hakika siku wananchi wakichoka unyanyasaji huu, poliCCM na mabwana wanaowatuma kufanya huu uhalifu, watajuta kuzaliwa Taznzania.
policcm na kahaba.jpg
 
Just reminds me of Mubarak and Co. how ever you are you have to leave a legacy!!!!
 
Nakikumbuka Sana kitabu cha "KULI" Lakini yana mwisho.

Kama si Leo kesho.
 
Hii hapa ni ya yule mtoto mdogo aliyepigwa risasi na polisi huko Tarime

mauaji%2Bya%2Bmtoto%2BDeus%2BJacob%2B9%2BTarime.jpg
 
Tanzania ni nchi ya watu wachache sana ambao binafsi hupenda kuwaita wenyenchi, wengine sote tuliobaki ni wananchi...
 
Mkuu inasikitisha sana kuona mamilioni ya Watanzania wakiendelea kuishi maisha ya umaskini uliokithiri katika nchi yenye utajiri mkubwa huku wezi, wahuni na mafisadi ndani ya Serikali hii dhalimu wakiendelea kukwapua matrilioni ya shilingi kila mwaka, halafu wanachi wanapodai haki zao mbali mbali huishia kupata vipigo vya hali ya juu vinavyosababisha vilema na hata mauaji ya raia wasio na hatia yoyote ile.

Inasikitisha Sana mkuu,sometimes kuexplain inakuwa ngumu hata
 
Ipo siku hii serikali ya CCM itatoka madarakani na mafisadi wote watawekwa ndani na hapo ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno.
 
Dawa ni kutii sheria bila shurti

Naona unajivua ufahamu na kujifanya kama huelewi kilichoandikwa.
Hivi hujui sheria hiyo hiyo hutambua haki za binadamu na inampa mtu uhuru wa kujieleza na kuandamana ili mradi afanye maandamano ya amani.Serikali ya CCM ndo inakuwa ya kwanza kuvunja sheria kwa kuwanyima raia wake haki zao za msingi.
Uwe na aibu wewe CCM inakufanya uwe kichaa bila kujijua yaani unatetea mpaka udhalimu kwa sababu upo CCM.
Nyambafu kabisa wewe.
 
Tz haina kiwango cha kutajwa kuna unadhalim ila wanaosema ni ukawa kwa kutotii sheria na kujifanya wajuji mbele ya wananchi il I waonewe Huruma nakulalamika ndio ajenda ya upinzani duniani so huna jipya
 
Tz haina kiwango cha kutajwa kuna unadhalim ila wanaosema ni ukawa kwa kutotii sheria na kujifanya wajuji mbele ya wananchi il I waonewe Huruma nakulalamika ndio ajenda ya upinzani duniani so huna jipya

Siku mama yako akipigwa risasi zinazopigwa hovyo ya tako utabadili mtazamo wako juu ya jambo hili.
 
Back
Top Bottom