Siku wananchi wakichoka kipigo cha askari, nini kitatokea?

Siku wananchi wakichoka kipigo cha askari, nini kitatokea?

Siku mama yako akipigwa risasi zinazopigwa hovyo ya tako utabadili mtazamo wako juu ya jambo hili.

Askari hana urafiki na mvunja sheria popote duniani kulingana na nchi husika so tii sheria utakuwa huru man
 
police brutality..upolisi imekuwa ni kimbilio la waliofeli kidato cha nne,they will do anything they are ordered to keep the dirty job!!!!
 
Askari hana urafiki na mvunja sheria popote duniani kulingana na nchi husika so tii sheria utakuwa huru man

Kama uliangalia channel ten juzi, jee yule mtoto mwenye majeraha miguuni na tumboni yaliyo sababishwa na polisi alikuwa mvunja sheria? Watu hawakatai polisi kufanya shughuli zao halali kwani huo utakuwa ujinga. Ila kila kazi inatakiwa kufanywa kwa weledi bila kuathiri wasio husika au kutumiwa kwa sababu za kisiasa eti kwa nia ya kukomoana.
 
Kwann waandamaneee..kwann wasipigwe?? Kuandama ni njia ya mwisho ya kutafuta haki jee njia zite za kutafuta haki wamezipitia
 
Touching thread!!!!
Mtoto huyo wa Tarime kaniumiza sana!!!!
 
Cku tukichoka,watatumbua

Achana na mawazo ya kuwatisha askari ndio we ye jukumu la kulinda amani name kama wewe na wajinga mna mawazo ya kuwageuka askari mnajisumbua take care
 
Huu uonevu una mwisho wake TIME WILL TELL
 
Siku wananchi wakisha choka kupigwa na askari patakuwa hapatoshi kabisa. Na wala isije kutokea hivyo itakuwa Palestina ndogo Tanzania.

Ikifika siku hiyo hivyo vyombo vya usalama vikae mbali na hao watu. Maanake kesi yake itahamia the hague
 
Tuchoke mara ya ngp na wao wamejua timewachoka ndio maana jambo la kuongea wao wanapiga risas Mungu yupo
 
Mtatiro.jpg

Julius Mtatiro

Posted Jumapili,Februari1 2015


Na Julius Mtatiro


Kwa ufupi
Lengo la makala hii ni kuonyesha tatizo hili linaloendelea kukua na kushauri hatua za kuchukua. Ni kweli kabisa kuwa nchi yoyote inakuwa na vyombo vyake vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kulinda mipaka ya nchi na hata hali ya amani ndani ya nchi yenyewe. Askari hawa huwa katika makundi tofauti na kazi tofauti kila mara. Kwa mfano, askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) huwa na jukumu la kulinda mipaka ya nchi. Majeshi mengine kama vile Polisi, Magereza, JKT n.k huwa na kazi maalumu ya kulinda amani ndani ya nchi. Wanajeshi mara zote hufunzwa mafunzo muhimu na hukanywa dhidi ya matumizi ya nguvu huku wakijulishwa kuwa siri ya mafanikio ya askari ni kuwa karibu na wananchi wa kawaida.

Matukio ya vyombo vya ulinzi na usalama kunyanyasa raia yamekithiri nchini kwetu. Raia wamekuwa wakinyanyaswa, wakiteswa, wakitishwa, wakiumizwa na mara nyingine kupoteza maisha kutokana na kipigo kutoka kwa vyombo vya dola au hata kupata ulemavu wa kudumu katika miili au akili kwa sababu ya kujeruhiwa vibaya na askari wetu.

Lengo la makala hii ni kuonyesha tatizo hili linaloendelea kukua na kushauri hatua za kuchukua. Ni kweli kabisa kuwa nchi yoyote inakuwa na vyombo vyake vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kulinda mipaka ya nchi na hata hali ya amani ndani ya nchi yenyewe. Askari hawa huwa katika makundi tofauti na kazi tofauti kila mara. Kwa mfano, askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) huwa na jukumu la kulinda mipaka ya nchi. Majeshi mengine kama vile Polisi, Magereza, JKT n.k huwa na kazi maalumu ya kulinda amani ndani ya nchi. Wanajeshi mara zote hufunzwa mafunzo muhimu na hukanywa dhidi ya matumizi ya nguvu huku wakijulishwa kuwa siri ya mafanikio ya askari ni kuwa karibu na wananchi wa kawaida.

Kwa mfano, Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania yalipoingia Uganda kumfukuza Idd Amin Dada yalipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wa kawaida yalifurahiwa sana na hivyo yalipewa kila taarifa muhimu za kupambana na adui. Askari wa jeshi lolote lile wanapokuwa hawana maelewano na raia huangukia mikononi mwa maadui kirahisi. Kwa hiyo, majeshi yote duniani hivi sasa yanajenga mikakati na maboresho makubwa ya kuwa “rafiki wa raia” na yanafanya kila yawezalo ili kukubalika kwa raia kwa lengo la kurahisishiwa kazi ngumu ya kulinda na kufuatilia masuala ya usalama.

Vyombo vyetu vya dola vimekuwa mstari wa mbele kunyanyasa na kuonea raia, kuwapiga, kuwadhalilisha na kutweza utu wao, kuna matukio kadhaa yanathibitisha hali hii:

Vurugu za gesi Mtwara

Januari hadi Mei mwaka 2013 kulikuwa na hali ya kutoelewana mkoani Mtwara. Wananchi waliandamana wakitaka majibu kutoka kwa mamlaka husika juu ya masuala ya gesi inayochimbwa mkoani humo. Wananchi waliona kuwa, ahadi zote zilizotolewa na Serikali hazijatekelezwa na badala yake Serikali imeanzisha mpango wa kusafirisha gesi kupeleka Dar es Saalam bila kuwajulisha wananchi uamuzi huo na una faida na hasara gani kwao. Maandamano yale yalipoanza Serikali ilituma askari jeshi wakatulize raia bila kuwekeza nguvu kwenye majadiliano na hatua za kistaarabu. Tulichokishuhudia Mtwara baada ya hapo ni wananchi kuteswa.

Sekeseke la gesi liliisha huku kuna raia wakiwa na vilema vya kudumu, watu karibia 12 walifariki dunia na miundombinu mbalimbali kuharibiwa. Wananchi mara zote hupenda maswali yao yajibiwe kwa wakati hasa kama yanahusu jambo lenye masilahi, na Serikali kwa kawaida huwa haitaki kutoa majibu hayo kwa wakati kuogopa kujichanganya kwa sababu haifanyi kazi kama timu. Wananchi wanaponyimwa majibu huanza viashiria vya kuchukua hatua mkononi na hata Serikali za mikoa na serikali kuu zinapoona viashiria hivyo, mara zote hazichukui hatua ya kupeleka ujumbe mzito wa viongozi ili wakae na viongozi wa wananchi na hata wananchi wenyewe ilimradi jambo lifafanuliwe na makubaliano ya msingi yafanyike, la! Mara zote serikali ikiona viashiria tu vya wananchi kudai jambo lao tena kwa maandamano ya amani kinachofuatia ni kutuma askari ili wananchi wapigwe na kukamatwa, wateswe na wakomeshwe.

Njia hii ya Serikali nyingi za Kiafrika na hususan Tanzania ni “njia ya kipofu”, maana haisaidii kitu, inawafanya wananchi wawe sugu, wazoee kupigwa, wajenge uadui na serikali na vyombo vyake, wasiwe wazalendo na waaminifu kwa taifa lao na inawafanya wananchi waone kama viongozi ni madikteta wasio na huruma hata kidogo. Wananchi wakijenga imani hii dhidi ya serikali na vyombo vyake na kisha ikaachwa iendelee kukomaa, tunajiandalia bomu zito siku za usoni ambalo likilipuka hakuna atakayejiokoa. Nasema hivi kwa sababu ni hatari sana kuwazoesha wananchi “usugu”, kuzoea mateso na kuonewa, kuichukia serikali na vyombo vyake n.k. maana wananchi ni wengi mno kila mahali na siku wakichoka hali hii ya kuonewa na kutwezwa, sote hatutakuwa salama.

Kuuawa kwa Daudi Mwangosi - Iringa

Tabia ya vyombo vya dola kutumia nguvu bila sababu katika mambo ambayo yanahitaji busara na mazungumzo ya kawaida ilikuwa sababu kubwa ambayo baadaye ilipelekea matumizi makubwa ya nguvu na kuuawa kwa Mwangosi. Daudi Mwangosi aliuawa Septemba mwaka 2012 akiwa katika majukumu yake ya uandishi wa habari. Eneo alilouawa huko mkoani Iringa lilikuwa na shughuli za kisiasa za Chadema.

Pamoja na Mkuu wa Polisi wa Wilaya kuruhusu shughuli za Chadema ambazo zilikuwa ni pamoja na ufunguzi wa matawi, Mkuu wa Polisi wa Mkoa alizuia shughuli hizo zisiendelee (jambo ambalo ni kinyume na sheria na ni nje ya mipaka ya kazi yake.

Wakati viongozi na wanachama wa Chadema wanatembelea vijiwe na ofisi kadhaa kufungua matawi yao, Polisi kwa maagizo ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa waliamua kutumia nguvu kuwatawanya na kuwakamata wananchi waliohusika katika tukio lile. Hapa ndipo Mwangosi alipolipuliwa na bomu ambalo mpaka leo halijulikani ni la aina gani. Mwili wa mwandishi huyu kijana ulisambaratika vipandevipande, baada ya hapo Serikali ilianza kutoa taarifa za kila namna za kujitetea na kuwasukumia waandamanaji makosa. Kuna wakati Serikali ilidai haijui bomu lile lilitoka wapi, mara ikasema lilirushwa na Chadema na mwisho wa siku ikakiri kuwa lilimponyoka askari mmoja.

Tukio la Daudi Mwangosi liliacha simanzi kwa wananchi wengi. Kila mtu alijiuliza matumizi ya nguvu ya namna hii yalikuwa ya nini? Yalikuwa na faida gani? Kwa nini nguvu itumike kuwashughulikia watu ambao kwa mujibu wa sheria walilijulisha Jeshi la Polisi juu ya shughuli zao? Je, shughuli za Chadema zilizuiliwa ghafla na RPC kwa sababu gani na kwa nini OCD aliziruhusu kabla ya hapo?


Jambo la kusikitisha ni kuwa, Kamanda wa Polisi wa mkoa ambaye alichukua madaraka nje ya mamlaka yake na kuingilia mkutano wa Chadema na kusababisha mauaji hayo, hakufukuzwa kazi wala kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu hata baada ya ripoti mbalimbali kuonyesha kuwa alikuwa chanzo cha mauaji yale na hadi sasa serikali inamlinda kwa udi na uvumba. Wananchi wanayajua haya na yanawaumiza sana.

Kuuawa kwa wananchi Nyamongo –Tarime

Mgodi wa dhahabu wa Nyamongo umekuwa ni uthibitisho mwingine wa matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya raia. Tatizo la Nyamongo linajulikana tangu zamani, awali huu ulikuwa ni mgodi wa wachimbaji wadogowadogo, baadaye Serikali iliamua kuuchukua ili kuwakabidhi wachimbaji wakubwa. Uchukuaji huo ulifanyika kiholela na ni kama wananchi waliporwa mgodi wao, baadhi yao walifidiwa kidogo na wengine hawajafidiwa hadi leo na huku maeneo yao yalichukuliwa.

Baada ya utaifishaji huo, Serikali haikuweka kinga yoyote ya kiuchumi kwa wananchi. Serikali ilifikiria kuwapa wawekezaji wa kigeni maeneo yote ya mgodi bila kufikiri kuwa wachimbaji wadogo ni lazima watengewe maeneo yao ili na wao waendelee na uchimbaji. Serikali haikufanya hivyo na haitaki, mwisho wa siku wananchi wanachoshwa na wanaamua kufanya maandamano kwenda mgodini na Serikali hutafsiri kitendo hicho kama “uvamizi wa mgodi” na wananchi hao huishia kupigwa risasi na polisi na kuuawa, Serikali haioni shida jambo hili likitokea tena na tena.

Mauaji ya wananchi Nyamongo ni tatizo kubwa sana na yanaendelea kila uchwao na hakuna hatua thabiti ambazo zimechukuliwa kuzuia mauaji haya na machafuko siku za usoni. Kila mara mauaji yakitokea, utasikia Serikali inasema “wananchi walivamia mgodi na kutaka kupora dhahabu hivyo polisi wamewapiga risasi na kuwaua”. Je, ni Serikali gani inayofurahia wananchi wake waendelee kuuawa kwa sababu wamevamia mgodi. Kwa nini wanavamia mgodi huo? Je, Serikali bado inashindwa kufanya uamuzi wa kuwapa maeneo maalumu waendeleze uchimbaji. Ama Serikali inataka wananchi hawa wakafanye kazi gani wakati kazi waliyoizoea tangu wamezaliwa ilikuwa ni kuchimba dhahabu. Kwa nini pia migodi hii isiwaajiri wananchi hawa wenye uzoefu ili watoe mchango wao? Tunadhani suluhisho ni kuwapiga risasi tu? Na tutawapiga risasi hadi lini ikiwa hatutaki kutatua mgogoro uliopo?

Jumapili ijayo tutaendelea na sehemu ya pili ya makala hii.

(Mwandishi ana uzoefu wa masuala ya uongozi wa kisiasa nchini. Ana shahada ya uzamili ya utawala na uongozi (M.A) na ni mwanafunzi wa fani ya sheria (LLB) – Anapatikana kupitia +255787536759, juliusmtatiro@yahoo.com).


CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, MziziMkavu, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Ablessed, Kikulacho Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, Daudi Mchambuzi, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, Kill 3, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto

Mtatiro anazungumzia wananchi gani wakichoshwa na kipigo cha askari?

Hivi Askari wanakaa wakipiga wananchi? Vyama vya siasa wasijidanganye na kujificha katika mwamvuli wa Demokrasia kufanya wanachotaka. Hiyo si maana ya demokrasia.

Wasijidanganye kw kuwa wana siasa wanaweza kufanya chochote.
 
Mimin kila nikisikia polisi kafa huwa naweka sherehe nyumbani na kujipongeza hata kama ni ndugu yangu.........
 
Tatizo sidhani kama lipo Polisi au kwa vyombo vya DOLA kwa maana ya Polisi,Jeshi,JKT au Mahakama,ila tatizo kubwa liko kwa VIONGOZI wetu au watawala wetu ambao hawaamini kama tuko kwenye SIASA ya vyama vingi,hawaelewi maana ya vyama vingi,hawajuia sheria mama iliyotunga Vyama vingi,hawajui mipaka yao kama chama tawala.

Wanachama wa CCM hawaelewi haki za msingi za wapinzani,hawajui kuwa haki ya kuandamana kisheria ipo,na anayeandamana mradi havunji sheria ya nchi basi anatekeleza HAKI yake ya msingi kabisa.

Hivyo CCM kubalini tu sasa mambo yamebadilika......
 
Mkuu inasikitisha sana kuona mamilioni ya Watanzania wakiendelea kuishi maisha ya umaskini uliokithiri katika nchi yenye utajiri mkubwa huku wezi, wahuni na mafisadi ndani ya Serikali hii dhalimu wakiendelea kukwapua matrilioni ya shilingi kila mwaka, halafu wanachi wanapodai haki zao mbali mbali huishia kupata vipigo vya hali ya juu vinavyosababisha vilema na hata mauaji ya raia wasio na hatia yoyote ile.

Halafu kuna wabunge walikua wanacheka wakati hoja hii ikizungumzwa ....

Napata wasi wasi kama hawa wabunge wana utimamu kisawasawa,iweje uchekelee mtu kupigwa na hana hatia?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sio hilo mkuu, huku uraiani, wananchi awaombi kuingia anga za polisi maana ni kero, imefikia hatua mtu anaibiwa vitu au kufanyiwa uhalifu, unamshauri kwenda kuripoti polisi anakataa, kisa ni wasumbufu na utaishiwa kutolewa hela bila suluhu kupatikana, raia wanaona bora waache tu mali zao ziende na wezi, Jeshi la polisi kwa hali hii limepoteza imani kwa wananchi kwa kiasi kikubwa mnoo
 
Panya road wataingia msituni na kututetea.lol!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mwisho wao unakuja, ipo siku na wao watakamatwa na kupigwa hivyo
 
Dah! Inna Liillah wainna illaihi Rajyun... "Wapigwe tu! Tumechoka by PINDA" ... Mimi nasema; Malipo ni hapa hapa Duniani ... Hakika watadhalilika kabla ya kuonja la ya umauti kwa dhulma zote wanazozifanya kwa Watanzania ...
Hii hapa ni ya yule mtoto mdogo aliyepigwa risasi na polisi huko Tarime

mauaji%2Bya%2Bmtoto%2BDeus%2BJacob%2B9%2BTarime.jpg
 
Back
Top Bottom