pefla
Senior Member
- Jan 31, 2012
- 105
- 74
Mwalimu ni mtu anayesaidia wengine/jamii kupata ujuzi, maarifa na tunu katika Nyanja mbalimbali zinazohusu jamii au ulimwengu/dunia. Na majukumu ya mwalimu yanaweza kutofautiana kadiri ya utamaduni husika katika nchi.
Kwa taifa la Tanzania mwalimu amechukuliwa kama shimo la katakata katika fikra fikirishi katika ujenzi wa maendeleo na ustawi wa jamii kwa taifa zima. Ndio maana hata matokeo ya mitihani mbalimbali hasa hasa ya kidato cha nne na sita ya kitangazwa mwanafunzi wa jamii husika anaulizwa umefeli hata alama ya kwenda kusoma ualimu huna? Lakini sio walimu wote wamekuwa walimu kwa sababu ya matokeo mabaya wa mitihani yao bali ni wito na kazi kama kazi nyingine.
Hii yote imetokana na taswira iliyojengwa na taifa letu kwa jamii kuhusu kazi/kada ya ualimu na imepelekea hata viongozi wa ngazi zote serikalini kujenga tamaduni ya kutowajali au kuthamini kada ya ualimu, ndio maana matamko ya kejeli na dharau yote ni ya walimu LAKINI na WAO NI CHIMBUKO LA MWALIMU DHARAULIWA.
Kuna kila sababu ya kuwa na walimu bora ili nao watoe elimu bora katika taifa letu.
Mwaka 1960 miaka mitatu baada ya kupatikana kwa Uhuru wa Ghana, aliyekuwa Rais wakati huo alipeleka bungeni mswada wa sheria ya kuwaongezea mshahara walimu, alisema “Naomba mniunge mkono ndugu wabunge katika hoja ya kupanga mshahara wa walimu wetu’’ anaendelea kusema “Mimi binafsi ni nimelazimika kuja bungeni kuhutubia kwa lengo moja la kuifanya Ghana iwatambue walimu na kuwapa mshahara unaoonyesha umuhimu wao kwa taifa hili. Mimi naamini kwa sababu sioni kama kuna namna unayoweza kutofautisha walimu wa Ghana na hatima au mustakabali wa Ghana’’ hii ni tofauti kidogo na taifa letu kila kukicha miswada iyopelekwa bungeni ni kwa ajili ya kupunja maslahi ya walimu na kuanzisha mifuko kandamizi kama CWT na umuhimu wa mwalimu unaonekana katika kazi zisizokuwa na maslahi kwao kwani tumejengwa katika uzalendo mfilisi kwa maslahi hayo tu.
Kwa mfano usimamizi wa uchaguzi katika ngazi zote (mitaa na uchaguzi mkuu) chaguo lao ni mwalimu na hii inapelekea walimu kuonekana siku zote za utumishi wetu kuwa shimo la TAKATAKA (garbage) katika jamii na kwa viongozi wetu kwani dharau inaoneshwa kupitia ahadi za uongo na ongezeko la shilingi elfu tisa(9,000/=) kwa mwaka. JITAMBUE
Lakini mwalimu anatumia zaidi ya nusu ya muda wake kujiandaa na kuandaa namna ya kumfinyanga mwanafunzi wake ili baadaye tuwe na kizazi bora na viongozi bora zaidi. Ili hili litokee, lazima mwalimu awekwe katika mazingira yanayofaa na yeye afae kwa majukumu anayokabidhiwa sio ahadi za uongo na kejeli juu yetu KUTOKA KWA UZAO WA MIKONO YETU NA JUHUDI ZETU.
Kutokana na kejeli hizo na ahadi za uongo leo kazi ya ualimu haivutii tena; kama leo watoto wa walimu hawatamani kazi ya wazazi wao, kama leo hii asilimia 70 ya walimu wanatamani kuacha kazi, tuna nini cha kujivunia katika taifa letu kama sehemu ya kuleta maendeleo katika taifa letu? Kazi ya kutengeneza taifa bora siyo kazi ndogo.
Na taifa bora litatengenezwa endapo wanaotengeneza watapunguziwa kejeli, dharau na ahadi za uongo na kama tutaendelea kuona elimu ni elimu kwa kushindwa kuthamini na kuwekeza kwa walimu siku chache zijazo tutanunua kila kitu na kutengeneza taifa la kejeli juu ya kada ya ualimu. Kumbuka Rais, Waziri Mkuu na wengine wengi ni kazi ya mikono yetu.
TAMBUA THAMANI YA MIKONO YAKO NA JUHUDI ZAKO