Siku Nitakayorudisha Namba......

Siku Nitakayorudisha Namba......

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Habari zenu za mchana wapendwa,

Natumai nyote hamjambo, kwa wale tunaowasiliana PM na nje ya JF nimekuwa hafifu kwenye mawasiliano kwa wiki mbili hizi kutokana na mambo kadha wa kadha hayo ni pamoja na majukumu yanayonikabili. Kama ulidhani nimechuna makusudi basi uelewe si hivyo.... ni ngija ngija za ndima.

Katikati ya majukumu nikapatwa na tafakuri, humu JF tumezoea kuona ID imepotea haichapishi tena wengine wakiwa wamejitoa mazima wengine wamefungua ID mpya wengine albadani wametutoka kwenye dunia hii.

Pia tumeshuhudia mara kadhaa watu wakileta mrejesho humu kuwa flani kafiwa na mtu wake wa karibu au mwana jamii mwenzetu amepata ajali au amelazwa anaumwa na saa nyingine kuwa mwanajamii mwenzetu ametutoka.

Tafakuri iliniuliza, hivi Kasie siku ukiaga dunia, kuna atakayejua humu JF? Kuna atayekuja kutoa taarifa au mrejesho kuwa kigagula Katie kavuta kamba....???!!

Je, wewe ulishajiuliza siku ukirudisha namba, kuna wanajamii humu wataojua na kuja kutoa taarifa? Taarifa tuu na si michango tafadhali. Je, wafikiri nani atayekuja kuleta taarifa zako humu?

Binafsi sina mahsusi wa kuleta mrejesho wangu humu, labda kama mpiga picha maarufu wa zamani aka Tyta bado yupo ndo ataweza leta mrejesho wangu siku nikirudisha namba kwa muumba. Maana huyu ndo alijitolea kunishushushu bila kunitaarifu maji yalipomzidi kimo akakimbia kusikojulikana na hatukuwa tumemalizana ugomvi wetu just like Watu8..... hehehehheee don't get suprised, kesi ya muuza matunda haijaisha.....

Asante Bw. Mtwango kwa kunitumia huu wimbo nikiwa napata mlo wa mchana.

Ni tafakuri tuu, as simple as that. Nothing complicated.

Kasie Mahaba Matata.
 
Kasie hivi Tyta alifia wapi?Maana kimya isjekuwa kadanja....!!!

Nina uhakika bado hajarudisha namba... Ila wapi yupo hiyo ni siri hadi siku atayoibuka tena.
 
Hili nalo neno...... kuna wengi siwaoni tena humu!!! ukute tayari walishagenda!!!
 
Siku nikirudisha namba, those around me will know, they will lay me to rest and that's enough.
 
Yawezekana, pia kuwa wamebadili vitambulisho ndo kila leo natafuta mchumba mara hivi mara vile.... basi tafrani tuu tunapigana vikumbo kwenye majukwaa ya JF huyu akiingia huku huyu anatoka huyu yuko chumbani na yule.....

Melo mwenyewe katulia kwa pembeni anatucheki tuu.
 
"Kasie Mahaba Matata", Hapa ndio pananiachaga njia panda

Unabakishwa na nini sasa hapo panda?

Ni rahisi tuu.... Yaani Mahaba halafu Matata.... yanakuwaga matamuuu hayooo.
Hehehehehehehheee ciao.
 
Habari zenu za mchana wapendwa,

Natumai nyote hamjambo, kwa wale tunaowasiliana PM na nje ya JF nimekuwa hafifu kwenye mawasiliano kwa wiki mbili hizi kutokana na mambo kadha wa kadha hayo ni pamoja na majukumu yanayonikabili. Kama ulidhani nimechuna makusudi basi uelewe si hivyo.... ni ngija ngija za ndima.

Katikati ya majukumu nikapatwa na tafakuri, humu JF tumezoea kuona ID imepotea haichapishi tena wengine wakiwa wamejitoa mazima wengine wamefungua ID mpya wengine albadani wametutoka kwenye dunia hii.

Pia tumeshuhudia mara kadhaa watu wakileta mrejesho humu kuwa flani kafiwa na mtu wake wa karibu au mwana jamii mwenzetu amepata ajali au amelazwa anaumwa na saa nyingine kuwa mwanajamii mwenzetu ametutoka.

Tafakuri iliniuliza, hivi Kasie siku ukiaga dunia, kuna atakayejua humu JF? Kuna atayekuja kutoa taarifa au mrejesho kuwa kigagula Katie kavuta kamba....???!!

Je, wewe ulishajiuliza siku ukirudisha namba, kuna wanajamii humu wataojua na kuja kutoa taarifa? Taarifa tuu na si michango tafadhali. Je, wafikiri nani atayekuja kuleta taarifa zako humu?

Binafsi sina mahsusi wa kuleta mrejesho wangu humu, labda kama mpiga picha maarufu wa zamani aka Tyta bado yupo ndo ataweza leta mrejesho wangu siku nikirudisha namba kwa muumba. Maana huyu ndo alijitolea kunishushushu bila kunitaarifu maji yalipomzidi kimo akakimbia kusikojulikana na hatukuwa tumemalizana ugomvi wetu just like Watu8..... hehehehheee don't get suprised, kesi ya muuza matunda haijaisha.....

Asante Bw. Mtwango kwa kunitumia huu wimbo nikiwa napata mlo wa mchana.

Ni tafakuri tuu, as simple as that. Nothing complicated.

Kasie Mahaba Matata.

Bana Congo tosimbana maboko....

Siku nikirudisha namba, those around me will know, they will lay me to rest and that's enough.

That's fact, there's no doubt about that. Leaving your marks here every now and then.... when one goes it matters to some extent to the rest that one is no longer...

Without any harm those who surround us covers everything though JF also surrounds us.

After all its not a big deal, cool beans.

Cheers.
 
Back
Top Bottom