Siku nimefanya ya Kajole

JEKI

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
4,709
2,000
Wengi hamlijui jina hili maarufu la Kajole, kifupi huyu alikuwa mwanariadha na baadae mcheza mpira katika kijiji chetu, alichaguliwa katika timu ya mpira kwa sifa ya mbio, kocha akiamini kazi itakuwa kumtangulizia mpira na yeye kukimbia, jamaa huyu alikuwa na miguu kama mikono, tofauti na matarajio ya kocha akiwa kiwanjani kwa kuwa hakujua kudrible mpira basi mara nyingi alikuwa akikimbia hadi kuutangulia mpira na hivyo kuwa kazi bure tu. Mfano wa kajole umefanana kabisa na kitendo nilichowahi kukifanya mbele ya bibi yangu, enzi hizo tukiwa watoto tunazuiwa kula nje ya nyumbani, siku hiyo tunatoka shambani na bibi, tukapita kwa rafiki yake, tukapewa viazi na maziwa, chakula nilichokipenda/ninachokipenda sana, kwa mshangao bibi akala na mimi nikagoma na nikatoa sababu ile ile, siwezi kula kwa watu, bibi alihangaika sana bila mafanikio, sikula. Hadi leo nimebaki kuwa mtu wa msimamo mkali.
 

naumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
4,710
2,000
Kajole anaefahamika Tanzania hana sifa hizo au ni a.k.a tu ya huyo star wa kijiji?
 

Sometimes

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
4,544
1,500
Kama Kajole au "Mohamed Kajole" ndiye anayezungumzwa, basi unaweza pata habari zake ukim-google. Alikuwa mchezaji wa timu ya Taifa na kocha wa Simba pia!
 

124 Ali

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
7,673
2,000
anayefahamika ana sifa gani? isije kuwa ndo huyu alijiendeleza tu.
Mohamed Kajole(RIP) ni mtoto wa kitaa bhana!alikuwa akiishi maeneo ya mburahati beki tatu matata timu ya simba,alichezea taifa pia ,huyu bwana hakuwahi kuwa mbwigira huyu mjanaja kabla hata hajakuwa maarufu,itakuwa huyo mbwigira wenu alijiita kajole na itabidi utuambie jina lake halisi ni tuntufye bin nani?
 

Changalucha

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
273
250
Umenikumbusha "Mazungumzo baada ya habari".


Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums
 
Oct 26, 2013
31
0
Mohamed kajole "Machela" alikuwa beki tatu wa Simba na stars. Alikuwa na mguu wa tende. Ukitaka kumjua muulize mtoto wa bob Ogola wa Gor Mahia alizolewa kwenye chaki na kupigwa ngumi. Alipokimbilia kwa Bob kulalamika a kaambiwa :wewe Hapana jua Kama ile ndio kajole ya Tanzania angalia itakuuwa! R.I. P. Kajole
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom