Mrs Gudman
JF-Expert Member
- Jul 3, 2015
- 613
- 1,300
Mwaka gani huo mzee?Ee bhana eeh hapa duniani huwaga kuna nyakati ngumu sana ambapo unaweza tamani kiama kitokee utoweke kuliko fedhedha au hali flani ya aibu na maumivu yanayokukuta .
Leo nimekumbuka tukio moja ambalo siwezi lisahau maisha yangu yote ,nilikuwa advance enzi hizo miaka kadhaa ilopita ticha wa kemia akasema kutakuwa na test(Physical chemistry) test enyewe ni swali moja tu la calculation na mfano wa hilo swali tushafanya na nimeelewa vizuri tu ,basi buana siku kaa mbili hivi kila mtu anajiandaa .
siku ya mtihani ikafika swali likaja lile lile hadi data hazijabadilika lina marks 25 na lipo moja tu,tukagawiwa karatasi tukapewa dakika tano tusome swali ,nilipoliona swali nikafurahi pia mana naona kabisa 25 yote nachukuwa ha ha
Nikachukua karatasi nikaandika jina ile nashika tu peni nianze kuandika data ,akili ikafuta kila kitu hata kucollect data siwezi yani sielewi ,nikawa najaribu nikumbuke basi hata fomula itanisaidia kucollect data nikashindwa pia kukumbuka fomula ,kumbuka hilo swali nalijua na nimelisoma vilivyo.
Dah nikawa naangalia pembeni je wenzangu wanafanya? kiukweli darasa nzima kila mtu alikuwa bize kukokotoa isipokuwa mimi tu.
Teacher anapita anaangalia jinsi watu wanafanya naona anapita kwangu mimi nimeandika tu jina huku zishatangazwa zimebaki dk 15 tu time iishe.
Nikainama juu ya dawati nikawa nasali Mungu anikumbushe kanuni ,kiukweli sikukumbuka ,nikakemea pepo la usahaulifu wapi mwisho wa siku nikabadili maombi ,nikawa natamani litokee janga lolote tetemeko au kiama woote tutoweke tu kuliko vile majibu yanavyoenda kuwa mimi nina 0/25 wenzangu wooote wana 25/25
Maombi hayo pia Mungu akuyajibu ,nikasikia pens down ,tukakusanya mimi nimeandika jina tu.
Kila mtu anafuraha vicheko na kumshukuru teacher kwa ile feva ,ilibidi niende tu bwenini kulala
Majibu yalitoka robo tatu ya darasa ilipata 25/25 mimi nikapata 2/25 hizo 2 niliwekewa tu kama zawadi ya kuandika jina na kuaribu karatasi ha ha.
Kitu gani kimewahi kukupata kama mimi???
#TIRIRIKA
#TUNATOKAMBALI
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]Kuna day nimekula mtungi sana kuanzia mida ya asubuhi hivi saa nne. Nililewa sana asee kiasi kwamba mpaka saa tisa hivi alasiri nilifanya kubebwa nipelekwe home.
Nikaingia chumbani nikavua nguo zote nikalala, mida ya saa 12 jioni mkojo umebana nikasema ngoja nitoke nje nikakojoe.. Ile natoka na wenge langu uchi wa mnyama kumbe watu wamekaa nje bi mkubwa na mashangazi walikimbia ghafla sikuona mtu nilirudi ndani kwa aibu hata mkojo sikuusikia tena.
Niliona aibu sana nikawa nafanya kuamka asubuhi kabla ya wote nasepa kama week hivi. Nikaona bora nihame home tu nisije kuzua mengine. Nikakaa mda sana bila kula mtungi. Saivi nakunywa kistaarabu
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sanaMm juzi tu hp tulikuwa na dua nyumbani cc ni waislam ss sura zilikuwa nyingiiiii kila mmoja akapewa zke ww utasoma sura flani ziwe 40 yule atasoma sura flani ziwe 60 na kadhalika mm nilipewa sura nyepesiiiii na nnaijua hainisumbui hata kdg coz nilipita madrasa bc umefika muda wa kuanza kusoma bakhti nzr tunasoma kwa pamoja ila kila mmoja anasoma chake bc mm nikatembelea nyota zle sauti za wenzangu wanaosoma sikusoma hata sura moja yaani kila nikijaribu naishia "bismillahi" memory haiji kabsaaaaaa cjui ni nn huwa kinatokea!
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]Hivi vitu ni kawaida mkuu, hutokea pia kwenye oral interview, unajikuta mzee unaweza Hata kusahau jina lako.. Wale panel members huwa wana enjoy saana
Haaahaaaa....bora ulihama!Kuna day nimekula mtungi sana kuanzia mida ya asubuhi hivi saa nne. Nililewa sana asee kiasi kwamba mpaka saa tisa hivi alasiri nilifanya kubebwa nipelekwe home.
Nikaingia chumbani nikavua nguo zote nikalala, mida ya saa 12 jioni mkojo umebana nikasema ngoja nitoke nje nikakojoe.. Ile natoka na wenge langu uchi wa mnyama kumbe watu wamekaa nje bi mkubwa na mashangazi walikimbia ghafla sikuona mtu nilirudi ndani kwa aibu hata mkojo sikuusikia tena.
Niliona aibu sana nikawa nafanya kuamka asubuhi kabla ya wote nasepa kama week hivi. Nikaona bora nihame home tu nisije kuzua mengine. Nikakaa mda sana bila kula mtungi. Saivi nakunywa kistaarabu
Sent using Jamii Forums mobile app