Siku Nilipotia maguu Dar kwa mara ya kwanza.

Siku Nilipotia maguu Dar kwa mara ya kwanza.

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Posts
42,099
Reaction score
12,932
Nimeshuka vizuri tu pale Ubungo bus terminal na nikakutana na wenyeji wangu ambao walikuja kunipokea. Kwa kuwa walikuwa wanaishi mbagala na usafiri ulivyo wa mashaka ilituchukua masaa matatu kufika huko. Nilipofika nilijuta, maana mtaani hapo nilisikia habari kuwa POPOBAWA kamtafuna jamaa mmoja nyumba ya jirani usiku uliopita. Na katika TV kulikuwa na mtabiri maarufu afrika mashariki na kati akitoa habari za popobawa eti akikutafuna lazima utangaze ili asirudi tena. Lakini kabla ya kulala yalifanyika maombi ya nguvu kutoka kwa wale wenyeji wangu ambao walikuwa walokole kukemea huyo pepo popobawa asiingie katika nyumba hiyo. Licha ya uchovu wa safari siku hiyo sikupata usingizi, ila namna nilivyolala ndio ilikuwa balaa. Kulikuwa na bukta, suruali na juu nikapiga jeans na mkanda, licha ya joto la Dar. Licha ya hivyo sikupata usingizi mpaka asubuhi..........
 
popombawa... sema kweli Katavi hajakuvua weye?
 
Last edited by a moderator:
Sasa utashangaa! Mimi kwa uwezo wa nguvu zilizokosa mwanga nilizoachiwa na Marehemu Babu yangu , nilifanikiwa kuwapiga miti mapopobawa wa3.
Sisi ndo Bagamoyo moja!
 
Sasa utashangaa! Mimi kwa uwezo wa nguvu zilizokosa mwanga nilizoachiwa na Marehemu Babu yangu , nilifanikiwa kuwapiga miti mapopobawa wa3.
Sisi ndo Bagamoyo moja!

halafu tangu yule shehe mtabiri maarufu wa afrika mashariki na kati afariki dunia haya mauzauza ya popobawa hayasikiki kabisa...
 
halafu tangu yule shehe mtabiri maarufu wa afrika mashariki na kati afariki dunia haya mauzauza ya popobawa hayasikiki kabisa...

Una maana Mz wa Magomeni mi10 Muembechai !
Kwa hiyo unahisi ndo ilikua mifugo yake ?
 
....au ndo unatangaza ili wakuache khekhekhekheeeeeeee...


shem judgement we noma!
 
Last edited by a moderator:
Katavi na wewe unaogopa hayo makitu?
 
Last edited by a moderator:
Nimebaki na vicheko tu! Mentor anasema kusema kwako hapa ndo unalipiga marufuku lisirudi, Judgement keshayapiga miti mapopobawa matatu, kudadadddki kufa hakuna breki sosi: Asprin.

Afanaaaaaleki, kufa hakuna breki wallah...!

Disemba inakaribia asee, na Mwarabu pale Mamsera ana stock ya kutosha. Naomba mwongozo wako na wa mwenyekiti Kaizer.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom