Da Vinci XV
JF-Expert Member
- Dec 7, 2019
- 3,871
- 6,468
SIKU NIKIWA MKUBWA.
Nikiwa mkubwa nitamfundisha mwanangu swala zima la Kutukumbuka sisi wazazi wake baada ya kumkatia simu mara Nne Mama yangu Aliyekuepo kijijini baada ya kuniomba Pesa ya Sukari
Nikiwa mkubwa nitakuwa Imaam ,na kumtahadharisha muumini kuhusu Uzinzi ,Baada ya kulala na Mkewe siku mbili zilizopita.
Nikiwa mkubwa nitamkataza kijana wangu kujihusisha na makundi ,wakati huo nikielekea kijiweni kuvuta bangi.
Nikiwa mkubwa nitawaelimisha vijana kuhusu athari za Punyeto ,wakati nikitoka dukani kununua sabuni kwa ajili ya Kujichua
Nikiwa mkubwa nitawafundisha watoto wangu namna ya kujipikia wenyewe, baada ya kutoka nao hotelini kununua Chakula.
Nikiwa mkubwa nitachangia Laki mbili kwenye Mazishi ya Rafiki yangu Aliyefariki baada Ya kukosa Elfu 30, ya Matibabu.
Nikiwa mkubwa nitamkataza wizi mtoto wangu , ninayemsomesha kwa pesa niliyochota kwenye Mradi , wa Ujenzi wa Zahanati na Shule.
Nikiwa mkubwa nitamfunza mwanangu kuwa na Adabu na heshima kwa wakubwa ,baada ya kumtukana Mzee anayelinda Nyumba yangu baada ya kuchelewa kufungua Geti.
Nikiwa mkubwa nitakuwa daktari ninayetoa elimu ya madhara ya Pombe na Ngono zembe, huku nikielekea bar kunywa Kreti za Bia na kununua Makahaba.
Nikiwa mkubwa nitampiga, Mwanangu kukojoa kitandani baada ya Kumpa soda tatu usiku kabla hajalala.
Nikiwa mkubwa nitamlaumu mke wangu, kwanini hanisaidii kuhudumia mahitaji ya Nyumbani ,Baada ya kumkataza kujishugulisha na vikundi vya wanawake vya kuwezeshana.
Nikiwa mkubwa nitawaeleza ndugu zangu umuhimu, wa matembele baada ya mimi kumaliza kula kuku mzima na mishikaki.
Nikiwa mkubwa nitampa mchele kuku wangu, Ili baadae nije nimle na Wali
Nikiwa mkubwa nitamkataza binti yangu kuvaa nusu Utupu, baada ya kumaliza kumuonyesha video za Nicki minaj na Gigy money.
Kesho nikiwa mkubwa nitamfundisha mtoto wangu kutafuta kwa jasho , baada ya kumdhulumu mama muuza midoli ,nilipokuwa namnunulia mtoto wangu mdoli wa kuchezea.
Nikiwa mkubwa nitawaeleza namna ninavyomchukia EX wangu, wakati huo huo naelekea kwake baada ya Kuniambia Amenimiss.
Nikiwa mkubwa nitadai mahari ya millioni 100 ,kwa binti yangu aliefukuzwa shule baada ya kupewa mimba, na Mwanaume asiyemjua.
Nangoja kwanza niwe mkubwa.
Tumeelewana Au mnangoja muwe wakubwa????