Kihorohonjo
Member
- Jun 11, 2009
- 34
- 7
Wadau,
Nilifanya muamala wa kuhamisha pesa kwa njia ya simu, bahati mbaya pesa sikuipata. Nilianza kufuatilia kwa kupiga simu NBC baada ya siku moja. Majibu ni kuwa pesa yako itarudi ndani ya saa 24. Leo ni siku ya tisa pesa haijarudi.
Nimefuatilia kwa kupiga simu kwa huduma kwa wateja na inaonekana watumishi wote wa kituo wamenifahamu hivyo wananikwepa. Jumatano nilipiga simu na mpokeaji aliamua kukaa kimya bila kujibu hadi nilipokata simu yangu.
Leo nimepiga na mtoa huduma alitoa ushirikiano na baadae kunieleza nikate simu anafuatilia suala langu na atanipigia simu baada ya muda kidogo. Hivi sasa ni masaa matano yamepita na sijapigiwa simu.
Wadau msaada wenu tafadhali.