Siku ngapi zinahitajika kurudishiwa pesa na NBC bank baada ya muamala kutokamilika?

Kihorohonjo

Member
Jun 11, 2009
34
7
Wadau,

Nilifanya muamala wa kuhamisha pesa kwa njia ya simu, bahati mbaya pesa sikuipata. Nilianza kufuatilia kwa kupiga simu NBC baada ya siku moja. Majibu ni kuwa pesa yako itarudi ndani ya saa 24. Leo ni siku ya tisa pesa haijarudi.

Nimefuatilia kwa kupiga simu kwa huduma kwa wateja na inaonekana watumishi wote wa kituo wamenifahamu hivyo wananikwepa. Jumatano nilipiga simu na mpokeaji aliamua kukaa kimya bila kujibu hadi nilipokata simu yangu.

Leo nimepiga na mtoa huduma alitoa ushirikiano na baadae kunieleza nikate simu anafuatilia suala langu na atanipigia simu baada ya muda kidogo. Hivi sasa ni masaa matano yamepita na sijapigiwa simu.

Wadau msaada wenu tafadhali.
 
Pia ingia kwenye mtandao kuna sehemu ya complaints jaza hapo na tuma mail customer care.Nikuhakikishie fedha zako zitarudi mm imeshanitokea zaidi ya Mara tano(5) najitumia hazifiki zingine kwa watu wengine.Maximum huwa ni siku 7.Mtandao wao ni majanga.Kuna benki moja kongwe nchini,yenye matawi kila wilaya iko vizuri kwenye mobile banking.Pole
 
Wadau nilifanya muamala wa kuhamisha pesa kwa njia ya simu, bahati mbaya pesa sikuipata. Nilianza kufuatilia kwa kupiga simu NBC baada ya siku moja. Majibu ni kuwa pesa yako itarudi ndani ya saa 24. Leo ni siku ya tisa pesa haijarudi. Nimefuatilia kwa kupiga simu kwa huduma kwa wateja na inaonekana watumishi wote wa kituo wamenifahamu hivyo wananikwepa. Jumatano nilipiga simu na mpokeaji aliamua kukaa kimya bila kujibu hadi nilipokata simu yangu. Leo nimepiga na mtoa huduma alitoa udhirikiano na baadae kunieleza nikate simu anafuatilia suala langu na atanipigia simu baada ya muda kidogo. Hivi sasa ni masaa matano yamepita na sijapigiwa simu.

Wadau msaada wenu tafadhali.
Si uende bank
 
Pia ingia kwenye mtandao kuna sehemu ya complaints jaza hapo na tuma mail customer care.Nikuhakikishie fedha zako zitarudi mm imeshanitokea zaidi ya Mara tano(5) najitumia hazifiki zingine kwa watu wengine.Maximum huwa ni siku 7.Mtandao wao ni majanga.Kuna benki moja kongwe nchini,yenye matawi kila wilaya iko vizuri kwenye mobile banking.Pole
bila shaka ni NMB
 
Back
Top Bottom