Siku mchepuko uliponiambia ana ujauzito wangu

Ilikuwa kama siku ya alhamisi hivi, mwaka juzi; rafiki yangu mmoja akanipigia simu, na kunijulisha ana ujumbe wangu, nikamuuliza ujumbe gani? akasema kuna dada fulani anakutafuta sana, anasema kwenye simu yako hakupati.

Nikamuuliza ana tatizo gani? akajibu, ''anasema ana ujauzito wako, pia yeye ana mume, na wewe una mke kwa hiyo ni changamoto; pia anahofia mumewe akijua itakuwa tatizo kubwa.'' Nikamuuliza yuko wapi, na anaitwa nani?, aliponiambia jina tu, nikakumbuka kweli nilishakuwa naye kwenye mahusiano.

Basi tukapeana 'appointment' kesho yake tuonane, mida ya saa tatu usiku.

Muda ulipofika nikaenda zangu kwenye eneo la tukio, nikawa napiga mvinyo wangu taratibu. Baada ya kama dakika 20 wakawa wamefika, wadada wawili, pamoja na huyo rafiki yangu.

Tukasalimiana, na mhudumu akaja kuwahudumia.

Kutokana na mbinu nilizozipata jando, kama mwanaume kamili, sitakiwi kumuharasi mtoto wa kike, zaidi ya kumpeti peti tu.

Tukawa tunapiga stori nyingi tu, za kuchekesha ili kumuweka sawa na ajione hakukosea kukutana na mimi; baada ya lisaa limoja na nusu kupita, nikamsogelea mrembo, na mazungumzo yakawa hivi:-

Mimi: Niambie mpenzi wangu, unachangamoto gani?
Yeye : Unajua baby, nina ujauzito wako
Mimi: (Sikushtuka, nikawa nampiga mgongoni kidogo ili aweze kupata joto), Sawa, wewe ulikuwa unatakaje; kwa sababu mimi nakusikiliza wewe, utakachokitaka mimi sitapinga?
Yeye: Mimi nataka nitoe, kwa sababu mume wangu akijua itakuwa tatizo
Mimi: Sawa ata ungetaka kuzaa kwangu haina shida, mi napenda watoto, nami kuwa na watoto wengi ni furaha pia
Yeye: Hapana, itaniharibia ndoa, naomba ukubaliane na maamuzi yangu.
Mimi: Sawa, nakubaliana na maamuzi yako,utakapokwama usisite kunijulisha
Yeye: (Akachukua glass tukagonga 'cheers' akani 'kiss' tukaendelea kupiga mvinyo huku tukiwa na furaha tele, akiwa ananiimbia wimbo fulani hivi wa mahaba)

Baada ya kukaa muda mrefu, tuliagana na wao wakaondoka; baada ya kufika akanipigia simu kwa furaha sana; akanishukuru kwa kumpokea vizuri, kwa sababu alikuwa akihisi labda ningemtukana au ningekataa huo ujauzito.

Akasema ''Equation x, you are a real gentleman''​
Sasa,dah nakwama kidogo!Hebu nyoosha maneno.Nia yake ilikuwa kukujulisha tu kwamba ana ujauzito wako?Au ilikuwa ni kukufahamisha tatizo kubwa lingetokea mumewe angejua?Au kukuomba ruhusa ya kuutoa ujauzito?Au kukuona ungepokeaje taarifa ya ujauzito huo?
Hata hivyo,at last,nini kilotokea?Alitoa ujauzito au aliutunza na kupata mtoto?Ikawaje?
 
Sasa,dah nakwama kidogo!Hebu nyoosha maneno.Nia yake ilikuwa kukujulisha tu kwamba ana ujauzito wako?Au ilikuwa ni kukufahamisha tatizo kubwa lingetokea mumewe angejua?Au kukuomba ruhusa ya kuutoa ujauzito?Au kukuona ungepokeaje taarifa ya ujauzito huo?
Hata hivyo,at last,nini kilotokea?Alitoa ujauzito au aliutunza na kupata mtoto?Ikawaje?
Mara nyingi mtu akiwa na tatizo kwa mara ya kwanza, kisaikolojia huwa kinamtesa na wakati mwingine anaweza kukata tamaa; alipokuja akawa mwepesi na kuona vitu vyote vinawezekana.
 
Kuna nini hapo? :D :D
Hawa mapacha kama mimi na ndugu yangu blonde. Nawatofautisha mmoja anavaa kitenge mwingine anavaa mtumba. Yupi aliyekupiga kibuti? Joanah au Joannah?
1355820-despecibleme-1489566962.jpg
 
Back
Top Bottom