Siku mbili za Halima Mdee rumande Oysterbay

Siku mbili za Halima Mdee rumande Oysterbay

Tatizo letu? Hivi unajielewa kweli? Tatizo langu na nani?
Wapinzani, upinzani sio uvunjifu wa heshima, Rais anastahili heshima yake, Huwezi kwenda kwenye media na kuongea kipumbavu namna ile, Demokrasia sio uvunjifu wa adabu, je ndio vile anavyoongeaga na baba yake?
 
Una ushahid kwamb kwend kwa mama ake alitak kutoroka au unashabikia tu mtu famous vle atoroke aende wap
Hlo unaloliombea halitafanikiwa hata kidogo wabunge tutapat weng kuliko 2015
VIVA CHADEMA
Soma vizur.mimi nilikuwa naeleza ya aliyetangulia ku post.Angali na soma huyo niliyemnukuu.
Ukiandika "Samahani" itatosha,ni uungwana tu.
 
Hata kama Rais ana element za siasa za chuki lakini sio kwa kushambuliwa kwa namna wanavyofanya wapinzani. Rais ni taasisi kumbuka.
Ukitaka kutendewa kiungwana na uwe muungwana. Shida ni kuwa CCM kwa ujumla wao wanaona kama vile wanaingiliwa ktk uendeshaji wa wananchi.
 
Una ushahid kwamb kwend kwa mama ake alitak kutoroka au unashabikia tu mtu famous vle atoroke aende wap
Hlo unaloliombea halitafanikiwa hata kidogo wabunge tutapat weng kuliko 2015
VIVA CHADEMA
Vivaaaa
 
Huyu dogo mimi namchukulia kama mtu wa mzaha mzaha. Anawachuuza watanzania kwa kuwaambia uoga ndio umetufikisha hapa na kuhimiza watu wasiwe waoga kumbe yeye ndiye muoga number one,analiamsha dude halafu anakimbilia kujificha kwa mama, bado najiuliza pia kama huyo mama nae ni mtu serious na inaashiria malezi ya mama ndiyo yamemfikisha hapo alipo,mtoto wa kike ana guts za kusimama hadharani kumkashifu Rais wa nchi halafu anakimbilia kwa mama! Lakini pia najiuliza kama huyo mama nae hakustahili kubebwa kwa kosa la kumficha mhalifu huku akijua kuwa anatafutwa na dola,alifaa kuchukuliwa kwa "Tanganyika jeki" apelekwe nae akapewe ujumbe wa MAMA MKANYE MWANAO.
 
Lakini yeye anaruhusiwa kwenda kwenye media na kusambaza chuki? Tumieni akili zenu kufikiri.
Tatizo lako unafikiri kuwa ukosefu wa adabu ndio kutumia akili vizuri. Kama umelelewa vizuri utajua kuheshimu watu, nayo ni akili nzuri, kama kila mtu unamuona sawa na wewe tu, sio sawa.
 
Ukimpata Mangu na Kova au Mwema waulize vipi maisha ya mtaani? Bado wale marafiki wanao japo walikuwa watumishi wa umma?.. Sasa vyeo vya iteuzi na vya kisiasa havina dhamana.
 
SIKU MBILI ZA HALIMA MDEE RUMANDE OYSTERBAY
Usiku wa kuamkia leo tarehe 6 Julai, 2017 ni usiku wa pili wa kulala korokoroni Mwenyekiti wa BAWACHA taifa, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Kawe CHADEMA Halima James Mdee.

Katika rumande ya Polisi Oysterbay wilayani Kinondoni, Mdee ameendelea kutumikia masaa 48 aliyopewa na Mkuu wa Awilaya ya Kinondoni Ally Hapi kwa kosa la kumdhihaki Mh. Rais Dr. John Magufuli na kutoa maneno machafu yanayoweza kuvunja amani.

MATAMSHI YA MDEE
Akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya CHADEMA Mdee ananukuliwa kudai kuwa Mh. Rais Magufuli amekua na "tabia ya hovyo...", "...ipo siku ataagiza watanzania (wake kwa waume) watembee vifua wazi...". Maneno mengine ni "...Rais lazima afungwe breki...",apewe semina elekezi n.k.

UCHOCHEZI
Halima Mdee anatajwa kutoa kauli za uchochezi kama vile "...woga wetu wananchi ndio unaotugharimu nchi hii..." "...watakaomfunga breki ni nyinyi wananchi...", maneno yanayotajwa kupandikiza na kuhamasisha chuki na vurugu kwa wananchi.

KUKAMATWA KWAKE
Baada ya amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mdee alianza harakati za kutoroka na kuruka mtego wa Polisi. Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni lilimkamata akiwa amejificha nyumbani kwa mama yake Kibamba wilayani Ubungo tayari kwa kutoroka.

RUMANDE
Halima Mdee anatajwa kuhifadhiwa katika rumande ya watuhumiwa wa uhalifu wa jinsia ya kike katika kituo cha Oysterbay Kinondoni.

BUNGE KUMUWAJIBISHA TENA
Akiwa bado anatumikia kifungo cha kutohudhuria Bunge hadi mwaka 2018, Halima Mdee ameingia tena matatani.

Kufuatia matamshi ya Mdee na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema, Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza kamati ya Kinga na Madaraka ya Bunge kukutana haraka kujadili kitendo cha Mbunge huyo kutoa matashi ya kulifedhehesha Bunge. Akikutwa na hatia huenda akaongezewa adhabu nyingine.
Duh!! kwa hiyo analiamsha dude halafu anakimbilia kwa mama kujificha,kwa hiyo wapiga kura wake tukiwa na shida nae tumfate kwa mamaake? Kumbe tunaongozwa na "mtoto wa mama"! Au mama ndiye alimtuma akaliamshe na sasa alikuwa anarudisha majibu?
 
Back
Top Bottom