Siku Manchester United iliposhushwa daraja

Siku Manchester United iliposhushwa daraja

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
Ni mashabiki wachache wa Manchester United wanaikumbuka siku ile ambayo timu yao ilishushwa daraja. Ilikuwa msimu wa 1973/74 na mechi ya mwisho ya ligi ilikuwa tarehe 27 Aprili 1974. Kwa mashabiki wa Manchester United wataikumbuka tarehe 27 April 1974 kama "the worst day in the history of football". Kwa wasioipenda Manchester United, wanaikumbuka hiyo tarehe kama "the best day in the history of football." Kwa mara ya kwanza Manchester United ilishushwa daraja baada ya kucheza kwenye ligi daraja la kwanza kwa miaka 36.

Lakini huwezi kuongelea tarehe 27 April 1974, siku ambayo Manchester United ilishishuka daraja, bila kumwongelea Denis Law. Denis Law ni legend Old Trafford. Alijiunga na Manchester United mwaka 1962 akitokea Manchester City. Aliichezea Manchester United kwa muda wa miaka 11, ambapo alifunga magoli 237 kwenye mechi 404 alizocheza. Mashabiki wa Manchester United walimwita "The King" na "The Lawman".

Itakumbukwa pia kuwa Manchester United ilikuwa ikisuasua kwenye ligi baada ya timu kupata ajali ya ndege Munich Ujerumani mwaka 1958 ambapo abiria 20 kati ya 44 walipoteza maisha. Kati ya abiria 20 waliofariki, saba walikuwa wachezaji wa Manchester United. Kwa hiyo, baada ya ajali hiyo, Manchester United ilikuwa wanapambana mara nyingi kuepuka kushuka daraja.

Baada ya kuichezea Manchester United kwa miaka 12, Denis Law alihamia Manchester City msimu wa 1973/74 bila ada (free transfer). Manchester United walikuwa hawamhitaji tena maana kiwango chake cha mpira kilikuwa kimeshashuka na umri pia ulikuwa umesogea. Pia George Best na Bob Chalton walikuwa wameshaondoka.

Katika mechi ya mwisho ya ligi msimu wa 1973/74, Manchester United ilicheza na Manchester City Old Trafford. Manchester United ilitakiwa kushinda ile mechi ili isishuke daraja. David Law alicheza lakini tokea mwanzo alionekana kutokuwa na raha maana kama timu yake kipenzi (Manchester United) ingefungwa basi ingeshushwa daraja.

Mpaka dakika ya 80 mechi ilikuwa bila bila. Mnamo dakika ya 81, Denis Law aliifungia Machester City goli kwa kisigino. Lilikuwa goli zuri na tamu lakini siyo kwa mshabiki yoyote wa Manchester United. Denis Law mwenyewe hakushangilia kwa kufikiri kuwa goli lake la kisigino lingeishusha daraja Manchester United. Mara tuu baada ya kufunga like goli, alibadiliswa huku akitoka uwanjani akiwa ameinamisha kichwa chini kwa masikitiko makubwa ya kuishusha daraja Manchester United.

Baada ya Denis Law kutoka uwanjani, mashabiki wa Manchester United walivamia uwanja na kumlazimisha refa kumaliza mechi katika dakika ya 85. Siku chache baadae, chama cha mpira kilifanya mapitio ya mechi ile na kusimama na matokeo ya mechi. Kwa hiyo, Manchester City ikawa imeshinda bao moja lililofungwa na Denis Law kwa kisigino na Manchester United kushushwa daraja.

Hata hivyo, ilikuja kugundulika baada ya mechi kuwa bado Manchester United ingeshuka daraja bila kutokana na matokeo ya ile mechi. Hii ilitokana na matokeo ya kwenye mechi nyingine za mwisho zilizochezwa siku ile. Lakini Denis Law aliamini kabisa kuwa goli lake la kisigino limeishusha daraja Manchester United.

Msimu uliofuata (1974/75) Manchster United ilicheza kwenye ligi ya daraja la pili na kufanikiwa kurudi tena ligi ya daraja la kwanza katika msimu wa 1975/76.

 
Last edited by a moderator:
acheni fitna vijana...leo mnacheza na chelsea u better concetrate on the game rather than lookin at the past
 
  • Thanks
Reactions: EMT
duh.! Kahistoria katamu ningefurahi kama kangejirudia siku za karibuni,ila kwa sasa naona kama ni ndoto. Marefa wanaiogopa ManU, na FA ya sasa sio kama ya zama hizo.!
 
Ahsante sana EMT,

Ni bora mashabiki wa sasa wakawa wanakumbushwa historia chungu kama hizi....Kuna watu wanaona kama Man U ya sasa hivi ni immortal....

Pia wengi hata hawajui kwamba kwenye miaka ya 1980...Liverpool ndiyo ilikuwa timu yenye jina kubwa kuliko zote Uingereza. Labda itawasaidia watu kujua kwamba zama huwa zina mwisho wake!!

800px-Liverpool_F.C._League_Progress_1893-2012.PNG


Ni hayo tu,
 
Last edited by a moderator:
acheni fitna vijana...leo mnacheza na chelsea u better concetrate on the game rather than lookin at the past
We dogo acha ututo wako........

Kucheza na Chelsea na Historia hii tamu kuna uhusiano gani?....Wewe kila siku unataka kusikia mazuri tu ya Man Utd.........Jamvini humu kuna mabandiko mengi tu, kama unaona hili halikufai si usee tu uende kwenye bandiko la 'Man Utd Hamshikiki'..........

Ukweli utabaki pale kwamba Man Utd walishawahi kushuka daraja....Period.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Simply History it does not affect anything in taking the title this season, as well as beating Tottenham today
 
Hiyo ni Man ya miaka hiyo, ingekua ya miaka hii wengekua walishapewa penalt na Denis Law lazima angepewa kadi nyekundu.
 
Historia ina machungu yake na hili ni moja ya hayo...Today and the whole future is at our disposal..what do we do now? We take it.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mavi ya kale hayanuki mtakufa na kijiba cha roho na timu zenu za kufanyia daeit
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Yap.. a good glimpse of history! Maana watz wengi wameanza kuangalia/kufuatilia int. football miaka ya 90. Ndivyo football ilivyo, ups and downs.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
tokea naikumbuka hii timu siipendi sijui kwanini baada ya kuiacha Everton nilikwenda Arsenal
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Itakumbukwa pia kuwa Manchester United ilikuwa ikisuasua kwenye ligi baada ya timu kupata ajali ya ndege Munich Ujerumani mwaka 1958 ambapo abiria 20 kati ya 44 walipoteza maisha. Kati ya abiria 20 waliofariki, saba walikuwa wachezaji wa Manchester United. Kwa hiyo, baada ya ajali hiyo, Manchester United ilikuwa wanapambana mara nyingi kuepuka kushuka daraja.

Baada ya kuichezea Manchester United kwa miaka 12, Denis Law alihamia Manchester City msimu wa 1973/74 bila ada (free transfer). Manchester United walikuwa hawamhitaji tena maana kiwango chake cha mpira kilikuwa kimeshashuka na umri pia ulikuwa umesogea. Pia George Best na Bob Chalton walikuwa wameshaondoka.

Mkuu inaonekana wewe uko kwenye muono wa "the best day in the history of football"(Gooners'/Scoucers' point of view?). Kumbuka kwamba 1964 Man utd ilimaliza ya pili kwenye ligi na ilishinda ligi mwaka 1965 na 1967. Mwaka 1968 ilichukua European cup ikiwafunga Benfica 4-1 kumbuka Eusebio alikuwa anachezea Benfica muda huo. Kwa mafanikio haya inabidi uangalie tena maana yako ya kusuasua kwenye ligi kulikosababishwa na Munich accident na relegation ya 1974.

Sababu za Man utd kuwa relegated ni pamoja na kuwepo kwa wachezaji wenye umri mkubwa baada ya Matt Busby kuacha kazi na McGuiness kuchukua nafasi yake, na baadaye Busby kurudi na baada ya hapo akaja meneja mwingine O'Farell ambaye alishindwa kumudu tabia ya baadhi ya wachezaji kama Best. Kisha Charlton, Faulkes na Best walistaafu. Pia muda huu(1970-74) kulikuwa na kikundi wachezaji wakongwe(old guard clique) ambao walikuwa hawaongei na wachezaji wapya wala kuwapa ushirikiano wa kutosha na hili lilikuwa tatizo kubwa.

Alipokuja meneja mwingine Docherty december 1972 akaanza kujenga timu mpya ikiwa na vijana wengi mpaka kufikia muda timu inashushwa daraja mchezaji wa kikosi kilichochukua kombe la ulaya alikuwa ni kipa peke yake Alex Stepney

Pia kuuzwa kwa Law ni sababu nyingine iliyozidi kuivuruga timu

Hata hivyo licha ya timu kushushwa daraja mashabiki waliendelea kuwa kuishangilia timu yao na ilikuwa nafasi kwa timu kujijenga upya.
 
Kwa hiyo unataka tufanyeje?? Kuweke turubai tusikitike au??


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom