Mkuu inaonekana wewe uko kwenye muono wa "the best day in the history of football"(Gooners'/Scoucers' point of view?). Kumbuka kwamba 1964 Man utd ilimaliza ya pili kwenye ligi na ilishinda ligi mwaka 1965 na 1967. Mwaka 1968 ilichukua European cup ikiwafunga Benfica 4-1 kumbuka Eusebio alikuwa anachezea Benfica muda huo. Kwa mafanikio haya inabidi uangalie tena maana yako ya kusuasua kwenye ligi kulikosababishwa na Munich accident na relegation ya 1974.
Sababu za Man utd kuwa relegated ni pamoja na kuwepo kwa wachezaji wenye umri mkubwa baada ya Matt Busby kuacha kazi na McGuiness kuchukua nafasi yake, na baadaye Busby kurudi na baada ya hapo akaja meneja mwingine O'Farell ambaye alishindwa kumudu tabia ya baadhi ya wachezaji kama Best. Kisha Charlton, Faulkes na Best walistaafu. Pia muda huu(1970-74) kulikuwa na kikundi wachezaji wakongwe(old guard clique) ambao walikuwa hawaongei na wachezaji wapya wala kuwapa ushirikiano wa kutosha na hili lilikuwa tatizo kubwa.
Alipokuja meneja mwingine Docherty december 1972 akaanza kujenga timu mpya ikiwa na vijana wengi mpaka kufikia muda timu inashushwa daraja mchezaji wa kikosi kilichochukua kombe la ulaya alikuwa ni kipa peke yake Alex Stepney
Pia kuuzwa kwa Law ni sababu nyingine iliyozidi kuivuruga timu
Hata hivyo licha ya timu kushushwa daraja mashabiki waliendelea kuwa kuishangilia timu yao na ilikuwa nafasi kwa timu kujijenga upya.