Siku Manchester United iliposhushwa daraja

Siku Manchester United iliposhushwa daraja

Kitu kilichonifurahisha Timu yetu ilishuka Daraja kwa Taaaabu Sana Kumbe...
 
Binafsi najua FC Barcelona,Real Madrid na Atletico Bilbao ndizo hazijashuka daraja,sidhani kuna nchi nyingine ulaya zaidi ya Spain,ambazo timu hazijawahi kushuka daraja ukiachilia mabara mengine sina habari nazo(unofficially).

Kwahiyo hata bara la Africa hulijui kuwa lina timu ambazo hazijawahi kushuka au kushuswa DARAJA? Simba au Yanga? ila mimi Nahisi Yanga kama ilishawahi shuka daraja kama sikumbuk kisawa sawa lol
 
asante kwa istoria mkuu, nilikuwa sijazaliwa wala kufikiriwa...Man u chama langu!!!
 
Kwahiyo hata bara la Africa hulijui kuwa lina timu ambazo hazijawahi kushuka au kushuswa DARAJA? Simba au Yanga? ila mimi Nahisi Yanga kama ilishawahi shuka daraja kama sikumbuk kisawa sawa lol
Tuwaulize kina Ndolanga,sidhani kama Yanga ilishashuka,tumuulize Gang Chomba,ila nakumbuka Simba ilinusurika miaka 3 mfululizo 1987,1988 na 1989 kina John Makelele ZigZag alimuambia Sahau Kambi hatosahau marehemu kwa sasa(RIP Sahau Kambi)
 
Dah sasa QPR,Aston villa,Wigan,Reading bila kuwasahau Newcastle inawalazimu wasome alama za nyakati.
 
Asante sana EMT umewafunza wengi wenye roho mbaya kwa Man UTD kwamba kuteleza si kuanguka na kila kitu kina mwanzo na mwisho.Hiyo ndio raha ya mpira huwezi kuzungumzia historia ya EPL bila MAN UTD na mahasimu Looserfool.Mashabiki matonge wamepata cha kuongea kijiweni...............Shukhurani EMT. :cheer2:
 
Man U ndio chama Kubwa Duniani na Tajiri kuliko klabu zote za soccer Duniani... Mwisho wa Kunukuu
 
Mavi ya kale hayanuki mtakufa na kijiba cha roho na timu zenu za kufanyia daeit

Chifu, umenivunja mbavu..

Timu za kufanyia diet?!?

Nadhani vibonge wote wasisumbuke kuingia gharama za gym, daktari n.k. Bali wawe mashabiki wa Arsenal na Liverpool.

Hii ni kali ya kufungulia mwaka.
 
Mkuu inaonekana wewe uko kwenye muono wa "the best day in the history of football"(Gooners'/Scoucers' point of view?). Kumbuka kwamba 1964 Man utd ilimaliza ya pili kwenye ligi na ilishinda ligi mwaka 1965 na 1967. Mwaka 1968 ilichukua European cup ikiwafunga Benfica 4-1 kumbuka Eusebio alikuwa anachezea Benfica muda huo. Kwa mafanikio haya inabidi uangalie tena maana yako ya kusuasua kwenye ligi kulikosababishwa na Munich accident na relegation ya 1974.

Sababu za Man utd kuwa relegated ni pamoja na kuwepo kwa wachezaji wenye umri mkubwa baada ya Matt Busby kuacha kazi na McGuiness kuchukua nafasi yake, na baadaye Busby kurudi na baada ya hapo akaja meneja mwingine O'Farell ambaye alishindwa kumudu tabia ya baadhi ya wachezaji kama Best. Kisha Charlton, Faulkes na Best walistaafu. Pia muda huu(1970-74) kulikuwa na kikundi wachezaji wakongwe(old guard clique) ambao walikuwa hawaongei na wachezaji wapya wala kuwapa ushirikiano wa kutosha na hili lilikuwa tatizo kubwa.

Alipokuja meneja mwingine Docherty december 1972 akaanza kujenga timu mpya ikiwa na vijana wengi mpaka kufikia muda timu inashushwa daraja mchezaji wa kikosi kilichochukua kombe la ulaya alikuwa ni kipa peke yake Alex Stepney

Pia kuuzwa kwa Law ni sababu nyingine iliyozidi kuivuruga timu

Hata hivyo licha ya timu kushushwa daraja mashabiki waliendelea kuwa kuishangilia timu yao na ilikuwa nafasi kwa timu kujijenga upya.

Heshima kwako chifu.

Hiyo ndiyo dawa za wale kama akina EMT wanaosimulia historia nusunusu kukidhi matakwa na mitazamo yao.

Yaani amesahau kwamba baada ya baada ya ajali ya Munchen, miaka 10 baadaye Man United ikaja kuwa timu ya KWANZA UINGEREZA kubeba kombe la klabu bingwa Ulaya.

Mwanahistoria anaruka matukio hapo katika na kushukia 1974?!? Jibu ni kuwa, ili kukidhi mtazamo wake.

Historia ikiandikwa kwa mlengo wa kukidhi matakwa, mapenzi, matazamio na mitazamo ya mwandishi, hakika historia hiyo lazima iwe potofu.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana EMT umewafunza wengi wenye roho mbaya kwa Man UTD kwamba kuteleza si kuanguka na kila kitu kina mwanzo na mwisho.Hiyo ndio raha ya mpira huwezi kuzungumzia historia ya EPL bila MAN UTD na mahasimu Looserfool.Mashabiki matonge wamepata cha kuongea kijiweni...............Shukhurani EMT. :cheer2:

Damn! I missed this kinda stuff.

Mashabiki matonge!!
Navoyne hao ndiyo wakoje?
 
Last edited by a moderator:
Heshima kwako chifu.

Hiyo ndiyo dawa za wale kama akina EMT wanaosimulia historia nusunusu kukidhi matakwa na mitazamo yao.

Yaani amesahau kwamba baada ya baada ya ajali ya Munchen, miaka 10 baadaye Man United ikaja kuwa timu ya KWANZA UINGEREZA kubeba kombe la klabu bingwa Ulaya.

Mwanahistoria anaruka matukio hapo katika na kushukia 1974?!? Jibu ni kuwa, ili kukidhi mtazamo wake.

Historia ikiandikwa kwa mlengo wa kukidhi matakwa, mapenzi, matazamio na mitazamo ya mwandishi, hakika historia hiyo lazima iwe potofu.

Thread haihusu siku Manchester United ilipokuwa timu ya kwanza Uingereza kubeba kombe la Klabu Bingwa Ulaya.

Thread inahusu siku Manchester United iliposhushwa daraja.
 
Hao hawajui kitu ila wanashabikia shabikia tu............hisia zao ugeuza facts..........kwa wanoko kule wamejaa tele hawajui kwanini wanaichukia Man UTD, utasikia basi tu siwapendi.
 
Thread haihusu siku Manchester United ilipokuwa timu ya kwanza Uingereza kubeba kombe la Klabu Bingwa Ulaya.

Thread inahusu siku Manchester United iliposhushwa daraja.

Kwa vile umeongelea suala la historia ya Man United, ulipaswa kuelezea kwa kina kilichotokea.
Huwezi kuelezea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964, bila kuzungumzia uhuru wa Tanganyika wa mwaka 1961.

Kubali tu unatoa historia ya Man United kwa hisia na matamanio yako.
 
Kwani hii thread inaongelea historia ya Manchester United? Kwani Manchester United iliungana na ni timu gani?

Kwa hiyo basi ulitaka kabla ya kuelezea siku Manachester United iliposhuka daraja nianze kwanza kwa kuelezea hisotoria ya Manchester United kuanzia mwaka 1878 ilipokuwa inaitwa Newton Heath LYR Football Club (Tanganyika) kabla ya kubadilisha jina mwaka 1902 na kuitwa Manchester United (Tanzania)? Ndivyo ulivyotaka eh?

Kubali tu unatoa historia ya Man United kwa hisia na matamanio yako.

Rudi kasome thread upya. Hii thread siyo kwa ajili ya historia ya Manchester United.

Hii thread ni kujaribu kuelezea siku Manchester United iliposhushwa daraja.

Kushushwa daraja ni sehemu ndogo sana ya historia ya Manchester United.

Niitamani Manchester United kwa sababu gani? I'm only attracted to women. Sorry.
 
Itakumbukwa pia kuwa Manchester United ilikuwa ikisuasua kwenye ligi baada ya timu kupata ajali ya ndege Munich Ujerumani mwaka 1958 ambapo abiria 20 kati ya 44 walipoteza maisha.......Kwa hiyo, baada ya ajali hiyo, Manchester United ilikuwa wanapambana mara nyingi kuepuka kushuka daraja.

Chifu, kwa ulichoandika hapo juu na unachokisema juu ya dhumuni la uzi wako, unajichanganya sana.

Ndiyo maana nimekwambia umeandika haya kwa hisia na matamanio yake (simaanishi kwamba unaitamani Man United; namaanisha matamanio yako ya kuandika kile kinachokufurahisha).

Huwezi kuandika hayo juu, halafu wapenzi wa Man United wakae kimya. Kwani unasahau kwamba pamoja na ajali ya Munchen, Man United ikawa timu ya kwanza toka Uingereza kushinda taji la klabu bingwa barani Ulaya mwaka 1968.

Bila kusahau ni katika miaka ya 1964, 1966 na 1968, wachezaji wa Man United Denis Law, Bobby Charlton na George Best waliweza kushinda tuzo za Ballon d'Or wakiwa Man United.

Pia kwa kipindi hicho unachodai kwamba Man United ilikuwa ikisuasua, msimu wa mwaka 1964-65 na mwaka 1966-67, timu ilishinda ubingwa wa daraja la kwanza.
Mwaka 1963 timu ikashinda kombe la FA kwa mara ya tatu. Ikashinda FA Charity Shield mwaka 1965 (kwa ushindi wa pamoja na Liverpool, baada ya kutoka droo ya 2-2) na 1967.

Sasa kusuasua kupi ulikokuongelea? Mtu unaongelea kushuka kwa timu mwaka 1974; unaunganisha na tukio la ajali ya mwaka 1958. Unadai timu ilikuwa ikisuasua baada ya ajali; lakini huzungumzii kiukweli kilichotokea kati ya mwaka 1959 hadi 1973.

Ndiyo maana nikakwambia, ni hisia tu ndizo zimekusukuma uandike historia isiyo kamili. Huwezi kuunganisha hayo matukio na tukio la kushuka daraja, bila kugusia yote yaliyotokea.
 
Hata hivyo licha ya timu kushushwa daraja mashabiki waliendelea kuwa kuishangilia timu yao na ilikuwa nafasi kwa timu kujijenga upya.

I hope wataendelea kufanya hivyo baada ya Fergie kutangaza rasmi kustaafu mwishoni mwa msimu huu.

I hope watakuwa wavumilivu na huyo kocha mpya mtarajiwa hasa pale timu inaposhindwa kufanya vizuri kama Arsenal.

I hope baada ya Fergie kuondoka Man Utd haitakuwa kama Liverpool.

I really hope all of the above.

I really do.
 
Hahahahahahaaaa!
 
Hahahahahahaaaa!

Mbona wacheka? I really do.

Mashabiki wa Man Utd are in for a shock.

Mbaya Fergie kashtukiza mno.

He didn't give them time to reflect and cool down.

Leo ni siku ya majozi kwao; alomost karibu sawa na siku ile timu iliposhoshwa daraja.

Yaani hata huu ubingwa waliochukua juzi hauna tena raha.

How can you celebrate whilst the big boss is quiting?
 
Back
Top Bottom