Siku hizi simwambii mke wangu asante kwa chakula

Siku hizi simwambii mke wangu asante kwa chakula

Huu unaweza kuwa ushauri mzuri, akunyimaye mpe.
Ushauri kama huu ni hatari sana. Kulikuwa na rafiki yangu akajaribu kupika kama mara mbili, mke wake akaanza kusifia kuwa mumewe anapika vizuri na chakula ni kitamu. Alipoacha ikawa nongwa. Katika ndoa kitu ambacho siyo endelevu kiache kabisa la sivyo kinaongeza ufa. Ni afadhali akale kwa mama ntilie akirudi ameshiba, hiyo itamfanya asituke
 
Sasa ikiwa H/G anafanya kila kitu cha ndani ya nyumba kimebakia nini amabacho hawezi kufanya?pengine H/G anauwezo wa
kumuhudumia mumeo kuliko hata mama mwenye nyumba...
Najua una uzoefu wa ndoa kuliko wengi humu. Kawaida ndoa ni ngumu na lazima ukubali mapungufu ya mwenzako na yeye ayakubali ya kwako. Ndoa haziendi kimikiki zinahitaji uvumilivu wa hali ya juu kuliko kufanya kazi na JPM. Kwa sisi wanaume kama mkeo hajisikii kukupikia usilazimishe, mbona tunakula hotelini na tunadai chakula ni kitamu? Kubali kuwa dada naye ni kama mtoto wako akipika yeye sawa. Kuna vitu mke wako anapenda kukufanyia mpende kwa hilo tu ili maisha yasonge mbele. Ila tukumbuke kama mkeo anafanya kazi na anachangia kwa hali na mali matumizi ya familia kuna vitu naye atakuiga.
 
Haya mambo yapo complicated sana. Mnatoka wote asubuhi, mnarudi wote usiku (hasa kwa wakazi wa Dar) ni ngumu mke kuwa committed jikoni. Tuwe tu wakweli, kuna maeneo ambayo kweli watu wakitoka job inawezekana sana kupika.

Tusiwe too conservative jamani. Hata wewe once in a while ingia jikoni upike.

Eli79

Unakuta watu wanaishi Upanga. Mke ana usafiri wake na kazini ni posta. Kurudi nyumbani ni haraka kuliko mke anayeishi Gongo la Mboto na anatumia daladala. Halafu umwambie huyu mama wa Gongo la Mboto akifika nyumbani saa mbili usiku aanze kuwasha jiko ( sio wote wenye gesi) apike.

Huo ni utumwa hiyo sio ndoa.
 
Najua una uzoefu wa ndoa kuliko wengi humu. Kawaida ndoa ni ngumu na lazima ukubali mapungufu ya mwenzako na yeye ayakubali ya kwako. Ndoa haziendi kimikiki zinahitaji uvumilivu wa hali ya juu kuliko kufanya kazi na JPM. Kwa sisi wanaume kama mkeo hajisikii kukupikia usilazimishe, mbona tunakula hotelini na tunadai chakula ni kitamu? Kubali kuwa dada naye ni kama mtoto wako akipika yeye sawa. Kuna vitu mke wako anapenda kukufanyia mpende kwa hilo tu ili maisha yasonge mbele. Ila tukumbuke kama mkeo anafanya kazi na anachangia kwa hali na mali matumizi ya familia kuna vitu naye atakuiga.
Nimekuelewa ila kama unavyosema kila mtu na mapungufu yake wengine wanadeka,nikupe mfano Mume wangu mie
Alikuja mama yake nyumbani tukawa nae sasa nimekwenda kazini nikampigia cm kumuliza Mkwe atakula nini ili nipite sokoni
kaseme atakachokula mumeo,nikamwambia ametaka ugali ntampikia nirejea,nimefika nyumbani mkwe kaingia jikoni kapika
sio kibaya chakula kitamu sanaa,lakini mume wangu kaniuliza why hukunipikia leo nikamwambia Mama amepika,hakusema kitu,siku ya pili mie nikokazini mamake kaingia jikoni kamfata Mama please usipike napenda mke wangu anavyopika
na anajua nini napenda nimerudi tuu mkwe kaaanza mmmmmmm "leo hii mie sijui kupika,chakula changu kibaya,mkewe ndio anajua mapishi haya mama umeshinda ingia jikoni ukampikie mumeo, mie uso ulikua mdogo na ilikua issue akawambia watoto wake wote,sasa kuna wanaume wengine ndio walivyo na inategemea na mazowea ulomzowesha..
 
Kwa mwanamke aliyepata malezi bora toka kwa wazazi wake hawezi mwachia house girl kila siku au kila kitu, hiyo haipendezi nikuiweka ndoa bond, baadaye tunalalamika dada kanichukulia mme, mme ni mtoto mkubwa ndani ya ndoa siku akiponyoka mbio kwa mchungaji wakati mchawi mwenyewe.
 
alikuambia yeye anatimiza majukumu yake yooote kiutamaduni wetu? huyo mke anatoka kazini saangapi?

Yaani hata weekend yuko kazini hapiki? kazi ipo
 
Nimekuelewa ila kama unavyosema kila mtu na mapungufu yake wengine wanadeka,nikupe mfano Mume wangu mie
Alikuja mama yake nyumbani tukawa nae sasa nimekwenda kazini nikampigia cm kumuliza Mkwe atakula nini ili nipite sokoni
kaseme atakachokula mumeo,nikamwambia ametaka ugali ntampikia nirejea,nimefika nyumbani mkwe kaingia jikoni kapika
sio kibaya chakula kitamu sanaa,lakini mume wangu kaniuliza why hukunipikia leo nikamwambia Mama amepika,hakusema kitu,siku ya pili mie nikokazini mamake kaingia jikoni kamfata Mama please usipike napenda mke wangu anavyopika
na anajua nini napenda nimerudi tuu mkwe kaaanza mmmmmmm "leo hii mie sijui kupika,chakula changu kibaya,mkewe ndio anajua mapishi haya mama umeshinda ingia jikoni ukampikie mumeo, mie uso ulikua mdogo na ilikua issue akawambia watoto wake wote,sasa kuna wanaume wengine ndio walivyo na inategemea na mazowea ulomzowesha..
Hizo ni ajali tunazosababisha sie wanaume. Katika maisha lazima ujue mama yako na mkeo ni kama wake wenza. Lazima ujue jinsi ya kumweleza mama yako kuhusu mkeo na jinsi ya kumweleza mkeo kuhusu mama yako. Akinamama huwa kila siku wanatuona kama watoto bado ukimkataza kupika kama alivyofanya ni shughuli pevu. Mwisho wa yote watadhani umemloga wakati si sawa. Mwisho nakupongeza kwa kuwa mke bora
 
Hii ni wake up call kwa wanawake tusijaribu kuona maisha ya ndoa yana usasa turudi jikoni kwenye majukumu ya kumpikia baba. Kwa mwanamke anayefanya kazi atafute siku na mida binafsi ili akae jikoni hawa wasichana wa kazi wengine hawajui kupika vizuri jamani sasa ukute umechoka sana kazini unarudi home unakuta dada amepika mnakula mezani chakula hakina taste unafika kitandani nako umechoka hutaki kuguswa mume lazima aunganishe makosa anaanza kuona huna umuhimu maana jikoni haupo kwenye kuandaa chakula na 6x6 unampa kwa nadra .
Kwa jinsi alivyoandika mleta uzi huyu ni aina ya mume ambaye anatamani kupikiwa na mkewe ili ale nyumbani na alipoona mke hapiki akatoa taarifa ya hali ya hatari sasa ameanza kuonyesha hatendewi haki anazungumza nje muda si mrefu huyo mke atabaki na kazi yake bila mume. Mke anapaswa kubadilika mara moja sana na kurudi jikoni. M
Aiepushe pia familia yake na mauzauza ya wadada wa kazi anaweza kuwalisha mikojo ya kutosha bila sababu wasichana wa kazi wa sasa wako kikatili zaidi shairilooooo[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]
 
mmmm Balaa mwenyezi mungu atunusuru mimi na wanawake wenzangu,ndoa zinatafrani zake jamani,lakini hata kama unafanya kazi weekend unaweza ukapika na hata siku za kawaida unaweza kumwambia dada akutayarishie wewe ukifika una
changanya kwanza sikuizi sio kama zamani unapika na mikaa Gas unaivisha mara moja,unaweza kubiwa mume kwa vitu vidogo kama hivi halafu unatafuta mchawi..
ujinga tu wa wanawake wa siku hizi...
 
Hizo ni ajali tunazosababisha sie wanaume. Katika maisha lazima ujue mama yako na mkeo ni kama wake wenza. Lazima ujue jinsi ya kumweleza mama yako kuhusu mkeo na jinsi ya kumweleza mkeo kuhusu mama yako. Akinamama huwa kila siku wanatuona kama watoto bado ukimkataza kupika kama alivyofanya ni shughuli pevu. Mwisho wa yote watadhani umemloga wakati si sawa. Mwisho nakupongeza kwa kuwa mke bora
Asante,ila sio mke bora najitahidi siunajua sikuizi hata malezi ya mume pia unatakiwa uwe mbunifu ..lol
 
Back
Top Bottom