Siku hizi simwambii mke wangu asante kwa chakula

Haya mambo yapo complicated sana. Mnatoka wote asubuhi, mnarudi wote usiku (hasa kwa wakazi wa Dar) ni ngumu mke kuwa committed jikoni. Tuwe tu wakweli, kuna maeneo ambayo kweli watu wakitoka job inawezekana sana kupika.

Tusiwe too conservative jamani. Hata wewe once in a while ingia jikoni upike.
Jamaa anasema angalau mara moja moja.
 
Hii kauli imenishutua, nikauli kutoka kwa rafiki yangu ninayemfahamu kwa muda mrefu. Ndoa yao ina miaka 5 sasa na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike, kwa haraka haraka unaweza kuiona ndoa yao kama ni ndoa imara na yenye upendo mkubwa na kutamani kujifunza kutoka kwao.

Majuzi nilikutana na huyu rafiki yangu tulikuwa na maongezi ya kikazi, katika maongezi yetu tukawa tumeingiza mambo ya familia, ndipo nilishutushwa na kauli ya rafiki yangu "siku hizi simwambii mke wangu asante kwa chakula" nikamuuliza, kwa nini? "Tangu apate hii kazi aliyonayo sasa yapata miaka miwili sili chakula kilichopikwa kwa mikono yake angalau mara moja moja, kwa siku chache za mwanzoni alijitahidi lakini haikudumu kwa muda mrefu akaacha kabisa binti wa nyumbani akawa ndiyo muhusika kwa 100%.
Imenichukua muda mrefu kila nimalizapo kula chakula hasa umwambia mke wangu asante kwa chakula, kilikuwa ni kitamu.

Kwa sasa nimegundua kuwa ninachokifanya ni unafiki tu wa kumfurahisha mke wangu, huku nikiwa na manunguniko moyoni. Kwa sasa nikimaliza kula nasema asante aliyepika chakula, kilikuwa kitamu sana, naona hii kauli imemshutua na kumchanganya kidogo"
Nikamuuliza kwa nini anatumia njia hii badala ya kukaa naye wakaliongelea hili tatizo, akasema "nimekwisha ongea naye mara nyingi ila amekuwa na sababu nyingi mara kuchoka, mara ubize wa kazi, sababu nyingi tu. Natamani angalau mara moja moja nile chakula chakula kilichopikwa kwa mikono ya mke wangu".

Wanawake jitahidi waume zenu wale chakula kilichopikwa kwa mikono yenu angalau mara moja moja.
Naomba nikuulize swali la kizushi....
Wewe hapo nyumbani kwako umeshawahi kupika?...Manake hizi ni zama zingine .......
 
unajua sometimes nikienda vijijini natamani ningekua na ujasiri kama wao manake mwanamke asubuhi anaenda kulima
akirejea anaenda kuchota maji na plus kupika,sisi wa mjini ambao ni Pen pusher mtu yuko kazini A/C full na akija nyumbani
hana mda wa kuangalia homework za watoto,wala kupika yeye na cm tuu kila kitu Dadaaaaaaaaaaa mpe mtoto uji,mara dadaaa ulisha pika chakula cha Baba,Dadaaaaaaaaaaa zile nguo ndogo za Baba umeziweka wapi yani 24/7 ni dadaaaaa eeh Dadaa halafu wana sema Baba ana mnunulia zawadi Dada ina maana gani...
halafu kuna usemi wa kwamba hujanioa niwe house girl wako yeye kashikilia mke ni pambo so house girl ni mtu mwingine.
 
Hilo tatizo limekuwa sugu kwa familia nyingi, wanawake mjitambue kujuwa umuhimu wenu ktk ndoa
Familia za wenye kujielewa,Baba pia hushiriki katika kupika.
Hii ni ngumu kuelewa sababu watu wa aina hii wapo katika level nyingine.
 
namuunga mkono.
ni unafiki kumwambia mke wako ahsante kwa chkula kitamu wakati hausiki hata kuweka chumvi.

amwambie tena na tena .angalau weekend vinginevyo nyumbani panakuwa hakuna tofauti na hotelini
 
Mkeo Ni mvivu wanangapi tuna kazi na chakula cha usiku lazima tupike ..nikutokujua Tu wajibu wake

ukishajua wajibu Wako na ukau appreciate wala hutaona km ni utumwa kutoka kazin nakuanza kupika
Kwa mtazamo tofauti ...mimi kama baba nimetoka kazini nika amua kuingia jikoni kuipikia familia yangu chakula ...je? ni kosa?
 
Mtazamo wa kisasa ukoje? Na unadhani ni kwa nini wanaume hawafanyiwi kitchen party?

Inaomekana mara nyingi mwanamke anawahi kurudi.

ndoa nyingi zinakufa kwa ajili ya hii mada.Jiulize mnaoana kwa ajili gani kama kila mtu alikuwa kwake alikuwa anapika kwa nini sasa muanze mambo ya ajabu.

Kila nyumba ina maelewano yake.

Ninachosema ni kwamba kama wote mnafanya kazi na mnarudi jioni sidhani kama ni fair mama watoto aende akapike, anyooshe nguo zako, awafanyie watoto tuition wakati wewe upo kwenye kochi unapiga wine. Huo sio upendo.

Kuna wakati mwanaume unakuwa unahamu ya kula kitu kuanzia mchana na unaweza kumpigia mke wako simu kumweleza na yeye atatune muda wake ili aandae hicho chakula.

Mara nyingi hizi fikra na hulka huwa mtu anatoka nazo nyumbani kwao kabla ya ndoa. Lakini mwisho wa siku ni mke na mume ndiyo wanaamua cha kufanya.
 
mmmm Balaa mwenyezi mungu atunusuru mimi na wanawake wenzangu,ndoa zinatafrani zake jamani,lakini hata kama unafanya kazi weekend unaweza ukapika na hata siku za kawaida unaweza kumwambia dada akutayarishie wewe ukifika una
changanya kwanza sikuizi sio kama zamani unapika na mikaa Gas unaivisha mara moja,unaweza kubiwa mume kwa vitu vidogo kama hivi halafu unatafuta mchawi..

Wengine kapika house girl,katenga house girl na anatoa vyombo housegirl,kama amezidisha chumvi yy ndio anakuomba baba msamaha kwa kuzidisha chumvi alafu asante umwambie mkeo sio fair,mke anabaki kuwa sex partner tu
 
Wakati mwingine hua naona maisha ya zamani yalifaa sana. Baba akatafute mama atunze familia lakini kulingana na uhalisia wa maisha haya ya sasa lazima na mama achakalike ili mambo walau yaende.lakini katika yote kila mmoja asisahau wajibu wake baba familia inakutegemea we kichwa hata kama mama mkurugenzi.nawe mama tunza mume na watoto hata kama ni DC ukirudi nyumbani ni mama...jaman hata Mara mbili tatu kwa wiki kuandaa kitu kwa mume na watoto.kila MTU akitimiza wajibu vizuri maisha matamu sana.
 
Kwa mtazamo tofauti ...mimi kama baba nimetoka kazini nika amua kuingia jikoni kuipikia familia yangu chakula ...je? ni kosa?
sio kosa umerudi na mood nzuri pika tu..
hata dada kupika sio kosa, mkipokeza ivyo kistudio sio mbaya inapendeza

shida inakuja pale ambapo mpishi Ni dada Tu kila siku iendayo kwa mungu wenye nyumba wamesahau majukumu Yao .

dada Ni msaidizi tu kazi Ni zenu
 
Naomba nikuulize swali la kizushi....
Wewe hapo nyumbani kwako umeshawahi kupika?...Manake hizi ni zama zingine .......
Nikipata nafasi napika, tena familia inafurahi kula chakula kilichopikwa na baba hasa watoto wakijua leo baba yuko jikoni wanafurahi sana.
 
Haya mambo yapo complicated sana. Mnatoka wote asubuhi, mnarudi wote usiku (hasa kwa wakazi wa Dar) ni ngumu mke kuwa committed jikoni. Tuwe tu wakweli, kuna maeneo ambayo kweli watu wakitoka job inawezekana sana kupika.

Tusiwe too conservative jamani. Hata wewe once in a while ingia jikoni upike.
Vipi kuhusu wa kijijini? Mama anampikia shambani asubui anarudi jioni na bado anaandaa chakula cha usiku.
 
Hapo panahitajika busara na umakini wa hali ya juu, Diplomasia itumike hapo tofauti na hapo familia itaingia kwenye mgogoro mkubwa sana na kusababisha mpasuko ambao haujawahi kutokea hapa dunia!
 
Kwa mtazamo tofauti ...mimi kama baba nimetoka kazini nika amua kuingia jikoni kuipikia familia yangu chakula ...je? ni kosa?
Ni kosa kubwa sana kisheria kuingilia majukumu ya mke wake unaweza kuhukumiwa jela miaka 15.
 
"Tangu apate hii kazi aliyonayo sasa yapata miaka miwili sili chakula kilichopikwa kwa mikono yake angalau mara moja moja, kwa siku chache za mwanzoni alijitahidi lakini haikudumu kwa muda mrefu akaacha kabisa binti wa nyumbani akawa ndiyo muhusika kwa 100%
duh!! hata siku za sikukuu,hana likizo?...miaka miwili si mchezo...
Lakini je hakuna majukumu mengine anayomfanyia mara moja moja kama vile kumfulia,kuandaa maji ya kuoga,piga deki chumbani nk...?
Vitu vidogo vidogo kama hivi hunogesha na kudumisha ndoa ila u''beijing'' ndio kikwazo..
 
Back
Top Bottom