Siku hizi Lowassa anashika Mic mbilimbili hadi tatu

Siku hizi Lowassa anashika Mic mbilimbili hadi tatu

Kipindi nchi hii ilikuwa inajikita katika vitu vitatu ili iweze kuendelea; Ardhi, Watu na Siasa Safi kulikuwa na maana yake tena muhimu sana. Wakati tunapata uhuru, ardhi ilikuwepo kubwa tu ila watu walikuwa wachache na siasa safi haikuwa safi kwa sababu walikuwa wamridhi siasa za propaganda kutoka kwa wakoloni na vibaraka wao. Miaka 50 baada ya uhuru, ardhi yenye maliasili nyingi ipo, watu wapo tena wakiwa na utalaam wa kila aina ila bado hakuna Siasa Safi kwa hiyo tusitegemee maendeleo. Siasa zilizopo zinajikita katik unafiki, uchochezi na uongo wa hali ya juu. Watu wanajikita katika vitu vidogo ambavyo havina mchongo wowote katika maendeleo. Vitu kama Mgombea huyu ni mgonjwa, kakosea kasema Sadam Husein ni wa Libya, kasema CCM Hoyee, Anaweza kupanda ghorofa anaweza, haweiz kukimbia mchaka mchaka !!! Vina faida gani kwa mwananchi wa kawaida ? Kama Mgombea kakosea kusema Sadam Husein ni wa Libya ina madhara gani hiyo ? Akiiingia Ikulu si atakuwa na washauri; aidha, mnataka Rais mwenye nguvu za kukimbia kwani wamaenda kushindana na akina Husei Bolt ? Kwa Siasa chafu za kujenga chuki na utengano miongoni wa Watzania, maendeleo yakujaje ilhali watu wanajitahidi kukwamishana kwa kila hali ilimradi mwenzake aonekane hajafanya chochote ili kipindi kijacho asichaguliwe, hiyo ni kuwaadhibu wanachi wasio na hatia !!!

Duh,,, safi sana, good comment..
 
Kuna watu waliwahi kumtukana mzee warioba wakasema ameezeka anakaribia kufa wawaache wao (huyo msemaji) waijenge nchi. Huyu bwana alishakufa na kumsahau na alikufa ghafla sana tukamlilia, but he is gone. Rest in Peace Komba
 
Wakenya walichagua raisi akiwa kwa wheel chair.. Nitampigia kura huyo huyo mgonjwa.
 

Attachments

  • 1442825194613.jpg
    1442825194613.jpg
    63.1 KB · Views: 189
Hata kama mtu aumpendi sio vizuri kujikita kwenye ugonjwa kwani sisi sote hafya tunazojidai nazo tumeazima kwa muda naweza kuondoka Mimi au yeyote anayeshabikia ugonjwa tujikite kwenye hoja za msingi Tanzania inayo matatizo mengi ambayo tunaweza kuchangia bira kuingiza swala la ugonjwa mbona jk alikuwa anaanguka majukwaani hila aikuwa hoja ya kitaifa kama hii ya EL
Timu ya kusimamia kampeni za chama tawala inafahamika
hivyo tusishangae kusikia matusi,kama kiongozi mzima alitoa matusi
siku ya uzinduzi ,ajabu ni ipi akina kibajaji kuendeleza matusi.
Dawa ni kuandaa vichinjio ndo wataelewa nguvu ya malofa.
 
amongeza na dakika za kuongea kutoka 3 hadi 5., nice improovement au vipiiiiiiiiiiii
Yuko makini mzee wa kampeni anajua pa kuanzia na kumalizia muda unapo yoyoma ndipo anapiga kazi ambapo asubuhi wanaamka wanamkumbuka hadi katika sanduku la kura
 
Hata kama mtu aumpendi sio vizuri kujikita kwenye ugonjwa kwani sisi sote hafya tunazojidai nazo tumeazima kwa muda naweza kuondoka Mimi au yeyote anayeshabikia ugonjwa tujikite kwenye hoja za msingi Tanzania inayo matatizo mengi ambayo tunaweza kuchangia bira kuingiza swala la ugonjwa mbona jk alikuwa anaanguka majukwaani hila aikuwa hoja ya kitaifa kama hii ya EL

Afya ya mgombea ni muhimu sana hususan Urais.

Kazi za kawaida tu unaambiwa ukapime afya kwanza itakuwa hii ya kutumwa na watu million 45?

Ni lazima tuhoji, hatutaki kuweka mgonjwa pale Ikulu kwa makusudi kabisa.
 
Mice???
Dada faizaFox come this way plz!

faizafox = FaizaFoxy.
Ndugu zangu wakristo wanasema "Itoe boriti katika jicho lako wewe mwenyewe ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako"
 
Ndio elimu yetu ilipofikia yaani kama mgombea uraisi anasema Saddam alikuwa raisi wa Kuwait !!unategemea nini kwa watu baki ??
Sijui anajisikiaje mtoto wa kiume kujiita jina la kike na kutumia picha ya kike
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom