Ilikuwa ni siku ya alhamisi, mpenzi wangu alinipia simu kwamba anaitaji tuonane. Kwa kweli alinishtua sana, nilijua labda amepatwa na tatizo. Nilipofika kwake aliniambia kwamba anaitaji kutoka na mimi kwenye sikukuu ya pasaka. Kwa7bu ya upendo wangu kwake nilimkubalia ombi lake. Ilipofika siku ya jumapili asubuhi alinipigia simu kwamba anajisikia vibaya (anaumwa), kwahiyo hawezi kwenda sehemu yoyote siku hiyo. Kwa kweli nilimuhurumia sana, nakumuahidi nitaenda kumuona siku hiyo. Japo kuwa alinikatalia kwenda kumuona, sikukata tamaa jioni nilienda kumuona, cha kushangaza sikumkuta na mlango ulikuwa umefungwa. Nikaanza kuwauliza majirani zake, walinijibu kwamba aliwahaga anakuja kwangu, nalipojaribu kupigia simu hakupatikana. Nikaamua kurudi nyumbani, wakat nipo njiani nikapigiwa simu na rafiki yangu kwamba amemuona mpenzi wangu akiwa na msichana mwingine wakiwa kwenye Bar fulani. Nakachukua bodaboda hadi eneo husika na nilichokishuhudia ni Mungu mwenyewe anajua. Jamani nimevurugwa sana. Nilikuwa naitaji marafiki wa kunifariji. Sichagui Dini, kabila wala jinsia. Wote kwangu ni marafiki tu.