Siku ambayo sitaisahau

Siku ambayo sitaisahau

Kila jambo hutokea kwa makusudi fulani. Mshukuru sana Mungu kwani kakuonesha kwamba huyo sio mume mwema.
Lingine, faraja ya kweli yatoka kwa Mungu tu!Usitegemee marafiki wakupe faraja aisee watakuumiza tu!
 
Ilikuwa ni siku ya Alhamisi, mpenzi wangu alinipia simu kwamba anahitaji tuonane. Kwa kweli alinishtua sana, nilijua labda amepatwa na tatizo. Nilipofika kwake aliniambia kwamba anahitaji kutoka na mimi kwenye sikukuu ya pasaka. Kwasababu ya upendo wangu kwake nilimkubalia ombi lake.

Ilipofika siku ya Jumapili asubuhi alinipigia simu kwamba anajisikia vibaya (anaumwa), kwahiyo hawezi kwenda sehemu yoyote siku hiyo. Kwa kweli nilimuhurumia sana, nakumuahidi nitaenda kumuona siku hiyo. Japo kuwa alinikatalia kwenda kumuona, sikukata tamaa jioni nilienda kumuona, cha kushangaza sikumkuta na mlango ulikuwa umefungwa.

Nikaanza kuwauliza majirani zake, walinijibu kwamba aliwaaga anakuja kwangu, nilipojaribu kupigia simu hakupatikana. Nikaamua kurudi nyumbani, wakati nipo njiani nikapigiwa simu na rafiki yangu kwamba amemuona mpenzi wangu akiwa na msichana mwingine wakiwa kwenye Bar fulani.

Nikachukua bodaboda hadi eneo husika na nilichokishuhudia ni Mungu mwenyewe anajua. Jamani nimevurugwa sana. Nilikuwa nahitaji marafiki wa kunifariji. Sichagui Dini, kabila wala jinsia. Wote kwangu ni marafiki tu.
......Changamkieni Fursa hii
 
pole sana jina lako linanikumbushaBEA BIANCA wa PANGAKO SA YO anapenda asipopendwa
 
Back
Top Bottom