Siku ambayo Kikwete anaondoka madarakani nitaiadhimisha kila mwaka

Wote ni wale wale.Huyo JK ndie alieweka msingi wa baadhi ya mambo tunayoyaona leo hii.

Ni katika utawala wa JK tumeona watu wakitekwa kama kina Dr.Ulimboka.

Ni katika utawala wa JK ndio imetungwa sheria ya mitandao.

Huyu JPM ana-take advantage ya mazingira yaliyoachwa na JK.
Mbona hatukuwahi kumsikia Kamanda Dr. Shoo akitoa waraka kuhusu Mambo hayo kipindi Hicho?
 
Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.

Nilishasema haya siku za nyuma na watanzania wakakasirika na wengine kujipiga vidole kwa hasira eti namuonea Kikwete.
 
Nilishafanya sana hasa nikikumbuka kutunyima Katiba Mpya ambayo leo ndio inafanya watu wanateseka.
Wakati nasikia mnamshangilia kama shujaa siku hizi! Mmemiss masafari ya nje ya kibunge na posho. Madeni ya uchaguzi hayalipiki. Siasa za kuchafuana na kupozana kwishney .....
 
Yaani nyie....
Unashangaa nini ? Kikwete ndiye ameleta haya yote yanayofanywa hivi sasa , Kikwete ndiye aliyepora ushindi wa Maalim Seif , Kikwete ndiye alimpeleka Kapilimba Tume ya uchaguzi , kitu gani hukijui ?
 
Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Nahisi kuna watu wameyasahau haya,na kubaki wanapondea kila mema yanayofanyika sasa hivi...
 
Ha ha ha Salary Slip bwana haka kakaburi kachungu
 
Back
Top Bottom