Siku ambayo Kikwete anaondoka madarakani nitaiadhimisha kila mwaka

Ndio asili ya kuwaita yule mnyama wa porini mwenye ndevu. Hamkawii kusahau. Mmoja akielekea huku na wao tiiiiim. Leo mnamkumbuka JKsio nyie mliokuwa mkimtusi hasa wewe mwenye hii thread.

Mkumbuke sana tuu. Sasa ni MR PRESIDENT JPM HADI 2025
 
Elewa kwamba utawala wa JPM unapanda mbegu za chuki sana,trust me,2025 JPM akimaliza utawala wake,kuna baadhi ya watu wake wataishi kama wakimbizi hapa Tanzania!!

Majaliwa Kassim hapendi kusikia jina la Bashite kwenye hii serikali,lakini ndo hivyo,Bashite ni mtoto wa Baba! Bashite hana vyeti,Bashite ndo master mind wa ujinga mwingi unaofanyika hapa Tanzania!

Bashite anafokea watu,Bashite anafanya lolote atakalo,Bashite anajiona yeye ni Mungu mtu! Hadi anasema yeye ni mtumishi wa pili Tanzania kwa uchapaji kazi baada ya Baba yake!!

Bashite huyu anatukana watumishi hovyo hovyo hajui kwamba anaweza achia hiyo ofisi na kua muuza asali kama marehemu Ditopile,au mkulima kama mzee Mashishanga
Majaliwa atakapompa uteuzi huyo bashite utaaibika kama mwenzio anavyoaibika Leo na Uzi wake huu.
 
Unashangaa nini ? Kikwete ndiye ameleta haya yote yanayofanywa hivi sasa , Kikwete ndiye aliyepora ushindi wa Maalim Seif , Kikwete ndiye alimpeleka Kapilimba Tume ya uchaguzi , kitu gani hukijui ?
Sherehe Mzee baba,au ndio ile mlomshangilia JK bungeni?
 
Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Ona ujinga wako ,angalia na unachongea kwa sasa
 
Kila siku bora jana.
 
Back
Top Bottom