Siku ambayo Kikwete anaondoka madarakani nitaiadhimisha kila mwaka

Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Kamanda sherehe lini?
 
kuondoka kwa kikwete ni sawa na kupona ugonjwa wa cancer. kikwete ni cancer iliyotafuna nchi kwa kipindi cha miaka kumi. asante mungu huu ugonjwa unaondoka kabla haujau wa TZ wote. uwarehemu waliotangulia kwa kuuwawa na ugonjwa huu. tulijitakia sisi wenyewe. wengine walisema ni chaguo lako mwenyezi, kumbe ni ugonjwa kutoka kuzimu.
Nani tena anafukua makaburi
 
Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Ona ulivyomnafiki,huyu huyu ambaye ulikuwa unamnanga siku hizi ndio unamsifia,tumeshawajua nyie hakuna mzuri yoyote akiwa CCM ila akija kwenu anageuka malaika.
 
Upinzani upo kwenye denial ...wengine tulijua nini kinakuja baada ya zile gia za 2015 ...tumefanya kila tunaloweza kuamsha watu kutoka kwenye usingizi ili tusonge mbele lakini ujuaji na kiburi umeifikisha upinzani hapa. Mbaya zaidi bado wengine hawajagutuka! Acheni kuibeza CCM na kuacha kuionya chadema. Chadema imepigwa ganzi amkeni!!!!
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom