Siku 7 Za rais JP zimepuuzwa,Majipu Bado yapo na Yanaendelea na wizi

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Sasa nimeamini Urais sio mbwembwe wala kelele.Ni mbinu na busara na kipaji mungu ana mtunuku mtu.
Rais Magufuli toka kaingia ikulu ndio anamaliza mwezi na point sasa,Aliingia kwa mkwara mzito kweli,Akatoa siku 7 kwa waliokwepa kodi wote kulipa kabla mkono wa serekali kuwatia mbaroni wahusika wote.
Leo Unakaribia mwezi toka onyo la siku 7 Litolewe na hamna aliyekamatwa,Zaidi watu wameonyesha dharau kwa rais kulamba kontena na magari bila kulipa kodi katika kipindi ambacho rais aliapa kudili na wakwepa kodi wakubwa.
Hii ina maanisha hamna mkwepa kodi aliye kizuizini mpaka sasa.Maana wangekuwa kizuizini tusingesikia tena haya yanayojitokeza,Upo Umuhimu wa Rais kutafuta jipu na kulikamua litoke kiini chake,Bila hivyo majipu yataendelea kuota na kuwa sugu,Vilivyo kamuliwa ni vijipu uchungu tu majipu bado yapo tena makubwa kweli kweli
 
Nafikiri kuna watu wanashikiliwa na kuna watu pia wamelipa kodi iliyokwepwa na wafanya biashara
 
Bora Lowassa kuliko Rais Magufuli!

Huyu Rais Magufuli kwa sasa anatimiza Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA!

Kama Lowassa angekuwa Rais wa Tanzania, kwa sasa mafisadi na majizi yote yangekuwa gerezani!

Kama Lowassa angekuwa Rais wa Tanzania, tusingesikia tena wezi na mafisadi. Wizi na ufisadi ungekuwa ni historia!

Watanzania ni hawaambiliki! Badala ya kumuweka Lowassa pale Ikulu wakaamua kutuwekea Rais Magufuli.

Mabadiliko yalikuwa ni Lowassa na Lowassa alikuwa Mabadiliko! My left foot.
 
Wakuu si nasikia mpaka mida hii upelelezi wa makontena ya awali yalioibiwa unaendelea ingali tena kuna makontena mengine yameibuliwa swali la msingi la kuhoji ni kwamba ile riport ambayo waziri mkuu aliyopewa ya upotevu wa makontena elfu mbili na ushee ilikuwa ni ndogo sana ukilinganisha na ya sasa na je riport ya awali aliminywa kupewa majina mengine kwa sababu gani...???
Na aliyempatia hiyo riport ya awali ni kwa nn asimpatie majina yote ya wakwepa kodi ili ashugulike nayo kwa pamoja au huu ni mwendelezo wa hapa kazi tu kwa maneno...????
 
Hv bado mnaimani na hii serikali ya maigizo? Mlipoambiwa ccm ni ile ile mlidhani wanamaanisha nn? Huwez kuwakamata watendaji wa chini ukawaacha wakubwa wakipeta utegemee matatizo yaishe. Unakata matawi ili mti ukauke? Mnashangaza.
Magufuli hana uwezo wa kuwakamata wahujum uchumi wote maana wengi ni vigogo wa chama chake na viongozi wa serikali ya awamu ya nne.
 
Mleta mada weka hadharani pale juu kwenye thread yako ushahidi wa makontena hayo kupitishwa baada ya nginjanginja ya Majaliwa.

otherwise kajipange na usheherekee ushindi wa Magifuli.
 
kila siku makontena yamekamatwa, hakuna hatua yoyote wanayochukuliwa wanaohusika
 
Sasa nimeamini Urais sio mbwembwe wala kelele.Ni mbinu na busara na kipaji mungu ana mtunuku mtu.
Rais Magufuli toka kaingia ikulu ndio anamaliza mwezi na point sasa,Aliingia kwa mkwara mzito kweli,Akatoa siku 7 kwa waliokwepa kodi wote kulipa kabla mkono wa serekali kuwatia mbaroni wahusika wote.
Leo Unakaribia mwezi toka onyo la siku 7 Litolewe na hamna aliyekamatwa,Zaidi watu wameonyesha dharau kwa rais kulamba kontena na magari bila kulipa kodi katika kipindi ambacho rais aliapa kudili na wakwepa kodi wakubwa.
Hii ina maanisha hamna mkwepa kodi aliye kizuizini mpaka sasa.Maana wangekuwa kizuizini tusingesikia tena haya yanayojitokeza,Upo Umuhimu wa Rais kutafuta jipu na kulikamua litoke kiini chake,Bila hivyo majipu yataendelea kuota na kuwa sugu,Vilivyo kamuliwa ni vijipu uchungu tu majipu bado yapo tena makubwa kweli kweli

Siku ya kufanya usafi ilyotangazwa na Mh. Magufuli, Kikwete alisema kuwa wakwepa kulipa kodi hawataisha na wataendelea...manake nini jamani? Ndiyo hayo sasa.
 
Siku ya kufanya usafi ilyotangazwa na Mh. Magufuli, Kikwete alisema kuwa wakwepa kulipa kodi hawataisha na wataendelea...manake nini jamani? Ndiyo hayo sasa.
Hili swala la ukwepaji kodi limekuwa kama biashara ya unga kule colombia kukata huu mzizi lazima wanaCcm walie tena wa ngazi ya juu kabisa
 
Bora Lowassa kuliko Rais Magufuli!

Huyu Rais Magufuli kwa sasa anatimiza Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA!

Kama Lowassa angekuwa Rais wa Tanzania, kwa sasa mafisadi na majizi yote yangekuwa gerezani!

Kama Lowassa angekuwa Rais wa Tanzania, tusingesikia tena wezi na mafisadi. Wizi na ufisadi ungekuwa ni historia!

Watanzania ni hawaambiliki! Badala ya kumuweka Lowassa pale Ikulu wakaamua kutuwekea Rais Magufuli.

Mabadiliko yalikuwa ni Lowassa na Lowassa alikuwa Mabadiliko! My left foot.
inabidi upewe cheo cha uongo na upotoshaji wa ukweli.
 
Mimi naomba msaada humu mtu mmoja anisaidie vipi mfanyabiashara anaweza akaiba contena bandarini au ICD.jamani tuwe wakweli .tatizo hili ni sehemu tatu kuu .1) aitha ni TPA au watu wa ICD's ,2) ni TRA na 3) ni mawakala wa kutoa mizigo bandarini. Kunawafanyabiashara wapo kwenye biashara kwa zaidu ya miaka 30 ,llakini hata geti namba 5 halijui wala ICD hazijui ila wanatozwa mamilioni ya hela na hawa mawakala.likibumburuka hawa mawakala wanakimbia
 
Back
Top Bottom