Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari - 2022: Rais Samia awahimiza wanahabari kuzingatia mila na desturi za Kiafrika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Samia.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) ambayo inafanyika leo Mei 3, 2022 Jijini Arusha.

Kabla ya Rais Samia kuanza kuzungumza, mijadala imeendelea ukumbini:

DKT. RIOBA: MAMLAKA ZINAPATA UGUMU KUZUIA NGUVU YA DIGITALI
Kupitia maendeleo ya teknolojia kuna vipaji vingi vimeonekana kupitia vyombo vya habari huku Serikali na taasisi zake zikipata wakati mgumu kudhibiti kila kitu kinachotoka mitandaoni.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba ambaye ameongeza kuwa licha ya nguvu ya mamlaka nyingi lakini ulimwengu wa digitali hasa mitandao ya kijamii umeleta mambo mengi na imekuwa ngumu kudhibiti kila kitu.

“Kuna watu wengi mmoja mmoja wametumia mitandao kujiendeleza na wamepata faida. Nilikuwa nazungumza na ndugu yangu Max ambaye naye aliniambia jinsi ambavyo kumekuwa na mabadiliko makubwa ya digitali katika Jamii Forums,” Rioba.

DKT. RIOBA: UHURU WA DIGITALI UMELETA MADHARA MENGI
Pamoja na maendeleo ya uhuru wa kujielezea kupitia digitali upande mwingine kuna madhara ambayo yameongezeka kutokana na maendeleo ya teknolojia.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba anasema:

Tamaduni nyingi zimeuliwa, umoja wa taifa upo hatarini, usalama wa taifa kuwa hatarini kutokana na wale wanaotaka kupinga mamlaka, makundi ya kigaidi yanatumia mitandao kupanga mambo ya na kufundisha wengine ugaidi kwa njia ya kidigitali na kuongezeka kwa habari za uwongo.”

SALOME KITOMARI (MWENYEKITI, MISA-Tanzania)
Licha ya mafanikio katika Sekta ya Habari, bado kuna changamoto kadhaa zinazohitaji kutatuliwa

Miongoni mwao ni ushindani usio sawa, hali duni ya wanahabari na kuongezeka kutumia watu maarufu kama watangazaji

CHURCHILL OTIENO (EAES):
Bado tuna waandishi ambao wanapata msongo wa mawazo kutokana na kazi wanazofanya

Tuna Wanahabari walio chini ya ulinzi Nchini Rwanda, Ethiopia, Eritrea na DR Congo

Vilevile, vitisho dhidi ya wanahabari vinazidi kuchukua sura mpya

RAIS SAMIA AWASILI
Rais Samia ameshawasili eneo la tukio katika Ukumbi wa Hoteli ya Gran Melia Hotel Jijini Arusha na ameanza kwa kutembelea mabanda mbalimbali.

Shughuli inaanza rasmi, baadhi ya viongozi na wageni waalikwa wanazungumza

Dkt. Jim Yonazi (Katibu Mkuu Wizara ya Habari)
Maadhimisho ya World Press Freedom Day 2022 duniani yanafanyika Nchini Uruguay

Kwa Bara la Afrika, na kwa mara ya kwanza, Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari inaadhimishwa Jijini Arusha hapa Nchini kwetu

Wynne Musabayana (AU)
Umoja wa Afrika unachukua fursa hii kupongeza Vyombo vya Habari kwa kuitangaza Afrika hata katika wakati mgumu wa Janga la COVID-19

Vyombo vya Habari vina nafasi muhimu na ya kipekee katika kuhakikisha Waafrika wanapata taarifa za kimaendeleo

Tunawashukuru wanahabari kwa kazi ambayo wanaendelea kufanya, hasa katika wakati mgumu sana wa janga la Covid.

Tutaendelea kuwa marafiki wao na kurahisisha kazi zao.

Tulibainisha kwa dhati sana kwamba ni muhimu kwetu kama Waafrika kuchukua jukumu la kueleza simulizi zetu.

Zlatan Millisic: Mratibu Mkazi wa Shughuli za UN
Mwaka huu kaulimbiu ni "Uandishi wa Habari na Changamoto na Kidijiti"

Kaulimbiu hii inakutumbisha namna mbalimbali ambazo uandishi wa upo hatarini kupitia dijitali

Anders Sjöberg (Balozi wa Sweden-TZ)
Wanahabari mara nyingi wanaweza kujikuta katika mazingira hatari yanayoweza kugharimu maisha yao

Tunatoa heshima kwa Wanahabari ambao wamelipa gharama kubwa kwasababu ya kufanya kazi zao

Deodatus Balile (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania -TEF)
Kuna nchi nyingi waandishi wanawindwa kwa kutumia teknolojia ya habari, kwa mujibu wa takwimu za UNESCO, waandishi 55 wameuawa mwaka 2021, mwaka 20 2020 waliuawa waandishi 65

Tunaomba Serikali zetu Afrika kwa jumla zilinde maisha ya waandishi wa habari kwani inaumiza waandishi kupoteza maisha na waovu asilimia 80 kutochukuliwa hatua

Waziri wa Habari, Nape Nnauye ametangaza ataunda kamati ya pamoja kati ya wadau wa habari na Serikali kupitia sheria zinazolalamikiwa, ameahidi kufikia Settemba 2022 sheria zote zinazolalamikiwa zitakuwa zimepatia utatuzi

Taarifa za Waandishi wasio na mipaka imeonesha Tanzania ilikuwa na anguko la Vyombo vya Habari ila sasa hali inatia matumaini. Tangu mwaka 2016 Tanzania ilikuwa nafasi ya 71 kati ya nchi 180, anguko liliendelea hadi (Rais Samia) ulipolidhibiti
-
Mwaka 2017 ilikuwa ya 83, mwaka 2018 ikawa ya 93 mwaka 2019 ikawa ya 118, mwaka 2020 ikawa ya 124. Kwa hizi hatua ulizochukua nakuhakikishia haitashuka tena

Nape Nnauye, Waziri wa Habari
Wanahabari wa Tanzania na kwingine Afrika wanakutana hapa Arusha nchini kwetu wakati ambao tasnia ya habari inapaswa kusimama imara kuhakikisha rasilimali za Afrika zinawanufaisha Waafrika

Mapitio ya Sheria ya Huduma za Habari yamelenga kuboresha zaidi Tasnia ya Habari

Tunapitia Sheria hii inayolenga kuweka Sekta ya Habari kuwa inayojitegemea na kuheshimika na isaidie kuboresha maslahi ya Wanahabari

Tunatumia busara ili mambo yaende. Hivyo ni busara kujiepusha na kujaribu kuchokonoa busara tunayotumia. Msinitie majaribuni

Wizara ninayoiongoza itaendelea kuimarisha ushirikiano na Vyombo Vya Habari na Wadau wa Habari Nchini na Nje ya Nchi

Hiyo ni kuifanya Sekta hii kukua na kuwa na mchango mkubwa kwa Taifa

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Nipo hapa nanyi kwa heshima ya pekee, niwakaribishe wageni wote, nimeambiwa mna ratiba ya kuzunguka Arusha, niwaombe sana zungukeni mfanye utalii, huwezi kujua unaweza kukuta warembo wazuri wa Kitanzania, zungukeni muione Tanzania

Nimefurahi kuona uwakilishi wa Wanahabari kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika na hii inaonesha kuwa Sekta ya Habari kwa Bara la Afrika inajiunga na maendeleo makubwa yanaonekana

Baada ya Uhuru tulikuwa na magazeti 10 sasa yapo 285, tulikuwa na kituo kimoja cha Redio sasa vipo zaidi ya 200, hatukuwa na kituo cha TV sasa tuna vituo 55, kuna kituo kinaitwa Suluhu Televisheni lakini siyo cha kwangu ni cha familia

Kuongezeka kwa vyombo vya habari kumetokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano lakini pia utashi wa kisiasa ndiyo unaoruhusu uanzishwaji wa vyombo hivyo, ambavyo pia vinaongeza uhuru wa kujieleza

Nimeelekeza sheria mbalimbali za vyombo vya habari zifanyiwe marekebisho, na mchakato wa marekebisho hayo ufanywe kwa majadiliano na sio kwa sisi tunataka nini

Hatuwezi kukataa kuwa mitandao ya kijamii imekuwa inatupa fursa ya kujieleza jinsi tunavyoweza. Tutumie mitandao kujenga jamii, kukubaliana au kutokubaliana na mambo yanayotekelezwa na serikali, kupeana pole, kutumia fursa

Tukiruhusu haya (picha chafu) tutawaambiaje watoto wetu, katuni zilizopo mitandaoni, mwanaume kwa mwanaume wanabusiana, mwanamke kwa mwanamke, hatuzikontrol

Waziri na Wizara yako hamchuji, hatufikiri mpaka Rais aseme?

Serikali inaunda sheria lakini wa kwenda kuwaelimisha wananchi ni nyinyi waandishi wa habari. Utakuta mtu anapost picha za utupu mitandaoni, Wanafanya hivyo kwa kutokujua na wengine wameambiwa watalipwa

Juzi tumeonesha Msitu katika Royal Tour, Watu roho zipo juu, wanatamani kuja kuona msitu ambayo sisi hatuithamini

Hamuandiki mnaenda kujivua nguo. Mnasema huku hakuna Demokrasi, kuna Udikteta, mara mama kafanya hivi. Jivunieni kilicho chenu

Kumekuwa na jitihada kuunganisha umoja wa waandishi wa Afrika,

Nadhani huo mchakato uendelee ili muweze kulitetea bara hili linaloonekana ni masikini wa kila kitu hadi akili kitu ambacho sio kweli

Nimeona mitandaoni wiki moja baada ya kuonana na Makamu wa Rais wa Marekani akakutwa na Covid, Mtanzania akachora katuni mshale kuonesha mimi ndiye nimempa Covid, alipimwa nilioondoka, alivyoenda ziara kurudi ndiyo akakutwa na Covid

Mnaandika mimi nimempa Kamala COVID19, mnajiandikia tu. Mie nina Ngozi ngumu, kama mnaandika andikeni tu!

Nimelipokea ombi la makaratasi (karatasi za kuchapia machapisho mbalimbali), lakini si tunaenda kwenye digitali! Yawezekana kodi zimewekwa ili nguvu ihamie kwenye digitali lakini Waziri amelisikia ataona jinsi ya kulifanyia kazi

Viongozi wenzangu wa Afrika tushirikiane na waandishi wa habari ili kuweza kuleta chagizo la maendeleo ya kiuchumi. Maendeleo ya nchi yetu hakuna ambaye anatakiwa kubaki nyuma na Waandishi wa habari mpo kwa nini niwaache nyuma. Tunagombania kitu gani?

Waandishi wa Habari wa Tanzania tutafute muda tukae tuzungumze kama wanahabari na Serikali yenu ili tuzungumze kwa mapana na kuelewana zaidi
 
Peter Greenburg anamhitaji huku Marekani. Kuna scene inapaswa kuboreshwa kwenye filamu ya Royal tour
 
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) ambayo inafanyika leo Mei 3, 2022 Jijini Arusha.

Kabla ya Rais Samia kuanza kuzungumza, mijadala imeendelea ukumbini:

DKT. RIOBA: MAMLAKA ZINAPATA UGUMU KUZUIA NGUVU YA DIGITALI
Kupitia maendeleo ya teknolojia kuna vipaji vingi vimeonekana kupitia vyombo vya habari huku Serikali na taasisi zake zikipata wakati mgumu kudhibiti kila kitu kinachotoka mitandaoni.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba ambaye ameongeza kuwa licha ya nguvu ya mamlaka nyingi lakini ulimwengu wa digitali hasa mitandao ya kijamii umeleta mambo mengi na imekuwa ngumu kudhibiti kila kitu.

“Kuna watu wengi mmoja mmoja wametumia mitandao kujiendeleza na wamepata faida. Nilikuwa nazungumza na ndugu yangu Max ambaye naye aliniambia jinsi ambavyo kumekuwa na mabadiliko makubwa ya digitali katika Jamii Forums,” Rioba.

DKT. RIOBA: UHURU WA DIGITALI UMELETA MADHARA MENGI
Pamoja na maendeleo ya uhuru wa kujielezea kupitia digitali upande mwingine kuna madhara ambayo yameongezeka kutokana na maendeleo ya teknolojia.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba anasema:

Tamaduni nyingi zimeuliwa, umoja wa taifa upo hatarini, usalama wa taifa kuwa hatarini kutokana na wale wanaotaka kupinga mamlaka, makundi ya kigaidi yanatumia mitandao kupanga mambo ya na kufundisha wengine ugaidi kwa njia ya kidigitali na kuongezeka kwa habari za uwongo.”

SALOME KITOMARI (MWENYEKITI, MISA-Tanzania)
Licha ya mafanikio katika Sekta ya Habari, bado kuna changamoto kadhaa zinazohitaji kutatuliwa

Miongoni mwao ni ushindani usio sawa, hali duni ya wanahabari na kuongezeka kutumia watu maarufu kama watangazaji

CHURCHILL OTIENO (EAES):
Bado tuna waandishi ambao wanapata msongo wa mawazo kutokana na kazi wanazofanya

Tuna Wanahabari walio chini ya ulinzi Nchini Rwanda, Ethiopia, Eritrea na DR Congo

Vilevile, vitisho dhidi ya wanahabari vinazidi kuchukua sura mpya

Rais Samia ameshawasili eneo la tukio, amezunguka kuangalia katika mabanda, shughuli inaanza rasmi:
Ametoka saa ngapi Dar?
 
BAKWATA 0 - WANDISHI WA HABARI 1

Mungu anawaona BAKWATA & CCM kwa kusogeza sikukuu ya eid mbele (kutoka jumatatu hadi jumanne) kisa ugeni rasmi wa Samia katika balaza la eid wakati Samia anaratiba nyingine na waandishi wa habari
 
BAKWATA 0 - WANDISHI WA HABARI 1

Mungu anawaona BAKWATA & CCM kwa kusogeza sikuku ya eid mbele kisa ugeni rasmi wa Samia wakati Samia anaratiba nyingine na waandishi wa habari
Kwani wamesogeza mbele eid na wakati eid ni leo. Na unajua dini ya kiislam mwanamke ahudhurii msikitini wala kuongea mbele ya masheikh
 
Back
Top Bottom