Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,196
- 162,724
Habari wadau,
Kwa mtazamo wangu, siku 21 za maombolezo ya kitaifa wanapofariki viongozi(maraisi) ni nyingi mno hivyo napendekeza zipunguzwe kufikia siku 14 au hata chini ya hapo.
Wanadamu, kwa asili, tumeumbwa kusahau na hii si kwa bahati mbaya, bali ni ili kumuwezesha mwanadamu aendelee na maisha baada ya kupitia hali fulani katika maisha ambayo inaweza kuwa sio nzuri(kufiwa, n.k).
Kwa msingi huo, viongozi wa kitaifa wanapofariki, watu hupata mshituko siku chache za mwanzo na baada ya hapo, huanza kuzoea hali hio na kinachofuata watu huanza kuhesabu siku msiba uishe.
Hata nyimbo za maombolezo hugusa watu siku chache tu za mwanzo ila baada ya muda, watu huzizoe na kuzichukulia kama nyimbo nyingine tu za kuwaburudisha.
Mwili wa marehemu unapokuwa bado haujazikwa, walau watu kwa kiasi fulani wanakuwa Katika hali ya msiba, ila marehemu akizikwa tu, basi kinachofuta ni watu kukamilisha formalities na katika kipindi hicho, ndio watu huongeza hata kasi ya kuhesbu siku.
Kwa mfano, utasikia mtu anauliza hivi maombelezo yataisha lini?Wengine utawasikia wakisema wamzike tu jamani, n.k.
Ukweli ni kwamba, katika hali ya kawaida, msiba kama msiba hugusa zaidi wanafamilia, ndugu,jamaa na marafiki wa karibu tena hata wao(baadhi) huanza kusahau na kutamani msiba ufike mwisho na wao wapumzike /waendelee na maisha mengine.
Hivyo, ili kuwaondolea majonzi wanafamilia na ndugu wengine wa marehemu kwa kupiga nyimbo za maombolezo kwa siku 21, nashauri siku hizo zipunguzwe na ziwe siku 14 tu kwanini sidhani kama kuna sense ya msiba wiki mbili au tatu baada ya marehemu kuzikwa zaidi tu ya formalities za kitaifa za kukamilisha msiba na msiba si formalities bali ni hisia za watu kwa mpendwa wao.
NB:Sheria karibu zote mara nyingi hushirikisha wadau kabla ya kutungwa, ila sheria ya misiba ya kitaifa, hasa kipengele cha maombolezo ya siku 21, sidhani kama iliwahi pata maoni ya wadau(wafiwa) kwani sidhani kama walikuwepo wakati inatungwa.
Naomba nimalizie kwa kusema hivi:
Sometimes in life, it worth to agree when the rest or majority disgrees, and to disagree when the rest or majority agrees (time will decide who is right and who is wrong).
Similarly, sometimes it worth to be sceptical when the rest or majority are optimistic, and to be optimistic when the rest or majority are sceptical.