Sikio la kufa halisikii dawa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
572
2,550
Pamoja na kupanda kwa gharama za maisha, bado tunashuhudia ongezeko kubwa la kodi kila siku. Maneno ya viongozi yamekuwa yaleyale kila siku, hakuna matumani, jahazi linataka kuzama.

Sisi wananchi wa kawaida ni kama watu tuliotoswa baharini ingali hatujui kuogelea. Tumepokwa hata maboya tunayo tegemea kuwa yatatusaidia kwenye kupiga mbizi. Tupo kama mgonjwa aliye ICU, tumenyimwa hata hewa ambayo ndiyo tumaini letu la mwisho.

Tufanye nini sasa, tumekuwa kama wakimbizi kwenye nchi yetu wenyewe. Serikali imeamua kuweka pamba masikioni, haitaki kabisa kusikia tunavyolia.

Hili ni sikio la kufa, halisikii dawa.
 
Ukiona hivi basi utambue fika tunakaribia kwenye kilele cha mlima! Baada ya muda mfupi tutafika, na kuanza kuteremka tena bondeni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom