I call it "it is a promotion on Freemason" hakuongea cha maana. Wanawafanya vijana wengi kutojua ukweli halisi na kutamani kuingia huko wakidhani kuna utajiri, stupid kabisa.
Watanzania tutadanganywa sana, freemasons ipo miaka mingi nenda rudi, kwa nini hivi sasa ndiyo inaonekana inapamba moto sana??
Kumbuka adui huyo huyo ndio anaipromoti, akijifanya kuipinga au kuelewesha jamii. Sasa hivi kila kitu ni free masons, mtu akifanikiwa ni free mason, nyanja yeyote ukiwa umeonyesha njia watu wanasema ni free mason. Wamekwenda mbali zaidi na hata kuwaingiza watumishi wa Mungu wanaoheshimika kuwa ni free mason, nani atabaki salama?? Je free mason imeanza leo, kwani asifanikishe watu miaka yote? "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" Ni andiko ambalo haliwezi kutanguka.
Kumbuka jambo moja muhimu, kazi ya shetani KUUA, KUHARIBU NA KUIBA na mwenye masikio na asikie.
Mungu ni mwema na rehema zake zinadumu milele, msidanganyike.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.