Unajua kwanini 90% ya wana-hiphop huamini kuwa 2pac ni king wao?

Akilihuru

JF-Expert Member
May 20, 2022
1,444
2,832
Wakuu inakuaje, nina amini kila mtu yuko vizuri kiafya au sio wakuu.

Sasa leo nawaletea mada muhimu, na yenye kueleweka vizuri kwa kila mtu atakaesoma thread hii. Mada hii inamhusu rapper maarufu wa muda wote 2pac Amaru Shakur, ambae pamoja na kwamba ameshafariki miaka 26 iliyopita, Lakini mziki wake au ujumbe wake katika mziki unaendelea kuishi.

2pac au makaveli, ambapo wamarekani wenyewe wamempa sifa kwa kumpachika jina la 'The GOAT,' kirefu chake 'The Great Of All Time' (msaani bora wa muda wote) ni msaani aliefanya mambo makubwa katika mziki huo, hadi kupelekea wasanii wengi wakubwa katika mziki huo, walitoka kimziki kupitia baadhi ya mistari waliyoiba au ku copy kutoka katika nyimbo za mfalme huyo wa hip hop au rap. Na wasanii hao walioiba au ku copy kutoka kwa 2pac nimewaweka katika makundi matatu ya A, B na C.

A) Wapo waliotoka kwa ku copy au kuiba beat zake. Wasanii hao ni👇

1) Jay z ft Beyonce - 'Me and my girlfriend', Jay z aliu copy wimbo huo kutoka katika ile nyimbo ya 2pac ya 'Me and my girlfriend.'
Kwa wafuatiliaji wa mambo ya hip hop bila shaka washawahi kuzisikia nyimbo hizi. Na ikumbukwe kabla ya 2pac kufa, 2pac na Jay walikuwa na diss (ugomvi) ndo maana 2pac alimchana jay z live katika wimbo wake wa 'Bomb first'

2) Nas - huyu ashawahi ku copy beat ya 2pac afu akaingiza mistari ambayo ilikuwa imechanganywa na baadhi ya mistari iliyo katika nyimbo za 2pac (wimbo nimeusahau) Lakini tofauti na wasanii wengine, Nas ali copy nyimbo ya 2pac huku 2pac mwenyewe akiwa hai.
Pac alipotoka hospital baada ya kutolewa risasi tano alizopigwa, kitu cha kwanza alitunga nyimbo kuhusiana na tukio hilo la kupigwa risasi tano. Sasa baada ya siku chache baadae Nasi nae akatoa ya kwake inayolingana na ya Pac ikiwa na beat pamoja na ujumbe unaofanana na ule wa 2pac, jambo lililopelekea 2pac achukie na kutunga nyimbo ya kumpaka Nas mazima. Wimbo huo unaitwa 'Against all odds' 2pac alimpaka Nas, pamoja na Puffy Daddy live bila kumung'unya mung'unya maneno. Hapo chini naweka baadhi tu ya maneno katika verse ya kwanza akimchana Nas baada ya ku copy kutoka kwa 2pac 👇

🎶 This little nigga named Nas thinks he live like me, talking bout how he left the hospita took five like me.
You living fantasies, nigga i reject your deposit🎶 Kwa tafsiri isiyo rasmi (Huyu dogo anaeitwa Nas anafikiri anaishi kama mimi, anaongelea kuhusu kutoka hospital baada ya kupigwa risasi tano kama mimi.
Unaishi kwa nguvu za soda dogo, nigga sikubaliani na kile ulichoimba) hapo chini aliendelea kumchana kupitia verse ya mwisho ya wimbo huo 👇

🎶 Hey Nas you whole damn style is weak you heard my melody, read bout my life in the papers.
All my run-in with authorities felonious capers now you want to live my life, so what's the deal niggas that don't ride right.
You've seen too many movies, load em up against the wall, close his eyes since you lie, you die, goodbyee.
Let the real life niggas hear the truth from me,
What would you do if you was me nigga (against all odds)

B) wapo waliotoka kwa ku copy tu mistari yake, wasanii hao ni 👇

1) 50 Cent - hail marry, wimbo huu 50 alikuwa akim diss Ja rule, kuna baadhi ya maneno mengi katika verse yake aliyatoa kwenye wimbo wa 2pac wa Against all odds. Ngoja nitawawekea mistari ya 2pac na 50 cent hapo chini muone ninachomaanisha 👇
Verse ya 2pac 👉 🎶 This little nigga named Nas thinks he live like me, talking bout he left the hospital took five like me.
You living fantasies, nigga i reject your deposit.
Verse ya 50 cent 👉 🎶 Lil nigga named Ja (Ja rule) think he live like me, talking bout he left the hospital took nine like me. You living fantasies, nigga i reject your deposit.

2) Eminem nae hakuwa nyuma kwenye wimbo huo akaimba baadhi ya mistari ya verse kwenye nyimbo husika wa 2pac (kabla ya hapo Eminem alikuwa anaimba rap katuni, ile ya uchale chale) kwa wafuatiliaji wa ngoma za Eminem kuanzia mwaka 2012 kushuka chini wanafahamu ukatuni wake 😂😂😂😂.

3) Lil Wayne huyu nae ashaiga mengi mpaka kupelekea kutunga nyimbo inayofanana na ya 2pac, alipohojiwa na yeye alieleza jinsi anavyomkubali na kumheshim 2pac hadi kupelekea kutunga nyimbo inayofanana na ya 2pac inayoita 'Keep ya head' wimbo huu 2pac alikuwa ameutunga mahsusi kwa wanawake.
Hili kundi 'B' wapo wengi ila kwa kufupisha mada acha niishie kwa hao wawili.
C) Wapo waliotoka kwa ku copy style ya maisha ya 2pac, aidha kwa kutembea kama Pac, kuvaa kama Pac, kuchora tattoo zinazotaka kufanana na za Pac nk.

Muda kidogo nitakuja na baadhi ya wasanii wakubwa walio copy style hizo nilizoandika hapo juu. Hii inaonesha ni jinsi gani mfalme huyo wa hip hop anavyoheshimika na kukubalika kuliko msanii yeyote wa mziki huo na ndio maana wengi wametoka kupitia nyimbo zake na style zake.

Baada ya picha ya Nas akionesha heshima (respect) na utiifu kwa Pac kwa kuvaa t-shirt yenye picha ya Pac pamoj na kitambaa cha kichwani. Hapo chini kabisa nimeweka video ya Em na 50 wakionesha na wao utiifu wao kwa King (mfalme) wa Hip Hop 2Pac Amaru Shakur ambae ndio nembo kuu ya mziki huo kama ilivyo kwa Bob Marley Reggae au Michael Jackson Pop.

Kama mtu hafamu lugha ya malkia waliyotumia kina Em na 50 Cent ni bora atafute wa kumtafsiria ili awe na uelewa wa kile kilichozungumzwa na wasaani hao wawili wakubwa wa Marekani kuhusu King wao. Najua wapo watakaopinga lkn hii haiwezi kuondoa ukweli maana kila kitu kipo wazi kupitia kauli zao, mavazi yao, tatoo zao na nyimbo zao.

Pac For Life
images (13).jpeg
images (11).jpeg
 

Attachments

  • images (29).jpeg
    images (29).jpeg
    33.7 KB · Views: 74
  • Eminem 50Cent Interview after 2Pac Death - McMigxeRap.mp4
    9.7 MB
ile michano kwenye HIT EM UP daaa !!! jamaa alikuw mhuni vibaya mno.sio hawa marapa wakiwa wanakuchana wanaficha ficha unabaki unajiuliza kanichana mimi au kamchana fulan

sasa mwamba yeye alikuwa anaanza na jina la mhusika ,halafu zinafuata mazafacka sasa

na ndivyo maisha yanavyotakiwa yawe,nikikosea nichane sio kuniwekea mafumbo kama hawa marappa wa kibongo.
 
SEHEMU YA PILI INAENDELEA HAPO CHINI

2Pac kabla hajapigwa risasi mwaka 94 alikuwa na urafiki wa karibu sana na msanii ambae mwenyew alikuwa anamwita mdogo wake. Huyu sio mungine bali ni Notorious B.I.G wengi walizoea kumwita Big, Big poppa au Big small. Ilifikia kipindi mpaka 2pac akawa akimpa Big mic na yeye achane kwenye shoo mbali mbali ili kumpa jina. Lkn kama hiyo haitoshi 2pac akashirikiana na Big kwenye baadhi ya nyimbo zake. Ila urafiki wao uliingia dosari mwaka 94, baada ya 2pac kupigwa risasi katika gorofa 1 ambalo juu ya gorofa hilo ndipo ilipokuwa studio ya bad boyz ambayo Big alikuwa akiifanyia kazi. Inasemekana 2pac alikuwa anaenda kumtembelea mshikaji wake Big (ikumbukwe 2pac muda huo alikuwa akiishi Los Angeles CA) lkn kila alipokuwa akienda New York kufanya kazi zake alikuwa ni lazima akamuona rafiki yake Big ambae. Sasa siku hiyo alipofika kwenye ghorofa hilo lenye studio za kina Big, wakati 2pac akijingia kwenye lift akakumbana na vijana watatu ambao walimtolea gun (pisto) na kutaka awape kila alichokuwa nacho, yani cheni yake ya dhahabu, pete zake za dhahabu alizovaa videle vyote, ring ya dhahabu ya mkononi na fedha alizokuwa nazo. Kitendo kile 2pac hakukubaliana nacho kuibiwa kindezi japo jamaa walikuwa na gun, ikabidi 2pac atake kuwahi kutoa gun yake aliyokuwa nayo ili awadondoshe wao, kwa bahati mbaya jamaa wakamuwahi kwa kumpiga risasi tano, wakachukua vitu vyote walivyokuwa wamemuomba pamoja na ile pisto yake wakasepa navyo. Pac alipokuwa hospita mpaka anatoka hakupokea call yoyote kutoka kwa Big ya kumpa pole nk. Jambo hilo lilimfanya Pac ahisi kuwa huenda wale jamaa walitumwa na Big, na ukizingatia kabla ya kuja Pac alimjulisha kwa sim Big kuwa baada ya dakika kadhaa atakuwa ashafika pale kwenye studio yao.
Hiyo tisa ikapita, kumi ni pale Big alipotoa ile nyimbo ya Big Poppa ambayo ilitungwa na 2pac huku akiwa amempa Big verse 1 aimbe, ila kwa bahati mbaya kabla hawajaenda ku rekodi Pac akakamatwa na kufungwa. Wakati Pac yuko jela Big akaingia studio na kubadilisha kiitikio kisha kuweka verse zake na za 2pac kwa kutumia sauti yake mwenyewe. Kitendo kile kilimuumiza Pac kwani hakutegemea kuwa rafiki yake wa karibu angefanya yale aliyofanya kwake. 2pac alipotoka kupitia vyombo vya habari akamuahidi Big kuwa na yeye atamfanyia kitu ambacho kitampa maumivu zaidi ya maumivu yote akiyowahi kupata maishani kwake.

Wakati Big akitafakari ni maumivu gani hayo ambayo Pac atampa, Pac akatumia utaalam wake na ulimi wake mzuri katika kutunga nyimbo mbali mbali kumtongoza mke wa Big Faith Evans, dem nae kumbe toka kitambo alikuwa anamzimikia Pac lkn alikuwa anashindwa kumwambia shemej yake (2pac) ili asije kumwambia mume wake (big) Kwahiyo Pac alivyogusa tu ikawa kama mlevi aliekanyaga ganda la ndizi sakafuni, demu akaingia mazima. Pac akala tunda kimasihara, ila kwa malengo ya kumuumiza tu Big, akawa kila akitoka nae anamchukua picha, baada ya kuona tayari ameshapata alichotaka sasa akaenda kwenye media na kuwapa zile picha mbali mbali za yeye (2pac) na Faith Evans (mke wa Big)

Media kama kawaida wanataka wauze magazeti na habari mbali mbali, kesho yake wakatoa magazetini, redioni, kwenye tv nk. Wakati Big akiwa amechanganyikiwa jinsi demu wake alivyoweza kuingizwa 18 na Pac hadi kumvulia pichu, tena katika kipindi ambacho anajua kuwa ana ugomvi nae, ghafla akasikia 'Hit Em Up', iko hewani vituo vyote vya redio, tv na magazeti vinareport kuhusu wimbo huo uliomuacha uchi Big. Big akachanganyikiwa maradufu asijue cha kufanya, na hapo sasa ukawa mwisho wa uvumilivu wake kwa mkewe, so akaamua kuvunja ndoa na mke wake japo bado alikuwa anampenda.
Baadi ya mistari ya 2pac kwenye verse ni ilikuwa ni kumjulisha Big kuwa mkewe ashamla tunda kimasihara 👇
🎶Big you claim to be player but i f...k your wife.🎶
Picha hapo chini mtoto ashapewa mti wa maana na 2pac (real G) hadi jicho limeregea.
 

Attachments

  • images (15).jpeg
    images (15).jpeg
    42.8 KB · Views: 69
  • images (14).jpeg
    images (14).jpeg
    53.3 KB · Views: 65
  • images (19).jpeg
    images (19).jpeg
    35.2 KB · Views: 66
Tukiacha na hayo ya 2pac & Big.

Hawa chini ni wasaani ambao wameiga life style ya 2pac achilia mbali kuiga uimbaji wake, kurudia verse zake nk.

Picha namba 1 hapo 👇 Ja rule hapo chini akiwa amechora tatoo ya nyuma ya mgongo kama alivyokuwa amechora 2pac. Kwahiyo picha ya juu kulia ni 2pa, na picha ya chini kushoto ni Ja rule. Afu hiyo ya full upande wa kushoto ni ya 2pac mwenyewe.

Na picha namba 2 hapo ni Busta Rhymes na yeye hakuwa nyuma katika kuiga. Kama inavyoonekana hapo kulia juu ni picha ya 2pac, kulia chini ni Busta Rhymes na full upande wa kulia ni 2pac mwenyewe.
 

Attachments

  • IMG-20221027-WA0015.jpg
    IMG-20221027-WA0015.jpg
    93.4 KB · Views: 69
  • IMG-20221027-WA0014.jpg
    IMG-20221027-WA0014.jpg
    96.4 KB · Views: 62
R'Kelly yeye anasema alipomuona 2pac huko LA, akaanza kupiga kelele ya kumwita 2pac huku akimkimbilia (fikiria msanii kama R'Kelly na umaarufu wake lkn anamkimbilia 2pac huku anampigia yowe ili ageuke kumsalimia 😂😂😂) hili alikiri mwenyewe R'Kelly alipokuwa anahojiwa.

Lil wayne nae hakuwa nyuma, japo hakuwepo lkn amejitahidi na yeye kuchukua kadhaa kwa 2pac ili mziki wake ueleweke
 

Attachments

  • Screenshot_20221027-164830.jpg
    Screenshot_20221027-164830.jpg
    63.6 KB · Views: 59
  • Screenshot_20221027-171424.jpg
    Screenshot_20221027-171424.jpg
    61.7 KB · Views: 57
2pac ameacha alama kubwa katika mziki wake ikiwepo ile nyimbo yake ya 'Dear mama' na 'Change' ambazo alipewa zawadi na raisi wa kipindi hicho Bill Clinton. Lakini pia amekuwa kama ndio alama ya mziki wa hip hop ulimwengu. Ana mengi mno aliyofanya katika mziki huu ambayo mtu hauwezi kuelezea ukayamaliza. Labda nimalize kwa kuweka picha za watu ambao wameamua kuchora mpaka tatoo za 2pac kwenye miili yao.

Hapa mwana basketball mkubwa Marekani aliamua kuchora tatoo ya 2pac kwenye mguu wake kuonesha heshima kubwa aliyonayo mwana hip hop huyo na mtetea haki za watu weusi Marekani.

Wengine wanaofatia chini sitaandika majina bali nitaweka tu picha zao ambazo wameonesha heshima na kumkubali mfalme huyo wa hip hop
 

Attachments

  • Screenshot_20221027-165345.jpg
    Screenshot_20221027-165345.jpg
    67.2 KB · Views: 51
  • Screenshot_20221027-165219.jpg
    Screenshot_20221027-165219.jpg
    55.8 KB · Views: 52
Kidada Jonas huyu alikuwa fiance wake ambae walikuwa wanatarajia kufunga nae ndoa, na ndo walikuwa wote usiku ule wa 2pac kupigwa risasi
 

Attachments

  • images (20).jpeg
    images (20).jpeg
    16.7 KB · Views: 57
  • images (24).jpeg
    images (24).jpeg
    36.8 KB · Views: 59
  • images (25).jpeg
    images (25).jpeg
    26.6 KB · Views: 54
  • images (26).jpeg
    images (26).jpeg
    31.4 KB · Views: 54
Back
Top Bottom