Sikia hii ya mama Mkwe...UNGEFANYAJE HAPA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikia hii ya mama Mkwe...UNGEFANYAJE HAPA?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sizinga, Jul 25, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Hii nimeisikia leo Radio flani tanga:

  Kuna njemba moja alioa msichana mmoja mzuri tu, huyu dada mama yake alikuwa RPC(Mkubwa wa Polisi), ndoa yao ilifana sana. Baada ya miezi michache matatizo yakaanza katika ile ndoa. Yule binti akawa analalamika kwa mme wake kwamba kabadilika na mara nyingi huwa anarudi usiku sana, matunzo sio mazuri, muda mwingine hata fedha haachi.

  yule dada baadaya kuona hamna mabadiliko kwa mme wake akaamua kumshtaki yule jamaa kwa mama yake yule Polisi.(Mama Mkwe wa huyu jamaa). Kwa sababu mama mkwe anaheshima sana sehemu yoyote, basi busara ilitumika na yule jamaa akaitwa na Mama wa yule dada, jamaa akakalishwa chini na akaulizwa inakuaje siku hizi unarudi usiku sana na complain nyingine, jamaa akajitetea kwa kudai kazi tu nyingi kutafuta hela n.k, na akadai atajirekebisha, yakaisha.

  Sasa siku moja kutokana na utaratibu wa jeshi la Polisi kugundua wazamiaji, wakaamua kufanya utaratibu wa kukagua gesti za mtaani usiku(huyu mama akiwa ndio mkubwa wa msako), sasa guest walipoenda wakaamuru mapokezi kuorodhesha wageni wao walikuwa vyumbani, na badae kwa utaratibu wa kawaida wakaamua kupitia chumba hadi chumba kuuliza uraia wa wageni mule hotelini/guest.

  Sasa mlango wa kwanza kufungua jamaa uso kwa uso na mama mkwe, na alikuwa na kimwana ndani ya room, jamaa kutahamaki, mama mkwe...!!

  Kama wewe ungefanyaje hapo ilhali siku chache za nyuma umekalishwa chini na huyu mama.??
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ningejidai nimezimia baada ya kupata mshtuko.
   
 3. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii ni hatari kwelikweli! Unajua mama mkwe anaweza kumwek jamaa ndani kwa hasira kabla ya kufikiria namna ya kumwadhibu!
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Haa hii sasa kali, tutakupeleka ICU na mkeo atakuwa anakuhudumia.
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Hiki ndicho ilichokifikiria. sema utamsweka Lupango kwa kosa gani?
   
 6. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 3,999
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ...hahahahahahaha...Kosa..1..kukutwa nyumba ya wageni wakati si mgeni..
  Kosa...2..uzembe na uzururaji.(kumbuka ana kwake)
  kosa...3..kutembea nje ya ndoa..
  kosa...4..kumhatarishia mtoto wake..maambukizi ya v.v.u...
  hakukosi kweli hapo...eti mkuu...then anachanganya na adhabu zake...
   
 7. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Heheh anajifanya nae mgeni yani hamajawahi onana hata siku moja :biggrin1:
   
 8. GABOO

  GABOO Senior Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hapo hata ujiteteeje, lazima utakwenda na maji
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Unaukumbuka wimbo wa Shaggy, wasn't me halafu unaufanyia kazi!
   
 10. chavka

  chavka JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Najifanya simjui kabisa. walahatujawah onana najua hawezi kunitia ndani kwakuwa hatokuwa na uhakika na mm. pili hawezi kumwambia mwanae kama kanifuma gest. ila kiukweli baada ya hilo soo nitakuwa narudi home saa10 jioni maana hatwari
   
 11. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kwani utazimia siku zote? Na baada ya kuzinduka ukakuta mama mkwe yupo hapo hapo je? Utajidai umezimia tena?
   
 12. M

  Mpemba asilia Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Najifanya chizi natoka speed,naenda hosp naongea vzr na doctor ananiandikia nina malaria ya kichwani.kesho nikikutana na mamamkwe najifanya sikumbuki.eehh ila nikipona hapo sirudii tena.
   
 13. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,610
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Unazimia, afu ukizinduka unajifanya uko kwenye coma huelewi kitu wala huongei.
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hahahaha! Mamushka hiyo yako nimeipenda! Daaah, utabaki kwenye koma mpaka lini?..lol..
   
 15. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kuuwa so unamuomba mama mkwe mzigo
   
 16. serio

  serio JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  kosa 1 nomaa.,hahahaa
   
 17. Maayo

  Maayo JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa hapo mkuu unazima moto kwa petrol.
   
 18. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwa Tanga hilo si tatizo na haswa ukiwa dini fulani,na akiona ni tatizo kwa kawaida ya mama wa ki Tanga inabidi atafute jibu la kwanini hutosheki nyumbani mpaka unakwenda kula nje.
  Shida case ya hivyo ukumbane nayo Iringa au Tabora!
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mama mkwe hakukwenda kufumania yupo kazini kukagua uraia; nitajitambulisha haraka kama kaka yake Arafat nimekuja leo kutoka kijiji kuna pacha wangu anaitwa Arafat yupo hapa ameowa binti anayeitwa Fatuma mama yake nasikia ni RPC hapa nimekuja kuwatembelea niliambiwa kuwa wana matatizo mke wake alimshtaki kwangu sasa nimeigia usiku huu nataka kesho niende kuwasuluhisha na nitarudi kijiji kesho mapema na huyu niliye naye hapa ni mke wangu tumekuja pamoja kwa ajili ya hayo matatizo ya mdogo wangu, maana pia mke wangu ni mtu mzuri sana katika Nasaa za ndo kwasababu ni Mlokole wa kwa Kakobe kule kijijini kwetu amekuja kwa ajili ya kuwaombe hawa wanaondoa, je mna maswali mengine kama hamna tunaomba tulale sisi tumechoka sana na usafiri wa shida na hili giza la Ngereza.
   
 20. Maayo

  Maayo JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Umewahi kutunga novel we? Maana stori yako imeniacha mbavuless!! Ha! ha! ha! haaaa!
   
Loading...