Sijui tumemkosea nini jirani yetu

Sijui tumemkosea nini jirani yetu

graxana

Member
Joined
Nov 7, 2015
Posts
58
Reaction score
23
Wana JF habar zenu.

Naishi na familia yangu,miaka minne iliyopita tulihamia kwenye nyumba yetu hapa Dar.

Jirani yetu alitupokea kwa furaha na kutuambia habar za mtaa mzima,alituambia pia watu ambao yeye hawapend hatak tuongee nao.

Siku zinavyozidi kwenda tunatokea kuwazoea majirani wengine zaidi yake, kitendo hicho kimemuudhi na amegeuka adui yetu balaa, amewekea sumu mifugo yetu kuku na paka tuliye kuwa tunafuga wamekufa.

Kuna siku alikuja na mganga kwake tukashangaa kuku wetu mweusi haonekani na manyoya yapo shimon pake, bata wetu wakipita uwanjani kwake anawakata miguu.

Yaani tunaimbiwa taarab kila siku,alishawah kumvuta mdogo wangu kwake na kumng'ata begani mpaka tukampeleka hospital.

Akifagia kwake uchafu anatupa upande wetu coz sisi tupo chin yake kidogo,tumemripot police na kwa balozi mara kadhaa ila hatuoni hatua zozote zikichukuliwa,na hii inatuogopesha sababu anatumia had watoto wake kuwaumiza wadogo zangu na kutuibia mifugo yetu maskin tumepaki na vifaranga tu.

Naombeni ushauri.
 
Last edited by a moderator:
OMG !! pole saaaannaa !! Jee Nikupe dawa ya " HaL badirii "??
au msamehe bure ...maana yaonesha hana uhai mrefu huyo yupo trminal (karibu atapotea) !!
 
Wana fj, habar zenu,,
Naishi na familia yangu,miaka minne iliyopita tuliamia kwenye nyumba yetu hapa dar..jiran yetu alitupokea kwa furaha na kutuambia habar za mtaa mzima,alituambia pia watu ambao yeyehawapend hatak tuongee nao. Siku zinavyozid kwenda tunatokea kuwazoea majirani wengine zaid yake, kitendo hicho kimemuudhi na amegeuka adui yetu balaa,, amewekea sumu mifugo yetu kuku na paka tuliye kuwa tunafuga wamekufa,, kuna siku alikuja na mganga kwake tukashangaa kuku wetu mweusi haonekani na manyoya yapo shimon pake, bata wetu wakipita uwanjani kwake anawakata miguu,yaan tunaimbiwa taarab kila cku,alishawah kumvuta mdogo wangu kwake na kumng'ata begani mpaka tukampeleka hospital,akifagia kwake uchafu anatupa upande wetu coz ss tupo chin yake kidogo,tumemripot police na kwa balozi mara kadhaa ila hatuon hatua zozote zikichukuliwa,na hii inatuogopesha sabab anatumia had watoto wake kuwaumiza wadogo zangu na kutuibia mifugo yetu maskin tumepaki na vifaranga tu ..naombeni ushaur
Ni kumtokea na panga tu na kumuwasha za mashavuni, alafu hapohapo unaandaa hela ya kuwahonga polisi
 
Binafsi nilipohamia kwangu niligundua kuna ethics za kuishi nyumba yako binafsi na nyumba za kupanga, kwanza nyumba ya kupanga unaweza ukaweka kufuli ukasafiri hata mwezi lakini nyumba yako binafsi huwezi fanya hivyo, yumba ya kupanga unaweza ukawa unamkaribisha jiran mnapiga stori then anaondoka lakin nyumba yako binafsi usimkaribishe jiran akapazoea kwako n.k ulichokifanya wewe ulipeleka habari za uswazi kule ulipohamia (nyumbani kwako) hapo ndipo shida ilipoanzia
 
Wana JF habar zenu.

Naishi na familia yangu,miaka minne iliyopita tulihamia kwenye nyumba yetu hapa Dar.

Jirani yetu alitupokea kwa furaha na kutuambia habar za mtaa mzima,alituambia pia watu ambao yeye hawapend hatak tuongee nao.

Siku zinavyozidi kwenda tunatokea kuwazoea majirani wengine zaidi yake, kitendo hicho kimemuudhi na amegeuka adui yetu balaa, amewekea sumu mifugo yetu kuku na paka tuliye kuwa tunafuga wamekufa.

Kuna siku alikuja na mganga kwake tukashangaa kuku wetu mweusi haonekani na manyoya yapo shimon pake, bata wetu wakipita uwanjani kwake anawakata miguu.

Yaani tunaimbiwa taarab kila siku,alishawah kumvuta mdogo wangu kwake na kumng'ata begani mpaka tukampeleka hospital.

Akifagia kwake uchafu anatupa upande wetu coz sisi tupo chin yake kidogo,tumemripot police na kwa balozi mara kadhaa ila hatuoni hatua zozote zikichukuliwa,na hii inatuogopesha sababu anatumia had watoto wake kuwaumiza wadogo zangu na kutuibia mifugo yetu maskin tumepaki na vifaranga tu.

Naombeni ushauri.
Jaribu kuweka uzio huenda ikasaidia. Pole sana kwa hayo majanga.
 
Kwa nin mlianza kuongea na watu ambao yeye hawapendi.kumbe mlitaka wenyewe mana mlikiuka masharti
Utawezaje kuishi unaongea na mtu mmoja mtaani, coz yeye amegombana na karibia majiran wote, na ss ndo tunapakana nae kabisa,pia sisi hatujui ugomvi wao umeanzia wap, utaanzaje kuacha kuongea na mtu kwa sababu ya ugomvi usikuhusu na wala hauujui??
 
Pole binadamu wengine vigumu kuwaelewa ikiwezekana weka uzio zuia watoto ndugu kwenda kwake na mambo yako yawe yako wala usipende kumfwatilia
 
Pole sana mkuu cha kufanya hakuna haja ya kugombana nae ww mpuuzie hata kama akitupa matakataka we Piga kimya akimpiga mdogo wako usimulize omba mungu upate hela uweke ukuta mrefu ila nakushaur acheni maneno na kushtakiana mpuuzien tu huyo boya.
 
Hao majiran wapo, utakuta kashakosana na mtaa mzima, unapohamia anakuwa karibu na wewe ili uwe upande wake ukimzoea unamuona sio, ukishaanza kukaa pemben inakuwa taabu kweli! Dawa hapo n kujipanga na kuweka ukuta then zinabaki salam tu no more no less
 
Wewe kwa nn ulianza kuongea na maadui zake? Mtu akiwa rafiki wa adui yako inamaana na yeye ni adui yako pia , ndio principles zisemavyo..

Ila kwa ushauri tu ungeweka fence kubwa ya kutosha na kila mtu aendelee na maisha yake , mimi sijui watu mnaishije bila fence. Mm kwa maisha niliyokulia mpaka sasa , ni bora nikawa na fence ila nyumba ikawa ya namna yoyote , au nikawa sina nyumba ila nikawa na fence...
 
Pole sana. Kudeal na MTU wa namna hiyo itabidi uwe na roho ngumu tu
 
Wewe ni kibonde kiasi hicho? Una moyo mkubwa kama wa tembo yote hayo umefanyiwa ukayavumilia? Grow up! be a man kabla hajakudhalilisha siku moja atakukata vibao mbele ya mkeo na watoto wako!
 
Back
Top Bottom