Habari wana jamvi. Juzi katika mizunguko yangu mjini nilikutana na binti mmoja hivi mwanachuo. Kwa kumtazama kwa haraka haraka nikagundua hakuwa sawa. Kibinadamu nikamsogelea nikaanza kumsaili japo nwanzoni alitia ngumu kidogo. Badaye alinieleza kila kitu (kuhusu kutokuwa kwake sawa) nikaamua nimsaidie maana matatizo yenyewe yalikuwa madogo kwa upande wangu.
Baada Ya kuwa nimemtatulia shida zake ikabidi tukae sehemu kwa ajili ya kufahamiana vizuri. Mwisho Tukapeana namba za simu tukaagana.
Toka siku ile huyu binti amekuwa ni msumbufu wa kiwango cha dunia. Ananipigia simu mpaka saa Saba Usiku ananiuliza nimelala na nani wakati hakuna uhusiano wowote Kati yetu ambao kwa namna moja au Nyingine ungepelekea kuulizana maswali kama hayo. Meseji za miss you toka kwa huyu binti zimekuwa kero, kwa siku anaweza tuma hata kumi.
Huyu binti nilimsaidia kama ambavyo ningesaidia mtu Mwingine ila yeye msaada wangu aliupokea tofauti kabisa na naona anataka kunipa takrima ya kile kiungo pendwa kilichopo mubashara chini ya kitovu chake.
Kiukweli nimejitahidi saana kumpotezea ila kila ninvyompotezea ndivyo anavyoongeza juhudi. Akiendelea itabidi nichague moja Kati ya haya mawili; NIMTAFUNE au NITOE NAMBA YAKE LOVE CONNECT NISAIDIWE.