Wakuu hapa majuzi kati wakati natoka job naelekea hom majilan fulani hivi ya jion nipo zangu kwa miguu
Mara Kigari kikanipigia honi na kusimama kikitoa ishara niende
Basi nikasogelea hadi hapo
Nilivyo fika pale kuangalia kwenye hiyo gari nimekutana na mmama
Akaniuliza unaelekea wapi nikajibu hom
Akaniomba nimpe kampani kwa kupanda gari yake mzee mzima ni kapanda basi stoli za hapa na pale
Zikaendelea mwisho wa siku tukafika maeneo nikamwambia niachie hapa tukaagana vizuri
Nilichoshangazwa jana katuma text kaka nipigie alafu nikichek namba ngeni nikapiga akajitambulisha mi mtu flan nakuanza kunipa sifa kedeked afu akakata simu
Sikupata muda wa kumuuliza namba umepata wap maana sikuwahi kumpa
Leo tena kanichek kaniuliza uko wapi nikajibu hom akaniambia kaka nina shida nikamuuliza shida gani akasema wewe mtu mzima bhana chukua boda au tax njoo hom utakuja kujua
sasa hapa nipo njia panda sijui niende au nimpotezee ?
Kwenu wakuu
Wazee wa uzi bila picha haunogi ila Baadhi ya text-



nimefuta
View attachment 2047675