Sijui nifanyeje juu ya Jambo hili

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Mwaka 2018 kuna mwanamke nilikutana naye kwenye Facebook. Yeye alikuwa TZ mimi Canada. Tukaanza kuwasiliana kama marafiki tu mpaka mwaka 2019 tukaanza mausiano tulitokea kupendana saana na mwanamke huyu.

Mpaka nikaomba sapoti kwa ndugu zangu wanisaidie ili nipate kumuoa na kumleta uku
Lakini kwa bahati mbaya mambo yakawa mabaya upande wa familia yangu maana walimkataa binti huyu kwasababu zao wanazo zijua wenyewe.

Mimi sikukata tamaa nilipambana nikapata nauli ya kwenda Afrika kuonana naye. Nilivyo fika Afrika kwa bahati nzuri nilipata kukutana naye akanitambulisha kwa ndugu zake.

Baada ya mwezi mmoja nikiwa Afrika nikaona siwezi kurudi Canada bila kufunga naye ndoa ili nipate documents za kwenda kufanya declaration ya kumpeleka Canada kama mke wangu halali.

Wazo hili nilishirikisha ndugu kwa bahati mbaya tena wakanikataa kabisa nikafanya mambo kwa kushirikiana na marafiki zangu wa Canada wakanipa sapoti nikabahatika kuweka kidogo ya pesa kwao na binti na kufunga naye ndoa ya serekali Alafu tukafanya na kasherehe kidogo

Mimi nikarudi nyumbani nilijikuta na tengwa na familia kwa mambo ambayo nilienda kufanya afrika mimi wakanikosesha amani wakatafuta namba za binti huyo wakaanza kuongeya naye kwa kumtukana kuwa ameniroga sijui mambo mengi saana.

Nilijaribu kuwaomba sababu za wao kunikatalia kuoa binti huyo nilikuta ni sababu za kibaguzi tu kisa binti ni mtanzania mimi mkongo ndo maana familia hawakupenda mimi kuoa binti huyo

Baada ya kuona Sina amani na familia nikaona nijitenge na huyo mwanamke
Nikaamua kuachana na mwanamke uyo

Toka nijitenge na binti huyo kwasasa tuna miaka 3 lakini bado akili zangu zinagoma kuondoka kwake
Na nikisema ni mfanyie mchakato wa kumleta uko bado immigration watahitaji saini za Wazazi wangu tu ili kukamilisha mchakato mzima hapo ndipo kuna ugumu

Sijui nifanyeje
 
Afrika ndo wapi huko?
 
Najaribu hata kuconnect dots lakini bado sielewi uyo ana maana gani au ni wawapi
 
Back
Top Bottom