vyote vinafanya kazi sambamba ndo maana ukioa lazima uwe umejiandaa na ni muhimu kufanya kitu unachojisikia ukiona ujapata hamu ya kuoa ujue may be muda wako bado
nyooo miaka Tisa nabembeleza ndoa bado MTU anasema bado ...keshokutwa anakuja kukuletea kadi ya harusi anaoa...wakati Mie nshaanza kupata makunyanzi...
utazirudisha siku nyuma au?
Aisee Huyo binti atakua ana mdudu kichwani.
changamoto hii...kumpoteza mtu mliyekuwa na mahusiano ya muda mrefu hivyo si vizuri,halikadhalika kuingia kwenye ndoa pasipo maridhiano ya pamoja si jambo jema...nadhani mmojawao ajishushe na kuangalia mazuri ya hitaji la mwenzie,,kupitia hayo yanaweza mjengea mtazamo wa kukubaliana...yaweza kufunga ndoa isiwe sasa,lakini pia si kufika muda wa miaka minne...mwanamke anasema umri wake wa kuwa na mtoto umefika anataka azae akiwa kijana mwenyewe nguvu hataki kuja kuzaa wajukuu kimsingi jamaa anamuona mdada bado muda anao wa kutosha anaisi labda kuna external force ndo maana mdada kachachamaa
mbona unaongea as if ni kitu cha upande mmoja sijakupata point yako
Hahahaaaaa very interesting
Jamaa kanogewa na uhuru wa kifedha na kimaisha Kwa ujumla. Anaona ndoa itamfunga kitanzi ashindwe kula bata angali bado ana Miaka miwili tu kazini. Ndio shida ya kuchelewa kushika hela
Mwambie kuwa ndoa haito mzuia kula ujana, ni makubaliano tu ya namna mtakavyo ishi kwahiyo aache kumtesa mdada wa watu. Akizubaa anaolewa huyo na ataanza kuhangaika kujenga mahusiano mapya na mwanamke mwingine
sidhani kama hilo neno "hamu" umelitumia kwa usahihi maana kama unasubiri hadi upate hamu ya kuoa au ya kuwa na mtoto basi kuna tatizo, je hio hamu isipokuja kabisa ndio ndoa hamna?? Sio justication nzuri kwa mtu mwenye upeo mwema, ujana una mwisho, kesho inakuja, kama unataka kumuoa heri muaone saa hizi.
changamoto hii...kumpoteza mtu mliyekuwa na mahusiano ya muda mrefu hivyo si vizuri,halikadhalika kuingia kwenye ndoa pasipo maridhiano ya pamoja si jambo jema...nadhani mmojawao ajishushe na kuangalia mazuri ya hitaji la mwenzie,,kupitia hayo yanaweza mjengea mtazamo wa kukubaliana...yaweza kufunga ndoa isiwe sasa,lakini pia si kufika muda wa miaka minne...
Na inakuaje ukajisikia kabla hujajiandaa?
Usipomaliza kujiandaa inakuaje; kujisikia kutakoma au hakutakuja kabisa?
Kwani hisia za kuoa zinaletwaga na nini?
Usipojiandaa kwa wakati inakuaje wakati Binti wa watu umemuweka pending anasubiri tu hapo?
Ina maana walioko tayari ila hawajaoa wanasubiri wajisikie?
Vipi wale waliooa ila hawajisikii kuoa imetokea nini? Huko ''kujisikia'' kuna beba uzito gani kwenye maisha ya mume na mke? Mbona anajisikia kwenda kunywa maziwa tu bwerereeeeeeeee??
NB: Lengo langu sio kupata majibu, ila uone/ufikiri zaidi ya unachokisoma.
you threating him
utaona bila kuwa na utayari?
mkuu nikupata ila kuna tofauti kubwa sana kuoa na kunywa mazima ,kunywa mazima hata watoto wa secondary wanaweza ila step ya kuoa unatakiwa kujipima vya kutosa kuanzia mind yako hadi saikolojia